Gen. ABDALMAN SHIMBO UPO WAPI JAMANI....!??

mtemiwao

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
384
46
Haya polisi wamenyanganywa bunduki,raia wanauawa na majambazi na kuporwa mali zao,sasa huyu shimbo aliyeapa kupambana na raia wkt wa uchaguzi yupo wapi jaman atumie maguvu yake kwa majambazi??au kwakuwa ni kgm ni sawa?tunamtaka atokeze na kutupa mkakati wa kulinda wananchi dhidi ya huu uvumjifu wa amani labda kama anawaogopa kwakuwa nao wana silaha kama yeye
 
Jeshi Tanzania lilikuwa enzi za mwl, kwa sasa ni njaa tu na kujuana, hakuna wapiganaji hapo. Na siku vita ikitokea itakuwa aibuuu!!
 
Hili la kutekwa magari ni aibu kwa vyombo vya ulinzi na usalama na wakuu wao. Narudia inawezekana vipi watu wasubiri gari highway waiteke waue watu kisha vyombo hivyo vya uslama havichukui hatua za kimkakati?

Ni aibu inapokuja swala la kuzui demokrasia majeshi yetu yana mikakati mingi tu ikiwa ni pamoja na kununua magari ya upupu na gears zingine kibao. Kama sio unafiki tulionyeswa na vyombo vyetu vya usalama wakati wa uchaguzi na kama havijui nini cha kufanya naomba waende Burundi huko mtaona hususani majeshi yalivyojipanga kulinda raia wake.

Kwa kifupi kwenye highway zote kuna vituo vya kijeshi kila baada ya Km 50 hivi.
 
Kama sio shimbo basi hata huyo mwamunyange atokee atupe ni mkakati gani wa kuzuia huu uvunjifu wa amani ya nchi yetu,otherwise hatutawaelewa hawa wakandamizaji wa demokrasia
 
Hili ni tatizo ambalo viongozi wa Tanzania wanalo...Shimbo aliingilia shughuli ambayo sii yake kwa ile ilikuwa ni jukumu la Polisi. Sababu zilimfanya akurupuke na kuchemcha anazijua yeye mwenyewe..(Hosea nae anaangukia kwenye kundi lakuchemka)

How kama Simbo ana ule uchungu wa kuona amani nchini sasa hivi alikuwa anatakiwa afanye jambo...then ndipo aite vile vyombo vya habari aanze bragging....
 
Wanapenda sana kukimbilia kwenye Siasa wakati majukumu yao yanawashinda na hata Siasa zenyewe pia zinawaumbua. Kwa kifupi alitakiwa ajiuzulu kipindi kile kile cha uchaguzi...
 
Kwani jeshi letu lina vifaa? nasikia ufisadi umeenea mpaka kwa kina Shimbo na wenzake kazi kuiba kodi zetu. Kama ingekuwa ccm ndio wamevamia ungemsikia Shimbo na genge lake lakini ni watanzania halafu hawana faida na serikali ya ufisadi..who cares. Shimbo alikuwa analinda ajira yake atakapo staafu apewe ukuu wa wilaya au mkoa. Siasa za tanzania ni ushenzi mtupu
 
jamani hamjuhi kuwa alikuwa anatetea kitumbua cha shemeji, sasa kashapata kilichobakia ni kula tu kwakwenda mbele, jamaa huko jeshini posho za kujikimu hawajazioni huu mwezi watatu sasa.
 
jamani hamjuhi kuwa alikuwa anatetea kitumbua cha shemeji, sasa kashapata kilichobakia ni kula tu kwakwenda mbele, jamaa huko jeshini posho za kujikimu hawajazioni huu mwezi watatu sasa.
 
Jamani, kumbukeni majukumu ya Majeshi yetu (Polisi, Magereza, Jeshi la wananchi n.k) kuhusu kutekwa kwa basi hilo ni jukumu la Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania haliwezi kukurupuka na kwenda kuwasaka majambazi ambao Polisi wanaweza kuwamudu, chamsingi ni jeshi la polisi lijipange na mbinu za kisasa na kukabiliana na hao majambazi.
 
Jamani, kumbukeni majukumu ya Majeshi yetu (Polisi, Magereza, Jeshi la wananchi n.k) kuhusu kutekwa kwa basi hilo ni jukumu la Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania haliwezi kukurupuka na kwenda kuwasaka majambazi ambao Polisi wanaweza kuwamudu, chamsingi ni jeshi la polisi lijipange na mbinu za kisasa na kukabiliana na hao majambazi.

kwani kwenye uchaguzi jukumu la kulinda ni la jeshi la wananchi? kama aliweza kuingilia kwa kigezo cha uvunjifu wa amani sasa tunataka tumsikie kwa hili,tofauti na hapo tutajua ni mpambanaji na raia wema na si wahalifu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom