General Tyre: Is it a slow death to a once an East Africa Giant??

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
19
Salaam wanaJambo wenzangu. Nilitokea kupita mitaa ya Arusha siku chache zilizopita na kwa mshangao wangu mkubwa nikakuta kwamba kiwanda cha General Tyre (Njiro Area) kimefungwa.... Nilifanikiwa kuulizia juu juu (habari za mitaani) nikaambiwa kwamba kiwanda kimefungwa sababu wameshindwa kulipia bili za umeme na wamekatiwa umeme.

WanaJambo wenzangu, General Tyre ya miaka ile (wakati kila gari lilikuwa linavaa chapa jenerali) leo tunaambiwa kimeshindwa kazi sababu ya kushindwa lipia umeme??? Mimi nadhani mojawapo kati ya haya yametokea:

1. Ulaji kama ilivyo katika makampuni yetu makubwa!
2. Upinzani wa kibiashara kutoka katika makampuni kama Fireston (Kenya), Yana (TZ) na ya kiChina kumelisababisha kampuni letu kubwa kushindwa pambana!
3. Ni mbinu ya kulifanya shirika lionekane halina faida ili lisukumwe kwa bei ya kutupa!

Kulikoni General Tyre? Wenye data hebu tuambieni jamani....
 
Wakuu hii nilikuwa nimeiweka humu jamvini miezi kadhaa iliyopita kuhusu hiki kiwanda chetu.... Leo naona kwenye press kuwa eti kumbe kilifungwa since last year na sasa hata meneja alikuwa analipwa kukaa bure (tena ni Mnepali huyu.......... I reserve my comments)......

Hebu angalia hii ya leo manake kwa kweli inauma sana... kwanza naglia wafanyakazi, angalia reasoning ya kushindwa kuzalisha, angalia rasilimali za kiwanda....

Jamani, ni laana au ni ule usemi wa Nyani Ngabu...... (I am still in denial though!!!)

Wafanyakazi General Tyre wamtisha Shelukindo

na Mustafa Leu, Arusha

WAFANYAKAZI 400 wa kiwanda cha kutengeneza magurudumu ya magari cha General Tyre cha mjini hapa, wamemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho, William Shelukindo, kutekeleza ahadi yake ya kuwalipa mishahara yao ya miezi sita, vinginevyo watamfungia kiwandani hapo.

Wafanyakazi hao walitoa madai hayo jana katika kikao chao kilichofanyika kiwandani hapo, kikishirikisha viongozi wa juu wa kiwanda hicho kujadili hatima ya kulipwa mishahara yao na masilahi mengine, yaliyokwama kwa kipindi cha miezi sita sasa.

Wakati wafanyakazi wakijiandaa kuchukua hatua ya kumfungia kiwandani mwenyekiti wa bodi endapo atakuwa hana jibu la msingi kuhusu malipo yao,
Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Deven Lohan, alisema yuko mbioni kubwaga manyanga na kurejea kwao nchini Nepal, ifikapo Mei 28 mwaka huu kutokana na kiwanda kutokufanya kazi.

Katika kikao chao hicho, wafanyakazi walidai kuwa hawajalipwa mishahara yao kwa muda wa miezi sita sasa,
kutokana na kiwanda kusitisha uzalishaji, hali ambayo inawafanya kuishi katika mazingira magumu.

Wafanyakazi hao walisema kwamba juzi ilikuwa walale kiwandani hapo kushinikiza serikali kuwalipa mishahara yao, lakini baada ya mazungumzo na uongozi wa kiwanda hicho kupitia kwa
Meneja Utumishi, Philip Mweta, waliahirisha zoezi hilo na sasa wanasubiri utekelezaji wa ahadi ya Shelukindo.

Walisema kuwa Shelukindo aliwaahidi kwamba mishahara italipwa Mei 28 mwaka huu, hivyo waliombwa kuvuta subira na ndiyo maana wakaahirisha zoezi la kulala kiwandani hapo.

Walisema wao sasa wanaishi katika mazingira magumu huku baadhi yao wakigeuka kuwa omba omba kwani wanashindwa kulipia gharama za matibabu, kodi za nyumba na ada za shule.

Kiwanda hicho pekee nchini kilisitisha uzalishaji
Agosti 24 mwaka 2007 na kuanzia wakati huo wafanyakazi wake hawajalipwa mishahara ingawa bado hawajafukuzwa kazi.

"Iwapo kama hatutalipwa mishahara yetu tarehe hiyo waliyoiahidi tutakifunga kiwanda hiki, uzalendo umetushinda, hatuwezi tena kuvumilia wakati tunakabiliwa na matatizo kibao," alisisitiza mmoja wa wafanyakazi hao.

Wafanyakazi hao walisema kuwa kiwanda hicho bado kina uwezo wa kuzalisha magurudumu na kuhimili ushindani wa kibiashara na kuwa hakijafikia hatua ya kushindwa kuzalisha, bali tatizo kuna hila zinazofanywa na baadhi ya viongozi za kukihujumu ili kionekane hakifai ili kiuzwe.

Kiwanda kina mashamba makubwa ya mpira katika mikoa ya Tanga na Hai, mkoani Kilimanjaro.

Courtesy:
Tanzania Daima, 22/05/2008
 
Kila sehemu ni kilio cha kuliwa mali ya umma, lazima watafute njia ya kukiuza kwani hata NBC iliuzwa kwa kulazimisha kuwa ni benki kubwa sana haiwezi kuendeshwa kumbe walitaka kufisadi.

Wawaachie wafanyakazi waendeshe wenyewe badala ya kukiujumu ili wapate nafasi ya kukiuza.
 
General Tyre imeliwa na wakubwa, ma big boss.

Miaka kadhaa ya nyuma walipata mkopo kutoka NSSF wa bilioni 10 ukawa guaranteed na Waziri wa Pesa wakati ule bwana Basil Pesambiri Mramba. Akaitwa Lobbist kutoka Sauzi, akaandika pepa ya kulobbi wakati pesa wameshapata. Akalipwa Bilioni yake (10%) akafutika! Hiyo ilikuwa dili ya kwanza ya kupiga panga hizo pesa.

Mramba akarudishiwa fadhila, akafunguliwa kituo cha watoto yatima kule Rombo kwa ukarimu wa General Tyre. Hiyo ilikuwa ni ule wakati wa uchaguzi wa 2005. Mramba akachekelea, haachi kukisifia kiwanda (ambacho hakizalishi) mpaka leo!

Mheshimiwa Shirima wa Precision ndiyo aliyesaidia mu-introduce CEO wa General Tyre (mhindi kutoka Nepal) kwa Pesambiri. Shirima akapewa tenda ya kuchimba visima vitano vya maji kwa gharama ya Milioni ishirini kila kimoja. Vikachimbwa viwili palepale kiwandani na vingine kwenye houses za wakubwa ambazo hata hivyo zilikuwa hazina matatizo ya maji!

Wakasema hayo mabilioni waliyokopa ni pesa za kununua mali ghafi ili kiwanda kianze kuchapa kazi. Tangu wakati ule Kiwanda hakijawai kuzalisha kwa mfululizo wa zaidi ya miezi miwili. Pesa inaliwa tu. Mkurugenzi kutoka Nepal akaanza kuonyesha vimbweka vyake. Akaleta ndugu na marafiki kutoka Nepal. Wamekodishiwa majumba ya gharama kubwa kwa hisani ya General Tyre. Wakapewa kazi pale kiwandani kama wataalam ambao wanajifunza utaalam. Wakawa kila wikiendi wanaishia Manyara mara Serengeti.

Safari za nje nazo zikaanza. Ananunua tanzanite kwa wamasai kwa bei poa na pesa za mkopo anapeleka Marekani kuziuza kwa bei mbaya. Hakai Arusha kabisa. Kila siku ni Dar ama majuu. Akienda Dar lazima apitie Zanzibar atanue siku kadhaa na machangudoa kwenye hoteli za kitalii ndio afike Dar. Akamfukuza mkewe aka-import malaya kutoka kwao nasikia alikuwa mnenguaji mahili huko Nepal. Huyu mama akawa anafanya shopping yake Nairobi na General Tyre inalipa kila kitu. Alipomchoka akamfukuza. Anachangia mamilioni shughuli zozote zinazoendeshwa na wahindi marafiki zake. Amefadhili sana mbio za magari wakati matairi ya General Tyre hayashiriki. Amefadhili wapanda baiskeli ndugu zake wa kinepali wanaozunguka dunia nzima kwa baiskeli. Akiulizwa kwanini anatoa mamilioni kila siku bila mpango anasema anajenga PR.

Nasikia ni mtu mkubwa sana pale Legions Club Dar es Salaam. Akiingia klabu watu wote wanaacha kununua pombe maana yeye ndiyo 'spender' hiyo siku. Amewanywesha mawazilri na vibosile wote pale Dar es Salaam. Naona wanaogopa kumshika maana hatawanunulia u-drink tena. Amekula mabilioni yetu watanzania sasa nasikia ana mpango wa kubwaga manyanga arudi kwao kwa vile kiwanda kimeshindwa kuzalisha.

Hizi pesa ziko guaranteed na serikali hivyo ni sisi walipa kodi ndio tunayemlipia huyu bwana matanuzi yake.

Wakurungezi wa juu nao wanalipwa mishahara ya kutisha wamekaa kimya hawasemi kitu. Kila mtu anachora dili lake. Bosi mkuu anakula na mabosi wadogo nao wanakula kilafi vilevile. Ukipiga kelele unafukuzwa kazi. Wako waliojaribu kusema wakajikuta wako nje ya geti. Ufisadi unaendelea kama kawa.

Watanzania hapa tumeliwa na huyu fisadi wa kihindi. Ametufanyia mbaya sasa anaondoka zake raha mustarehe. Kampuni mama ya Continental Ujerumani yenye asilimi 40% imekifuta kwenye orodha yake ya viwanda kwa kuwa hakizalishi. Hivyo hamna mtu anayemwangalia huyu msela kama kiwanda kinazalisha au la.

Serikali ina asilimia 60% lakini mwenyekiti Shelukindo na wanabodi hawana interest, wao wanapewa matairi ya bure kila wakikohoa. Wakija kwenye vikao wanapigwa milioni zao na matairi wanameza super glue. Hawana la kusema wametulia tuli kama kwenye mtungi wa maji. Sasa hivi General Tyre inadaiwa kila kona. Hawajalipa wafanyakazi kwa miezi sita na ushee. Hawapeleki mafao NSSF ingawa wafanyakazi wanakatwa kila mwisho wa mwezi (kama wakilipwa mishahara). Hivyo kampuni ikifa wafanyakazi wataambulia patupu.

Sasa Nasikia kuna mhindi mmoja ambaye ni tyre dealer hapa Arusha ana mpango wa kununua kiwanda lakini anataka kife kabisa kwanza ili akipate kwa bei chee. Ni rafiki sana na huyu CEO na inawezekana ni dili wamepanga pamoja. Sitashangaa ukisikia akishakinunua kitazinduka na kuanza kufanya kazi kama hakina akili nzuri.

Ni ufisadi tu unaoendelea pale sio kwamba kiwanda hakiwezi kushindana na matairi mengine. UFISADI... period!
 
I hope this will be given the attention it deserves.It looks like in the heat of the Ballali issue this Ufisadi will get ignored.If followed up I can assure you it will shed light on the Big Mfisadi - Mramba.

And, Shelukindo needs to be investigated as well. General Tyre has been his Goose that lays the Golden Eggs. We need to recruit "A firing Squad" to deal with the situation in Tz.
 
Nyumbu...... Duh, kwa kweli inatosha... asante sana kwa mwanga manake duh.....

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!!!!!!!!!!1
 
NDIVYO TULIVYO!..
Hii ndiyo ilikuwa hofu kubwa ya mwalimu, hata chini ya Ubepari tumeshindwa kuendesha miradi ya uzalishaji isipokuwa tumefanikiwa kuunda tabaka la Mafisadi...
 
Heshima mbele wakuu..... Leo tena naona kweli jamaa wameamua kuinyonga kabisaaaa hii kampuni yetu na inaonekana tumeshaamua liwalo na liwe manake hakuna aliyeongea...

Daily News la leo limesema:

Exim Bank sues General Tyre over 600m/- debt

FAUSTINE KAPAMA
Daily News; Monday, May 26, 2008

THE Exim Bank (Tanzania) Limited has filed a suit at the High Court's Commercial Division against the General Tyre East Africa Limited, demanding repayment of 566,852.24 US dollars (about 600m/-) overdraft facility.

Through its advocate, Mr Dilip Kesaria, the bank has also filed an application, seeking either payment of
595,000 US dollars as security or attachment of its property situated on Plot 15 along Nyerere Road before judgement.

Judge Amir Mruma will hear the application on July 15 this year. It is alleged that on January 17, last year, the bank availed a temporary overdraft facility of 500,000 US dollars to the company under certain terms and conditions.

The company allegedly executed an indebtedness agreement (debenture), charging all its undertaking, good will, assets, book debts and property in favour of the bank.
After utilizing the loan, the company has defaulted to pay.

As at March 31, this year, the outstanding balance due was 566,852.24 US dollars. The bank sent several letters between October 24, 2007 and January 18, 2008, demanding repayment of the debt in full, but nothing was done.

The bank had no alternative, but to institute the suit to recover the amount and filed the application for attachment of the
company's properties under title number 18531 after learning that it intended to sell it. According to the affidavit by Mr Dinesh Arora, the General Manager of the bank, the company was planning to sell the property to CMG Investments Limited, who in turn intends to mortgage it to Diamond Trust Bank.

The company was deliberating to sell its property despite being charged to the bank as security for its indebtedness, with intent to obstruct or delay execution of decree that might be passed against them in the suit.

Courtesy:
Daily News, 26/05/2009
 
Hivi Wamarekani si ndio walikuwa "owners" wa General Tyre na makao makuu yalikuwa somewhere in Kentucky?

When did Americans give up the running of the company?
 
Shelukindo ajiuzulu uenyekiti Bodi ya General Tyre

John Mhala, Arusha
Daily News; Friday,May 31, 2008

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kiwanda cha kutengeneza magurudumu cha General Tyre cha mjini Arusha, William Shelukindo amejiuzulu wadhifa huo juzi asubuhi mbele ya mkutano wa wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Taarifa fupi ya kujiuzulu kwa Shelukindo ilitolewa na Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Daven Lohan, katika mkutano uliohudhuriwa na wafanyakazi wa kiwanda hicho kikubwa Afrika Mashariki.

Mmoja wa wafanyakazi hao aliyehudhuria mkutano huo, Nathan Mollel alisema mkurugenzi wa kiwanda hicho pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirima, walitoa taarifa ya kujiuzulu kwa Shelukindo ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga.

Hata hivyo, kujiuzulu kwa Mwenyekiti huyo wa Bodi kunaweza kuleta ‘kiza' zaidi katika kiwanda hicho kwani hadi sasa wafanyakazi 430 wa kiwanda hicho hawajalipwa mishahara ya miezi sita na haijulikani ni lini wafanyakazi hao watalipwa mishahara hiyo.

Shelukindo amekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda hicho kwa zaidi ya miaka 10 na imeelezwa kuwa mwaka 2005 kiwanda hicho kilikopa mkopo wa Dola za Marekani milioni 10 kwa ajili ya kununua mitambo na baadhi ya malighafi.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isidori Shirima hakupatikana kuzungumzia suala hilo, kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kujibiwa. Mollel, ambaye awali alikuwa Kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi (TUICO) katika kiwanda hicho, alidai hali ya kiwanda hicho ni mbaya na ni serikali pekee ndiyo yenye uwezo wa kukikomboa.

Alisema rasilimali nyingi za kiwanda hicho zimeuzwa kiholela bila ya kufuata taratibu, zikiwamo nyumba mbili za kiwanda hicho za mjini Arusha na ghala kubwa la kiwanda hicho lililoko Dar es Salaam na haieleweki fedha hizo zimetumikaje.
 
Mhe. Shelukindo aeleze sababu zilizomfanya ajiuzuru, naamini zitafumbua matatizo yaliyopo japo kiasi kama si yote. Bila kufanya hivyo kujiuzuru kwake hakutakuwa na faida kubwa kwa taifa.
 
General Tyre ilianzishwa baada ya Mwl Nyerere kutembelea Marekani mwishoni mwa miaka 60, alikuta General Tyre Amerika wanabadili technology ya utengenezaji wa matairi, mashine za zamani zilizopitwa na wakati kwa vigezo vya Marekani zililetwa Tanzania na kiwanda cha General Tyre [EA] Ltd kikaanzishwa.

General Tyre ilikuwa na hali nzuri kabla ya ujio wa CEO Deven Lohani mwaka 2000,ninaposema hali nzuri nina maana uwezo wa kununua malighafi,uwezo wa kuwalipa wafanyakazi mishahara,uwezo wa kulipia huduma zote [cash flow] ilikuwa nzuri.

Bwana Devendra Lohani akishikiana na mwenyekiti wa bodi W Shelukindo waliuza malori ya kusafirishia mizigi[matairi] kwa marafiki zake wakihindi kwa bei ya kutupa,aliuza nyumba na maghala kwa bei poa na bila kufuata taratibu za manunuzi.

Kufikia mwaka 2004 General Tyre ilikuwa katika hali mbaya sana kiasi cha kushindwa kulipa mishahara wafanyakazi wake kwa wakati.

Mwaka 2005 Deven alikuwa introduced kwa waziri wetu wa fedha Basil Mramba na Michael Shirima wa Air Precision na kufanikiwa kupata mkopo wa $10,000,000/= [tsh 12.5 bilioni].

Madhumuni makubwa ya mkopo ilikuwa ni kukifanya kiwanda kuwa cha kisasa kwa kununua mashine za kisasa na kiasi kidogo kununua malighafi.

Kwakifupi hakuna mashine wa malighafi iliyonunuliwa badala yake mashine za zamani zilipakwa rangi.
Fedha zililiwa kwa mbwembwe kiasi kwamba wenye akili tulijua muda si mrefu kiwanda kingefungwa,kwa mfano $1,000,000 zilipwa kwa kampuni feki Debt advisory international kama Consultation fees.

Miradi ya pwagu na pwaguzi ilianzishwa kama uyoga nia nikula fedha ya mkopo,Mzee Michael Shirima naye hakuwachwa nyuma katika ufisadi huu,kampuni yake ya precision haule ilikuwa ikilipwa tsh 10 milioni kila mwezi kwa kuegesha lori kiwanda bila kubeba mizigo,na kampuni yake ya water solution nayo ilipewa mradi wa kuchimba visima vinne kwa gharama ya tsh 28 milioni.

General Tyre ilitumia tsh 500 milioni kumkaribisha mfalme wa Nepal na ujumbe wake hapa Tanzania.

Maajabu ni kwamba tangu General Tyre ilipoanza rasmi uzalishaji wa matairi mwaka 1972 mpaka mwaka 2004 kila mwaka ilikuwa ikifanya ukaguzi [Annual Audit] lakini mwaka 2005 ukaguzi ulisimamishwa, tusisahau kwamba mwaka 2005 ndiyo mwaka General Tyre ilipata mkopo wa $ 10,000,000 kutoka NSSF.
 
In my opinion, kifo cha General Tyre was just a matter of time. This company survived that long kwa sababu, mfumo wetu wa zamani, kiwanda kiliweza ku-monopolise market.

Competition iliporuhusiwa ikawa ndio death warrant ya General Tyre, to survive competition ilibidi uzalishaji uwe large scale ili cost per unit iwe ndogo. Sasa economies of scale ikawa impossible sababu you need a bigger market which was not guaranteed, hence tyres za nje zikawa cheaper than our own, with this scenario in motion quite naturally ikawa elimination of the unfit
 
SoA,

I beg to differ Mkuu.... Hivi miaka ya ya mwishoni 90 na mwanzoni 2000 ni matairi gani yalikuwa yanadunda hapa nchini?? Nakumbuka competition kubwa ya GT kwa miaka mingi sasa ilikuwa Firestone (sasa Yana) ya hapo kwa watani wa jadi. Still GT waliendelea ku dominate soko la matairi ya middle class vehicles (4x4, 700 and 750 by 15 and 16 respectivelly). Kwa upande wa malori walikuwa wamesha give up long ago baada ya kuanza kwa safari za mchana (tyre burst sababu ya joto kulinganisha na Michelin, Dunlop etc).

Sasa tukisema kwamba GT walishindwa ku compete na rivals sidhani kama ni sawa.... Ukiangalia NIC, NMB, NBC etc nadhani GT nalo liliingizwa kwenye mpango ambao wengi wameshasema kwenye threads mbalimbali, "Intentional sabotage to lower value" tayari kwa ubinafsishaji!!

Hivi unafahamu kwamba pamoja na kwamba GT hawajazalisha matairi kwa muda sasa, still kuna watu wanayatafuta kwa wale vendors/dealers walioweka kwenye stock na yanaendelea kudunda. Tena believe me hata hawa vendors wanauza jina la GT kusaidia kuuza hata haya Yana tyres, utamsikia vendor anakwambia "Tairi safi sana hizi ni kama General tu mzee"

Naomba kuwakilisha!!
 
Morani75,

Nimekupata. Let's hope we live to see the day, baada ya huo so called 'UBINAFSISHAJI'. General Tyre arise from its ashes, to once again conquer the roads of the motherland
 
General Tyre imeliwa na wakubwa, ma big boss.

Miaka kadhaa ya nyuma walipata mkopo kutoka NSSF wa bilioni 10 ukawa guaranteed na Waziri wa Pesa wakati ule bwana Basil Pesambiri Mramba. Akaitwa Lobbist kutoka Sauzi, akaandika pepa ya kulobbi wakati pesa wameshapata. Akalipwa Bilioni yake (10%) akafutika! Hiyo ilikuwa dili ya kwanza ya kupiga panga hizo pesa.

Mramba akarudishiwa fadhila, akafunguliwa kituo cha watoto yatima kule Rombo kwa ukarimu wa General Tyre. Hiyo ilikuwa ni ule wakati wa uchaguzi wa 2005. Mramba akachekelea, haachi kukisifia kiwanda (ambacho hakizalishi) mpaka leo!

Mheshimiwa Shirima wa Precision ndiyo aliyesaidia mu-introduce CEO wa General Tyre (mhindi kutoka Nepal) kwa Pesambiri. Shirima akapewa tenda ya kuchimba visima vitano vya maji kwa gharama ya Milioni ishirini kila kimoja. Vikachimbwa viwili palepale kiwandani na vingine kwenye houses za wakubwa ambazo hata hivyo zilikuwa hazina matatizo ya maji!

Wakasema hayo mabilioni waliyokopa ni pesa za kununua mali ghafi ili kiwanda kianze kuchapa kazi. Tangu wakati ule Kiwanda hakijawai kuzalisha kwa mfululizo wa zaidi ya miezi miwili. Pesa inaliwa tu. Mkurugenzi kutoka Nepal akaanza kuonyesha vimbweka vyake. Akaleta ndugu na marafiki kutoka Nepal. Wamekodishiwa majumba ya gharama kubwa kwa hisani ya General Tyre. Wakapewa kazi pale kiwandani kama wataalam ambao wanajifunza utaalam. Wakawa kila wikiendi wanaishia Manyara mara Serengeti.

Safari za nje nazo zikaanza. Ananunua tanzanite kwa wamasai kwa bei poa na pesa za mkopo anapeleka Marekani kuziuza kwa bei mbaya. Hakai Arusha kabisa. Kila siku ni Dar ama majuu. Akienda Dar lazima apitie Zanzibar atanue siku kadhaa na machangudoa kwenye hoteli za kitalii ndio afike Dar. Akamfukuza mkewe aka-import malaya kutoka kwao nasikia alikuwa mnenguaji mahili huko Nepal. Huyu mama akawa anafanya shopping yake Nairobi na General Tyre inalipa kila kitu. Alipomchoka akamfukuza. Anachangia mamilioni shughuli zozote zinazoendeshwa na wahindi marafiki zake. Amefadhili sana mbio za magari wakati matairi ya General Tyre hayashiriki. Amefadhili wapanda baiskeli ndugu zake wa kinepali wanaozunguka dunia nzima kwa baiskeli. Akiulizwa kwanini anatoa mamilioni kila siku bila mpango anasema anajenga PR.

Nasikia ni mtu mkubwa sana pale Legions Club Dar es Salaam. Akiingia klabu watu wote wanaacha kununua pombe maana yeye ndiyo 'spender' hiyo siku. Amewanywesha mawazilri na vibosile wote pale Dar es Salaam. Naona wanaogopa kumshika maana hatawanunulia u-drink tena. Amekula mabilioni yetu watanzania sasa nasikia ana mpango wa kubwaga manyanga arudi kwao kwa vile kiwanda kimeshindwa kuzalisha.

Hizi pesa ziko guaranteed na serikali hivyo ni sisi walipa kodi ndio tunayemlipia huyu bwana matanuzi yake.

Wakurungezi wa juu nao wanalipwa mishahara ya kutisha wamekaa kimya hawasemi kitu. Kila mtu anachora dili lake. Bosi mkuu anakula na mabosi wadogo nao wanakula kilafi vilevile. Ukipiga kelele unafukuzwa kazi. Wako waliojaribu kusema wakajikuta wako nje ya geti. Ufisadi unaendelea kama kawa.

Watanzania hapa tumeliwa na huyu fisadi wa kihindi. Ametufanyia mbaya sasa anaondoka zake raha mustarehe. Kampuni mama ya Continental Ujerumani yenye asilimi 40% imekifuta kwenye orodha yake ya viwanda kwa kuwa hakizalishi. Hivyo hamna mtu anayemwangalia huyu msela kama kiwanda kinazalisha au la.

Serikali ina asilimia 60% lakini mwenyekiti Shelukindo na wanabodi hawana interest, wao wanapewa matairi ya bure kila wakikohoa. Wakija kwenye vikao wanapigwa milioni zao na matairi wanameza super glue. Hawana la kusema wametulia tuli kama kwenye mtungi wa maji. Sasa hivi General Tyre inadaiwa kila kona. Hawajalipa wafanyakazi kwa miezi sita na ushee. Hawapeleki mafao NSSF ingawa wafanyakazi wanakatwa kila mwisho wa mwezi (kama wakilipwa mishahara). Hivyo kampuni ikifa wafanyakazi wataambulia patupu.

Sasa Nasikia kuna mhindi mmoja ambaye ni tyre dealer hapa Arusha ana mpango wa kununua kiwanda lakini anataka kife kabisa kwanza ili akipate kwa bei chee. Ni rafiki sana na huyu CEO na inawezekana ni dili wamepanga pamoja. Sitashangaa ukisikia akishakinunua kitazinduka na kuanza kufanya kazi kama hakina akili nzuri.

Ni ufisadi tu unaoendelea pale sio kwamba kiwanda hakiwezi kushindana na matairi mengine. UFISADI... period!

Hivi hawa ma-expatriate wanapokuja hapa nchini hawapewi targets with some milestones kwa muda maalumu au ndio mambo ya ufisadi viongozi wetu serikalini wanakuwa hawaoni?.......Nadhani sasa inabidi wananchi tubadilike na kuwa wakali.
 
Kiwanda cha General Tyre kimeshindwa kuzalisha matairi kwasababu ya ufisadi wa wanasiasa wenye tamaa ya kutaka kumiliki kila kitu kwa gharama yoyote.Nimesoma post za wenzangu ambao wamejitaidi kueleza kwa undani jinsi GTEA ilivyotafunwa na viongozi wetu wasiokuwa na huruma kwa nchi yao.

Binafsi mimi ni mfanyakazi wa General Tyre [EA] Ltd, kwahiyo ninachoandika si kitu cha kusikia au kuambiwa bali ni mambo ambayo nimeyashuhudia yakitendeka. Tulijitahidi kupiga kelele kwa kadri ya uwezo wetu lakini hakuna waliotaka kusikiliza kilio chetu mpaka kiwanda kilipofungwa au kusimamisha uzalishaji kabisa.

Kwanza nakubaliana kwa 100% na ndugu Kabonde kwamba mashine za General Tyre ni za zamani sana,kiasi kwamba hata ajira kwa wafanyakazi wa kiwandani walitakiwa kuwa na kilo zisizopungua 70 kgs,kigezo cha elimu kilikuwa akizingatiwi sana kama uzito.

General Tyre ilianza kuyumba mara mfumo wa uendeshaji ulipobadilishwa,mfumo wa zamani ulikuwa hivi, General Manager [Chief executive officer], Sales & Marketing Manager, Chief Financial Officer, Factory Manager wote walikuwa wanatoka Marekani, Human Resouce Manager alikuwa mtanzania na wote walikuwa wanaingia kwenye mikutano ya Bodi. Mfumo mpya uliwaengua managers wote kutoka Marekani isipokuwa General Manager [Chief executive officer] pekee. Tatizo kubwa ni kwamba manages wa kitanzania walikuwa si wajumbe wa bodi na mamlaka ya nidhamu ilihamishiwa chini ya General Manager. Sijui kama wa JF mmenielewa au mmeshagundua sanaa iliyofanyika.

Mfumo mpya ulimpa madaraka makubwa kupita kiasi General Manager afanye kila analotaka kufanya bila kuhojiwa na Managers wa kitanzania, mfumo huu pengine ungeweza kufanyakazi kama bodi ya wakurugenzi ingeamua kufanyakazi yake ipasavyo lakini bodi nayo ikaungana na General Manager kuiba mali ya umma.

Naomba kutafautiana na ndugu Kabonde pale anaposema General Tyre iliacha kufanya ukaguzi wa kila mwaka [annual audit] kuanzia mwaka 2005. Mwaka 2005 ukaguzi ulifanyika na kampuni ya Ernst & Young kama kawaida lakini ripoti haikutolewa. Kuna sababu kuu mbili zilizopelekea ripoti ya wakaguzi Ernst & Young kufichwa nazo ni:

1) Mwaka 2005 wakaguzi nje {external auditors} walitakiwa na NBAA kukagua kwa kufuata viwango vya kimataifa. Kabla ya maagizo ya NBAA wakaguzi walikagua Balance Sheet peke yake. Ukaguzi wa mwaka 2005 uliofanywa na vijana wa Ernest & Young ulikuwa wa kutisha kwa mafisadi

{A} walikagua Trading, Profit & Loss a/c {B} Account zote zilizokuwa na figures kuanzia 1milioni.

Kwa wataalamu wa fani ya uhasibu watanielewa haraka kwamba Trading,Profit & Loss a/c matumizi {expenses} zinaonekana bila shida, Devendra alidhani kuna baadhi ya wafanyakazi wa department ya Account walimchongea kwa wakaguzi kumbe utaratibu ulikuwa umebadilika.

2) General Manager Devendra Lohani Mhindi wa Nepal mwenye uraia wa Marekani hakuwahi kukaguliwa kwa kiwango hiki.

Bahati mbaya kwake mwaka 2005 alikuwa ame-lobby akapata mkopo wa tsh 12.3bilioni kutoka NSSF kwa njia za ajabu ajabu. Ernst & Young walipomaliza ukaguzi walitoa Draft kwa General Manager kama taratibu za ukaguzi zinavyotaka ili management iweze kuipitia na kuangalia kama kuna hoja ambazo zimekosewa zisahihishwe kabla ya kupelekwa kwenye bodi ya wakurugenzi.

Hoja za wakaguzi zilikuwa nzito kwa fisadi Devendra,hasa matumizi yake binafsi ambayo Ernst & Young walisema wazi ni makubwa kupindukia, $ 1 million Consultation fee ya Debt Advisory International nazo zilimkaba koo Devendra, gharama za kumkrimu mfalme Gyanendra Shah wa Nepal na ujumbe wake nazo zilikosa majibu kutoka kwa Devendra Lohani.

Kila kitu kinawezekana Tanzania bwana Devendra hakurudisha ripoti kwa wakaguzi na bodi ya wakurugenzi chini ya mwenyekiti W Shelukindo nayo haikuhangaika kuiulizia na huo ndiyo ukawa ni mwanzo na mwisho wa kufanyika kwa ukaguzi General Tyre. Mara nyingi najiuliza bodi ya wakurugenzi ya General Tyre ilikaa bila kuona financial report kwa miaka mitano sijui walikuwa wanajadili nini zaidi ya kugawana posho za vikao na kumwacha bwana Devendra akitutambia kwamba yeye yuko mbele ya serekali yetu tukufu kwa miaka kumi zaidi!

Inabidi nipumzike kidogo mambo ya GTEA ni mengi mno ni bahati mbaya ufisadi wa Devendra haukupewa umihimu unaostahi labda kwasababu General Tyre iko mikoani pengine ingekuwa Dar tungeisikia kama tulivyoisikia EPA, Radar nk
 
Mkuu ngongo, karibu jamvini.... Hii maneno umeleta jamvini Mkuu inaweka chumvi zaidi na kupelekea watu kama sisi wenye uchungu wa kuona "such a giant factory" ikiangamia kwa kudhullumiwa!!! Nina uhakika kama kwenye maneo mengine ambapo sauti ya watu (ikiwemo JF) imesikika na kuleta mabadiliko, huku napo tutafanikiwa....

Alisema Mkuu FM, Amandla!!
 
Morani 75,nashukuru kwa kunitia moyo lakini wenzio tuna kwenda mwezi wa tano bila salary,kama ni suala la uchungu nadhani wafanyakazi wote wa GTEA LTD wakwetu umezidi.Bado nitaendelea kuwapa habari za ndani kuhusu GTEA LTD ambazo hamjawahi kuzisikia mahali popote.
 
Heshima mbele wakuu..... Leo tena naona kweli jamaa wameamua kuinyonga kabisaaaa hii kampuni yetu na inaonekana tumeshaamua liwalo na liwe manake hakuna aliyeongea...

Daily News la leo limesema:

Exim Bank sues General Tyre over 600m/- debt

FAUSTINE KAPAMA
Daily News; Monday, May 26, 2008

THE Exim Bank (Tanzania) Limited has filed a suit at the High Court’s Commercial Division against the General Tyre East Africa Limited, demanding repayment of 566,852.24 US dollars (about 600m/-) overdraft facility.

Through its advocate, Mr Dilip Kesaria, the bank has also filed an application, seeking either payment of
595,000 US dollars as security or attachment of its property situated on Plot 15 along Nyerere Road before judgement.

Judge Amir Mruma will hear the application on July 15 this year. It is alleged that on January 17, last year, the bank availed a temporary overdraft facility of 500,000 US dollars to the company under certain terms and conditions.

The company allegedly executed an indebtedness agreement (debenture), charging all its undertaking, good will, assets, book debts and property in favour of the bank.
After utilizing the loan, the company has defaulted to pay.

As at March 31, this year, the outstanding balance due was 566,852.24 US dollars. The bank sent several letters between October 24, 2007 and January 18, 2008, demanding repayment of the debt in full, but nothing was done.

The bank had no alternative, but to institute the suit to recover the amount and filed the application for attachment of the
company’s properties under title number 18531 after learning that it intended to sell it. According to the affidavit by Mr Dinesh Arora, the General Manager of the bank, the company was planning to sell the property to CMG Investments Limited, who in turn intends to mortgage it to Diamond Trust Bank.

The company was deliberating to sell its property despite being charged to the bank as security for its indebtedness, with intent to obstruct or delay execution of decree that might be passed against them in the suit.

Courtesy:
Daily News, 26/05/2009

Hii nilikuwa sijaiona vizuri.

Ni kweli General Tyre imeshitakiwa kwa makosa ya Devenrda Lohani kufanya utapeli.mwisho mwa mwaka 2005 baada ya mafisadi kumaliza kutafuna fedha za NSSF walikimbilia EXIM bank kuomba Overdraft facility, Godown Plot 15 along Nyerere Road liliwekwa rehani kama security.

Deveni Lohani na Rose Soloka {financial Manager} walitengeneza lease nyingine na kuamua kuliuza kwa C M Gachuma kada maharufu wa CCM mkoani Mwanza kwa tsh 1.8 bilioni lakini kiasi kilichoingia katika a/c za General Tyre kilikuwa ni tsh 800 milioni tu zingine mpaka leo hatuji zilipelekwa wapi.

Rose Soloka kakimbilia TIB zikopelekwa fedha za EPA, labda atapeleka ujuzi wake wa kifisadi alioupata General Tyre?
 
Back
Top Bottom