General knowledge, najua hukufundishwa darasani

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
Changamsha kichwa kwa kuongeza knowledge mpya na kuongeza uelewa wa mambo ambayo mengi hayafundishwi darasani!

MESOPOTAMIA

Ni eneo lenye historia kubwa kuhusu binadamu wa kale. Lipo kati ya mito miwili mikubwa Mashariki ya Kati, Tigris na Euphrates. Inatajwa kwamba Bustani ya Eden ilikuwa kwenye eneo hili ambalo kwa sasa ndipo zilipo nchi za Iraq, Kuwait na sehemu ndogo za Iran, Syria na Uturuki.

VENUS FLYTRAP

Huu ni mmea wa ‘ajabu’ ambao unakula wadudu. Mmea huu jinsi ulivyo, una maumbile ya kuwavutia wadudu mbalimbali kutokana na harufu yake nzuri na nta inayotoa. Wadudu wanapotua juu ya majani yake, hujikunja haraka na kuwaviringisha ndani yake na kuanza ‘kuwala’ kwa kutumia kemikali zake ambazo huwayeyusha wadudu kisha majani kufyonza virutubisho vyake.

IKULU YA VERSAILLES

Bila shaka umewahi kusikia kuhusu ikulu kubwa, bora na zinazolindwa zaidi duniani kama The White House ya Marekani, The Buckingham Palace ya Uingereza na kadhalika. Sasa chukua hii, The Palace of Versailles ndiyo ikulu kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia na ilijengwa mwaka 1682 na Mfalme Louis XIV wa Ufaransa.

Watalii zaidi ya milioni saba na laki saba hutembea kujionea maajabu ya teknolojia zilizotumika miaka ya zamani kwa kujenga ikulu hiyo.

MSAKO WA WACHAWI WA SALEM

Matukio ya msako wa wachawi, yalianza kuripotiwa mwaka 1692 katika eneo la Salem, Massachusetts nchini Marekani. Katika tukio hili linalotajwa kuwa msako mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwa wachawi, watu zaidi ya 200 walikamatwa kwa tuhuma za uchawi, 19 wakakutwa na hatia kisha kunyongwa, wengi wao wakiwa ni wanawake.

MGUNDUZI WA DICTIONARY

Bila shaka unazijua dictionary. Basi kwa taarifa yako, Noah Webster ndiye anayetajwa kama baba wa dictionary duniani. Ndiye aliyeandika dictionary ya kwanza duniani, The Merriam-Webster Dictionary mwaka 1828 na hata baada ya kifo chake, dictionary yake imeendelea kufanyiwa marekebisho na ndiyo inayoaminika zaidi duniani katika lugha ya Kiingereza.

VALENTINA TERISHKOVA

Huyu ndiyo mwanasayansi mwanamke wa kwanza kupaa kwenda anga za juu kabisa. Hiyo ilikuwa ni Juni 16, 1963 na aliruka na chombo kiitwacho Vostok 6 akiwa na wanasayansi wenzake wa Urusi na kuweka rekodi ya aina yake.

VOX POPULI

Haya ni maneno ya Kilatini ambayo maana yake ni ‘Sauti za Watu’. Hutumika sana kwa wanaharakati wanaopigania uhuru na demokrasia.

AMPERSAND

Bila shaka huwa unaitumia sana alama hii ‘&’ unapoandika, lakini je unajua jina lake inaitwaje? Basi kwa taarifa yako, inaitwa Ampersand na hutumika kuunganisha maneno, ikiwa na maana ya ‘na’ kwa Kiswahili na ‘and’ kwa Kiingereza.

RENNAISSANCE

Hiki ni kipindi katika historia ya mwanadamu ambacho kinatajwa kwamba ndipo binadamu wa sasa alipozaliwa upya na kupata ufahamu kamili kuhusu yeye na mazingira yanayomzunguka. Ilitokea karne ya 16 na ilianzia barani Ulaya.

MACHOZI MWEZINI

Utafiti unaonesha kwamba ukiwa mwezini au kwenye anga za mbali, huwezi kutokwa na machozi hata kama una huzuni kali kiasi gani. Hii ni kwa sababu nguvu ya uvutano iliyopo huko, hairuhusu machozi kutoka wala kutiririka.

JOTO LA KIFO

Mwezi Juni, mwaka 2019, Bara la Ulaya liliweka rekodi ya aina yake baada ya joto kuongezeka kuliko kawaida. Nchini Ufaransa, kiwango cha juu kabisa kilichorekodiwa kilikuwa ni 46.1 sentigredi.

Jumla ya watu 868 nchini Ufaransa walipoteza maisha kutokana na joto hilo, huku mtu mmoja akiripotiwa kupoteza maisha nchini Ubelgiji. Mbali na vifo vya watu, wanyama wa porini na mifugo mingi pia iliathirika.

UXORIOUS

Uxoriuos ni neno la Kiingereza ambalo linamaanisha mwanaume ambaye anampenda sana mkewe kiasi cha kugeuka ‘bwege’. Yupo tayari kufanya chochote ili kumfurahisha mkewe, hata kama moyoni atakuwa anaumia kwa kiasi gani. Mtu wa aina hii anakuwa na wivu sana na hisia za juu kwa mkewe, lakini hana uwezo wa kumdhibiti kwa chochote.

UKRAINE

Ukraine ndiyo nchi ya pili kwa ukubwa wa eneo barani Ulaya. Nchi ya kwanza ni Urusi (Russia) yenye eneo la kilometa za mraba 3,972,400 huku Ukraine ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 605,628. Mbali na ukubwa wa eneo, Ukraine pia ni nchi ya pili kuwa na jeshi kubwa zaidi barani Ulaya baada ya Urusi.

AKIDI IMETIMIA

Pengine umewahi kusikia sana msemo huu, ‘akidi imetimia’ lakini pengine huelewi maana yake ni nini. Basi kwa taarifa yako, neno akidi kwa Kiingereza linaitwa Quorum na linamaanisha idadi ya watu wanaotakiwa ili mkutano uweze kufanyika na kuwa halali kisheria.

KITABU CHA OBADIA

Katika Biblia Takatifu, Agano la Kale, kuna kitabu kinachoitwa Obadia ambacho ndiyo pekee chenye sura moja tu, ikiwa ni mistari ishirini na moja. Katika agano jipya, kuna vitabu vingine vinne, ambavyo kila kimoja kina sura mojamoja na kuvifanya kuwa vitabu vidogo zaidi katika Biblia. Vitabu hivyo ni Philemon, Yohana 2, Yohana 3 na Kitabu cha Yuda.

MAYAI VIZA

Hewa ya Hydrogen Sulphide, inayotengenezwa maabara na wakati mwingine kutokea katika katika hali asilia, inatoa harufu kama mayai viza. Inaelezwa kwamba ni vigumu sana kutofautisha harufu ya Hydrogen Sulphide na yai viza au yai lililooza. Unapovuta Hydrogen Suphide kwa muda mrefu, unaweza kudondoka na kupoteza fahamu.

X-RAY

Bila shaka umewahi kusikia kuhusu picha za X-Ray, zile anazopigwa mtu ili kutazama mpangilio wa mifupa yake ya ndani, hasa pale anapopata ajali au anapokuwa na maradhi. Basi kwa taarifa yako, Mjerumani Wilhelm Conrad Röntgen ndiye aliyegundua picha hizi Machi 27, 1845. Mwaka 1901 alishinda tuzo ya Nobel kwa ugunduzi huo.

CALAMA

Katika Jangwa la Atacama nchini Chile, kuna kijiji kinachoitwa Calama. Basi kwa taarifa yako, mvua haijawahi kunyesha kwenye kijiji hiki tangu maelfu ya miaka iliyopita! Wenyeji hawaijui kabisa mvua kwa sababu hawajawahi kuiona maishani mwao.

MWANAUME VS MWANAMKE

Wanaume wanao uwezo wa kusoma maandishi madogo zaidi kuliko wanawake wakati wanawake wanao uwezo wa kusikia sauti za chini zaidi kuliko wanaume. Kwa wastani, mwanamke anachezesha kope zake mara mbili zaidi ya mwanaume kwa kila dakika moja.

Hashpower7113!
 
Na ni chama cha chadema pekee duniani kilichowahi kuteua mgombea urais ambaye yupo kwenye list of shame ya chadema yenyewe.

Rekodi hii iliwekwa mwaka 2015 nchini Tanzania.
 
Back
Top Bottom