Gen. Mrisho Sarakikya aliwahi kuhusishwa na Uhaini?

Gustanza_The

Senior Member
Aug 6, 2008
126
7
Wakuu, nani anafahamu [kiundani] kuhusu uhaini wa aliyewahi kuwa the first Chief of Defence Forces, General Mrisho Sam Hagai Sarakikya...? Niliwahi kusimuliwa zamani kuwa huyu jamaa alipanga kuipindua nchi/ua Nyerere enzi hizo[Lugalo], na kwamba mtu pekee aliyeokoa hayo mapinduzi alikuwa ni General David Musuguri. Je, ni kweli?

P.S. Kuna paper ninayoaandika kuhusu hali aya kisiasa nchini Tanzania tangu tulipopata uhuru mwaka 61 mpaka leo hii, hivyo I want to get the facts straight kabla sija-submit hiyo paper. So help me by posting down anything you know about uhaini wa huyu jamaa. Just anything.
Peace!
 
..i was suprised kwamba Sam Hagai Mirisho Sarakikya alikuwa haja-retire jeshini mpaka majuzi wakati Mkapa anang'atuka.

..tena Mkapa akampandisha cheo na kuwa 4 Star General, akamtunukia nishani ya utumishi uliotukuka, na official kustaafu toka JWTZ.
 
Be careful na hiyo paper yako some of the JF sources are so questionable.. ni ushauri tu...

I know Masatu, ila nachotafuta hapa ni opposing views. Ninazo info tayari, ila source yake ina-lean upande mmoja tu...[and I'm sure kuna watu wengi humu walio na nyeti za kumwaga kuhusu suala hili...] so, kukutoa wasiwasi mkuu, nitazifanyia vetting kali hizo info zote nitakazozipata kabla ya kuziingiza ndani ya paper.
 
Sarakikya hajawahi kuhusishwa na kesi ya uhani.Kwa kifupi wanajeshi wa vyeo vya chini walitishia kupindua nchi punde tu baada ya uhuru wakikwera na uongozi wa Brigedia mwingereza na mshahara mdogo.Kuchaguliwa kwa Brigedia mwingereza kulitokana na ukweli kuwa kulikuwa hakuna mtanzania aliyefikia cheo cha kuweza kuwa CDF maana mkoloni ali-limit vyeo kwa watu weusi.

Wakati huo Sarakikya alikuwa kapteni na hakuhusika ndio maana alikamatwa na kutiwa ndani na wanajeshi wenzake waongoza mgomo maana alichukuliwa kama mmoja wa wasaliti kwa kuwa umande hakukimbia kawa wengi wao wakati huo.

Nyerere alidharau mgomo huo mpaka aliposhauriwa na kawawa kuwa hali si nzuri na ikabidi afichwe kwa muda.Mpaka leo sehemu alipojificha inabakia kuwa siri iliyofichwa vizuri katika historia ya nchi hii?Oscar Kambona ndie aliyekuwa mediator kati ya serikali na wanajeshi hao wenye hasira na alifanikiwa kuwatuliza baada ya purukushani za hapa na pale ambazo sitaweza kuziweka hapa kwa sababu ya muda.

Inasemekana Kambona alikuwa na lengo moja na wanajeshi waasi ila alibadili mawazo baada ya kuona wanajeshi hao wana akili ya kibangi bangi na hasira zilizopitiliza.Baada ya fujo kutulia Nyerere aliibuka kutoka mafichoni akifikiria mambo shwari.

Mwalimu akatumia ujanja wa kutoa amri kuwa atafika lugalo kukagua gwaride kwa hiyo kila askari awe tayari.Wanajeshi waasi walikataa kama mwanafunzi mtukutu anapokataa kutii amri ya mwalimu ya kufanya usafi.

Inasemekana kila askari aliendelea na shughuli zake kama amri hiyo haijatoka kwa amiri mkuu.Jaribio lingine la mwalimu lilishindwa na ndipo alipogundua kuwa jeshi limekosa utii kwakwe na kugundua mpango wa kumpindua huko pale pale.Aliomba msaada wa Majeshi ya Uingereza na Malikia akatuma makomando wachache na helikopta.

Ndani ya masaa machache sana wanajeshi wa Tanzania walisalimu amri pasipo umwagaji wa damu baada ya ACTION ndogo tu kutoka kwa vijana wa malikia.Ndipo nyerere alipomrudisha nyumbani Brigedia mwingerez,kuunda jeshi jipya la JWTZ, kuongeza mshahara na KUMRUSHA CHEO SARAKIKYA KUTOKA KAPTENI MPAKA BRIGEDIA NA KUMTEUA KUWA CDF wa kwanza wa jwtz mzawa wa Tanganyika.

Sarakikya alistaafu kishujaa kama Meja Jenerali na kutokana na mchango wake mkubwa Mkapa alimpandisha kwa hesima mpaka Jenerali kamili cheo hata baada ya kuwa alishastaafu.Mtiririko wa yeye kupanda vyeo haujawahi tokea Tanzania na sidhani kama itajirudia.
 
Sarakikya hajawahi kuhusishwa na kesi ya uhani. Kwa kifupi wanajeshi wa vyeo vya chini walitishia kupindua nchi punde tu baada ya uhuru wakikwera na uongozi wa Brigedia mwingereza na mshahara mdogo...

Asante mzee mwafrika kwa ufafunuzi wako wa kina; ila nina swali hapo: Hivi, ni nini kilichosababisha Mwalimu akamtupa Sarakikya kuwa balozi wa tanzania [kama sijakosea, Nigeria]; na kumpachika Musuguri kuwa mkuu wa majeshi?
 
Gustanza-The,

..kuna school of thought tofauti.

..kuna wanaodai Mirisho Sarakikya kweli alipanga kumuondoa Mwalimu.

..kuna wengine wanadai yalikuwa majungu tu.

..suppose alitaka kumpindua, je walitofautiana nini na Mwalimu?

..pia ilikuwaje Mkapa akampandisha cheo na kumpatia mafao yote? ninavyoelewa mimi Sarakikya hana shida mpaka atunzwe na jeshi.

NB:

..Sarakikya alipoondolewa jeshini aliteuliwa kuwa waziri wa michezo na utamaduni. baadaye ndiyo alipelekwa ubalozini.

..pia Maj.Gen.Abdalah Twalipo ndiye aliyechukua nafasi ya Sarakikya.

..Musuguri aliteuliwa CDF baada ya vita vya kagera kuchukua nafasi ya Twalipo.
 
Sarakikya alistaafu kishujaa kama Meja Jenerali na kutokana na mchango wake mkubwa Mkapa alimpandisha kwa hesima mpaka Jenerali kamili cheo hata baada ya kuwa alishastaafu.Mtiririko wa yeye kupanda vyeo haujawahi tokea Tanzania na sidhani kama itajirudia.

Hapa naomba nikusahihishe kidogo. Baada ya Sarakikya kutumikia nchi kama balozi nchini Kenya kwa muda mrefu sana akiwa na cheo cha Major-General na akiwa bado ni askari, kwa mujibu wa taratibu cha kijeshi alitakiwa awe amepandishwa cheo kwenda General. Hivyo, baada ya kuona kwamba hakupandishwa cheo, kabla ya kustaafu rasmi aliomba kupandishwa cheo kama stahili yake halali na CDF aliyekuwepo wakati huo kutoa ushauri unaofaa kwa rais, na ndo maana alipandishwa cheo kuwa Generali na akastaafu akiwa Generali. Kwa hiyo Sarakikya alistaafu na akiwa na cheo cha Generali na siyo Major-General.


So far, kuna Conspiracy theory inayomhusisha Sarakikya na njama za kumpindua Nyerere zilizofichuliwa na Marehemu Abdallah Twalipo wakati huo akiwa Kanali ambaye alimjulisha kawawa kwa siri na kawawa kumjulisha Mwalimu. Hiki ndo chanzo cha Sarakikya kupelekwa nje kuwa Balozi kwa kipindi chote cha utumishi wake kilichosaria, na pia Chanzo cha marehemu Abdallah Twalipo kuwa CDF.

Tuendelee na conspiracy theories zingine kama zipo...............
 
ngereja,

..lakini wakati Sarakikya anatumia jeshi hakukuwa na utaratibu wa CDF kuwa na cheo cha 4 star General.

..Twalipo hakupandishwa cheo kuwa Lt.Gen baada ya vita vya Kagera?

..pia Musuguri ali-serve kwa muda mrefu kama Lt.Gen na Mkuu wa Majeshi.

..Twalipo na Musuguri walipandishwa vyeo kuwa Generals siku moja Mwalimu alipokuwa akitoa nishani kwa wananchi mbalimbali waliotumikia taifa kwa muda mrefu.

..hata hivyo Twalipo alikuwa senior kwasababu he wore his insignia first.

..sasa kwanini Sarakikya alistahili hicho cheo cha 4-Star General??!!

NB:

..conspiracy theory nyingine: Ernest Mwita Kiaro ndiye askari aliyepita vyeo vyote mpaka kuwa Major General.

..kutoka kuwa Maj.General alipaishwa kuwa 4 Star General na kuukwaa U-CDF!!
 
So far, kuna Conspiracy theory inayomhusisha Sarakikya na njama za kumpindua Nyerere zilizofichuliwa na Marehemu Abdallah Twalipo wakati huo akiwa Kanali ambaye alimjulisha kawawa kwa siri na kawawa kumjulisha Mwalimu. Hiki ndo chanzo cha Sarakikya kupelekwa nje kuwa Balozi kwa kipindi chote cha utumishi wake kilichosaria, na pia Chanzo cha marehemu Abdallah Twalipo kuwa CDF.

Tuendelee na conspiracy theories zingine kama zipo...............

Thanks ngereja kwa post yako. So far maelezo uliyoyatoa yanarandana na maelezo niliyopewa na mtu aliyewahi kufanya kazi serikalini [karibu na mchonga], ila utofauti ni kwamba, Musuguri ndiye aliyemshitua Mwalimu na sio Twalipo. So, sijui sahihi ni lipi? Hivyo naomba kwa anayefahamu zaidi kuhusu hii issue atufafanulie...
 
Serpent General,

Kama kuna makosa ya kupandishana vyeo kutokana na ngazi za vyeo, tunayaona tena hapa kwenye suala la Jeshi na hasa kuhusiana na Sarakikya.

Si kuwa hatukuwa na utaratibu wa vyeo vya jeshi ambavyo vilifikia 4 star au 5 star general Tanzania, bali ni uvivu wa ama wizara ya utumishi na upandaji vyeo au ni kukosekana kwa utasih kutoka viongozi kupandisha watu vyeo (government scales) ili kunyima watu mishahara au kuwapa wanachostahili.

Je, Nyerere alikataza watu wasipandishwe vyeo makazini au ni waliokuwa na majukumu walishindwa kufanya kazi zao kwa visingizio visivyo na maana kama tutaoa wapi pesa za kuwalipa, siasa ya ujamaa na azimio au kuona kuwa kupandisha mtu cheo ni kumpa nguvu nyingi na madaraka makubwa zaidi?
 
Rev.Kishoka,

..nadhani mwanzo jeshi letu lilikuwa dogo hivyo hakukuwa na ulazima wa CDF kuwa 4 Star general.

..40 yrs ago JWTZ ilipoanzishwa CDF alikuwa ni Brigadier na Chief of Staff wake ni Major.

..baada ya vita vya Kagera jeshi limekuwa na idadi ya Major Generals [2 star] imeongezeka. hiyo inaweza kuwa sababu ya kulazimisha CDF awe General na Chief of Staff awe Lt.Gen.

..nadhani Sarakikya case yake ni unique. kumbe hakustaafu jeshi alipoteuliwa waziri na baadaye balozi.

..hata Mayunga naye i think i heard somewhere that he was promoted to Lt.Gen. tayari akiwa ni balozi. i dont know if it is true.

NB:

..nadhani tatizo ni MIZENGWE na MAJUNGU yanatumika kuwaondoa wahusika huko Jeshini.
 
jokaKuu,
Hii ya Sarakikya kuondolewa jeshini haikuwa na mizengwe. Julius alimwita pale Msasani akampasha juu ya njama zake za kupindua serikali, Sarakikya akabaki mdomo wazi. Lakini ukiangalia taratibu, utaona Mkapa somehow aliwatafuta wote wale waliogombana na Nyerere, kukiwemo Bibi Titi, Mzee Fundikira, na kujaribu kuwasogeza karibu naye. Nimejiuliza juu ya hili na hitimisho langu bado siwezi kuliweka hapa.
 
jokaKuu,
Hii ya Sarakikya kuondolewa jeshini haikuwa na mizengwe. Julius alimwita pale Msasani akampasha juu ya njama zake za kupindua serikali, Sarakikya akabaki mdomo wazi. Lakini ukiangalia taratibu, utaona Mkapa somehow aliwatafuta wote wale waliogombana na Nyerere, kukiwemo Bibi Titi, Mzee Fundikira, na kujaribu kuwasogeza karibu naye. Nimejiuliza juu ya hili na hitimisho langu bado siwezi kuliweka hapa.

Just using polite words is that wanafunzi wa Mwalimu ni Wanafiki!
 
mkapa inaonyesha kama alitaka kuonyesha yeye ana nguvu kuliko "mwalimu".

labda alitaka yeye legacy yake ibakie kuliko ya mwalimu, na kuamua kufanya yale yote yaliyokuwa yakinung'unikiwa kuhusu mwalimu.......kama kuwakumbatia watu waliogomana nae .

asanteni kwa shule nzito.
 
Jasusi said:
Hii ya Sarakikya kuondolewa jeshini haikuwa na mizengwe. Julius alimwita pale Msasani akampasha juu ya njama zake za kupindua serikali, Sarakikya akabaki mdomo wazi. Lakini ukiangalia taratibu, utaona Mkapa somehow aliwatafuta wote wale waliogombana na Nyerere, kukiwemo Bibi Titi, Mzee Fundikira, na kujaribu kuwasogeza karibu naye. Nimejiuliza juu ya hili na hitimisho langu bado siwezi kuliweka hapa.


Jasusi,

..sijui kwanini Mwalimu hakumchukulia hatua za kisheria "mhaini" Sarakikya pamoja na "wahaini" wenzake.

..matokeo yake ni "mhaini" anakuja kuwa 4-star general, na taifa linaingia gharama ya kumhudumia "mhaini" mpaka kifo chake.

..kama hiyo siyo MIZENGWE basi tutafute definition nyingine ya neno hilo.

..halafu ni Mwalimu ndiye aliyemsamehe Bibi Titi na kumtoa kifungoni. tena hata kuna mkutano wa hadhara ambao walikuja ku-appear pamoja.

..Mzee Mwinyi naye alikuja kumrudishia Bibi Titi nyumba yake iliyotaifishwa kutokana na azimio. utaona basi Mkapa alikuwa anaendeleza pale alipoachia Mwalimu na Mwinyi.

..Chifu Fundikira sijui matatizo yake na Mwalimu yalikuwa yapi. there are a lot of stories going around.

..Mkapa aliwateua Fundikira,na Makongoro Nyerere, kuwa wabunge ktk mazingira ya kutatanisha sana.

..kwa mtizamo wangu Mkapa alipaswa kumpa "mkono wa pole" Balozi Christopher Kasanga-Tumbo. sielewi ni sababu gani za msingi zilizosababisha akawekwa kizuizini kwa miaka zaidi ya 25.

NB:

..ni kitu gani kilimpelekea Sarakikya kutaka kufanya mapinduzi ya kijeshi?
 
NB:

..ni kitu gani kilimpelekea Sarakikya kutaka kufanya mapinduzi ya kijeshi?

Let me speculate, the Northern Corridor struggle for Power! I will not be suprised to hear that Chief Marealle was behind this.

Kuna jamaa wengi Wameru waliokuwa Jeshini ambao walibidi watimke baada ya Sarakikya kupigwa mtama.

The question becomes, was the campaign to instal a Notherner (Chaga, Meru, Maasai, Pare) and get rid of Nyerere?

Sasa kama theory na speculation yangu ni sahihi, nini hasa lilikuwa chimbuko la nia ya kumuondoa Mwalimu? was it political, economical or struggle for power (Uchifu) in which Marealle was still mad at Mwalimu move towards Uhuru in 1961?

What if Fundikira another chief was behind the unity to dispose Mwalimu and hence the animosity between Mwalimu and Fundikira?

We may have to go back to the council of machifu that was stripped its powers and chiefdom by Nyerere soon after independence!
 
Mwaka jana Wizara ya Mambo ya Nje ilianza kutoa tuzo za kwa mabalozi wanaoitangaza Tanzania vizuri ambayo inaitwa tuzo ya Mrisho Sarakikya...
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom