Gen. Davis Mwamunyange aachie ngazi akawe Mkuu wa Posta Tz

Huwezi kuwa mkuu wa majeshi legelege hivyo, posta barua zikichelewa sio issue,

Kwahiyo posta ndo wanapelekwa watu wafu??
Mtaacha lini kuwa na mawazo mgando kwamba mtu akiharibu mahali flani basi ahamishiwe sehemu nyingine.
Mtu akiharibu lazima aachishwe kazi na aadhibiwe vile vile sio kuhamishwa.
 
Huwezi kuwa mkuu wa majeshi legelege hivyo, posta barua zikichelewa sio issue,

Kwahiyo nchi hii haina watu wengine wenye uwezo wa kufanya kazi hadi tuendelee kung'ang'ania baadhi ya watu hata kama wameonesha udhaifu katika utendaji kazi wao. Badilika jinsi ya kufikiri. Hata huko posta kuna watu wanatuma ujumbe na nyaraka za haraka sema hawana uwezo wa kutumia njia zingine za kisasa zaidi kama fax na kadhalika. Hivyo kufanya uzembe wa kuwapatia huduma ni kutokuwatendea haki. Usifikirie mjini tu. Fikiria huko vijijini kwenu pia. Unadhani huduma za internet na fax zinawafikia. Je wangapi pia wana access na huduma hizo.
Kama mtu ameonesha utendaji mbovu PIGA CHINI tafuta mwingine aendelee na kazi. Hakuna haja ya kuhamishana vitengo ni kuendeleza uzembe tu.
 
Mtazamo ndugu wana jf hii mnaionaje gen davis mwamunyange abadilishiwe post badala ya kuwa mkuu wa majeshi awe mkuu wa posta tz? Kama alivyo fanya mwai kibaki pale kenya ? Kwanini? Mauaji mbeya kmya?,wanajeshi wa congo kuingia hadi kigoma bandarini kmya?,mapigano ya jkt tabora kmya?,mapigano ya jwtz pale ngara na wanajeshi waasi wa burundi kmya?,al-shabab 28,50 kmya' etc sasa je huyu m2 yupo?au alikwishaga kufa zamani? Labda namuonea kumuliza maswali haya?

Mkuu ulifikiria kabla ya ku post, maana wazo lako linakufedhehesha sana. Naomba nikusaidie kwa mapana kuhusu argument yako. Mkuu wa Majeshi siyo mwanasiasa wala msemaji wa jeshi. Yeye ni professional soldier na anashughulikia mambo ya kijeshi na taaluma zake. Mtu ambaye anatakiwa kujibu hayo maswala unayoyauliza ni waziri wa ulinzi. Kwenye hali ya kawaida waziri wa ulinzi anaitisha mkutano na waandishi wa habari au vinginevyo na mkuu wa majeshi anakuwepo kama waziri atamtaka ili kujibu masuala ya kitaalam ya kijeshi endapo waziri atashindwa kuyajibu. Kama nimeleweka vizuri basi mgomvi wako wewe atakuwa ni yule alhaj mtoto ambaye ni waziri wa ulinzi. Tatizo la tanzania ni viongozi wapofu kuongoza raia vipofu, mwisho wa safari yetu ni shimoni
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom