General Tire- kabla ya kuweka ma bilions ya walipa kodi reserch ifanyike

SON OF THE LAND

JF-Expert Member
Oct 7, 2015
204
210
Tanzania yetu imezoeleka kwa ukurupukaji wa mambo mengi halafu hayafiki mwisho au hayawi ya mafanikio mamo mengi hatuyaangalii kwa kirefu na mapana hatuna RD centers (research and development) katika kila sector ili kila tulifanyalo tuwe tumefanya research za kutosha

sasa turudi kwenye topic yetu ka nini nimeandika hili ni kuhusu General Tire, tumesikia mh rais anatarajia kuwekeza mapesa mengi tu which is good kwa uchumi na ajira ila only itakua good kama hivyo vitu viwili vita work otherwise kiwanda kitakua hakina tija kitakua kama shirika la ndege baadala ya kuwa sehemu ya kuongeza mapato kwa nchi imekua kituo cha kupokea misaada as if ni HIV centre, badala ya kupunguza presure ya budget imekua ikiongeza buden sababu nayo inakinga mikono kila siku kuomba ipewe hela ili ijiendeshe na ukijiuliza kuna umuhimu wowote kwa shirika hili kuwepo itasikia story nyingi et ni nembo ya taifa inatambulisha taifa camon jamani tunavyo vitambulisho vya kutosha na tumesindwa kuvitumia kujitambulisha, Kilimajaro mountain, serengeti mbuga still hatujaweza kujilikani

sasa kwa General Tire ulimwengu wa biashara unabadilika sana na kuna mambo mengi ya ku consider ili kiwanda kifanye kazi kwa manufaa, tusishikirie yale ya zaman eti kilikua kina lisha east Africa nzima, ya thats true ila mambo yanabadilika sana, ndugu zetu kenya walitufanyia figisu nyingi kwenye kufanya na kuchangia hiwanda kufa lakini sasa kile cha kwao nacho CHALI kimeshindwa kujiendesha kutokana na ushindani na wanakifunga hivi karibuni, sasa ni elimu ipi tumejifunza hapo ndio maana nikaomba RD ziwepo kuna lakujifunza hapo then kuna huyu adui numba moja ni huyu mchina lazima tumuangalie ni jinsi gani tuaweza kushindana nae kwa ubora na bei kuwa rahisi na nafikiri hio ndio big challenge kwetu maana biashara huria itakiua hicho kiwanda in just two years

sasa GT inabidi kabla ya kuanza kazi wafanye thourough research niliyo yataja hapo juu ni kianzio tu inabidi waingie ndani kwa mambo mengine mengi tu ili waweze kufanikiwa
i wish GT the best ila wawe makini tu kisianzishwe kisiasa au kimihemko


OUR HEAVENLY FATHER BLESS TANZANIA. AMEN
 
Back
Top Bottom