Gender, Women empowerment and National development

GAGL

JF-Expert Member
Aug 5, 2010
296
202
Habari wana JF. Nakuja tena na maada nyingine ambayo yaweza onekana ni ya kawaida sana lakini kwa great thinker hili suala lina impact kubwa sana katika maendeleo ya taifa letu. Africa tumekuwa watu wa kupokea kila kitu kutoka mataifa yaliyoendelea. Leo naomba tujadili hili suala ambalo wamelileta wakati wao hawalifanyii kazi kama walivyolileta kwetu. Kwana naomba kuuliza, hivi Dr. Migiro, Helen Johnson, Hilary Clinton, Angel Meckel, Dr. Rice, Victoria na wengine walishika nyadhfa hizo kwa kuwa ni wanawake? Mama Masalakulangwa kama mnamfahamu, ni journalist mkubwa aliongelea suala la mikopo kipindi flani akasema: 'Hainingii akilini ninapoona kuwa msichana mwenye division two anapewa mkopo wakati mvulana ananyiwa kwa kuwa ni mvulana' hapa alimaanisha vigezo vya utoaji mikopo visiangalie ujinsia ili kuondoa unyonge wa mwanamke. Inabidi nae akidhi vigezo sawa na mwanaume ili asiwe mtu wa kuhurumiwa kila siku. Wana JF, sipingi harakati za kumkomboa mwanamke, ila swali hapa ni kwamba tunamkomboa mwanamke kutoka kwenye nini? Je kuwajaza wanawake bungeni hata kama hawana sifa za kuwa viongozi ni kuwakomboa? Ni kweli ukimuelimisha mwanamke umeelisha jamii yote? Kuwa na wanawake wengi madarakani ni kweli kunalinyanyua taifa kiuchumi? Kuwa na majaji wengi wanawake ni kuboresha idara ya mahakama? Ni kweli mwanamke hawezi kupigania nafasi za juu sambamba na wanaume mpaka abwebwe? Je tuliielewa kweli dhana ya kumkomboa mwanamke au tuliipokea tu? Jiulize, tulikuwa na mamalkia wengi tu wa kike kabla ya ukoloni, mfn Zingankuwu, malkia wa Kush (Ethiopia), pia walikuwepo kule Sudanic states karne ya 16, soma historia ya Haile Selasei, utaona kulikuwa wanawake wenye nguvu kisiasa. Hawa walibebwa na nani? Mimi nadhani hili ni suala la kifamilia, kiukoo na kikabila zaidi, na sio kitaifa. Taifa lazima liendelee. Nawasilisha.
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,231
CAGL

Fanya kuhariri hii kazi yako uweke pragraph ili tuweze kusoma uzuri kabla ya kuchangia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom