Geita: Waziri Mkuu Majaliwa, afungua Ofisi za TRA Chato

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,482
54,839
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa afungua ofisi za TRA, Wilaya ya Chato, mkoa wa Geita
maja1.jpg

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikata utepe kama ishara ya kufungua jengo jipya la ofisi ya TRA, Wilaya ya Chato, Mkoani Geita katika ufunguzi uliofanyika leo mjini Chato.
maja2.jpg

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akihutubia wananchi wa Chato wakati wa ufunguzi wa jengo la TRA wilayani humo mkoani Geita leo.
maja4.jpg

Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere akitolea maelezo ya kina kwa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa namna jengo la ofisi ya TRA Chato litakavyoweza kuchochea ukusanyaji wa mapato katika Wilaya ya Chato.
maja5.jpg

Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa maagizo kwa watendaji wa TRA mara baada ya kupata maelezo ya jengo la ofisi ya TRA kutoka Meneja wa TRA wilaya ya Chato Abdallah Mtumwa
maja6.jpg

Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa ofisi ya TRA katika uzinduzi wa ofisi hiyo uliofanyika leo katika wilaya ya Chato, mkoa wa Geita

Katika Hotuba yake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutowatoza kodi ya majengo wazee walio na umri zaidi ya miaka 60.

====

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa,amesema kuwa kila mwananchi wa Tanzania anawajibika kulipa kodi kwaajili ya ujenzi wa Taifa na kwamba uchumi utajengwa na watanzania kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa kwani kufanya hivyo itawaza kusaidia upatikanaji mkubwa wa kodi.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa zinduzi wa Jengo la mamlaka ya mapato nchini(TRA)Wilayani Chato Mkoani Geita, ambalo ujenzi wake umeghalimu kiasi cha Sh ,Bilioni 1.4.

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa Kila mwananchi ambaye anastahili kulipa kodi la lazima alipe bila ya kushurutishwa kwani ni jambo la kawaidia na kwamba nchi ambazo zimeendelea ni kutokana na wananchi wake kujenga destuli ya ulipaji wa kodi

Pia ameendelea kueleza kuwa Kutokana na maelekezo ya Ilani,Katika Mwaka 2016/17 Kuanzia Mwezi Julai,2016 hadi kufikia mwezi Aprili ,2017 Serikali imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilion 20.7 Sawa na Asilimia 70.1 na kwa lengo la mwaka walijiwekea malengo ya kukusanya Sh,Trilion 29.5,Kati ya makusanyo hayo mapato ya ndani ya kodi yalikuwa ni Sh,Trilioni 11.6 Sawa na Asilimia 77.1 ya lengo la kukusanya Sh,Trilion 15.1

Aidha Waziri Mkuu ametoa Wito kwa Kila mwananchi kuakikisha anadai na kupewa Risiti ya manunuzi ya bidhaa alizonunua na kwamba TRA ihakikishe kila mfanyabishara anakuwa na mashine za kielektroniki.


Kamishina wa mamlaka ya mapato TRA Charles Kichere amesema kuwa Pamoja na kuboresha miundo mbinu ya majengo Mamlaka imeanzisha mifumo ya ukusanyaji mapato kwa njia za kielekitroniki ambazo zitaunganishwa na ofisi hiyo ili kutoa huduma kwa urahisi kama ilivyo kwenye ofisi zingine kote nchini.

"Baadhi ya huduma zitakazotolewa hapa ni kama; Utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), utoaji wa leseni za udereva, huduma za usajili wa magari, ukusanyaji wa kodi za majengo, na kodi zinginezo ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa mujibu wa Sheria"Alisema Kichere.

"Haya yote yanafanyika kwa lengo la kuhakikisha kodi na tozo mbalimbali zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinakusanywa kikamilifu ili kufikia lengo la makusanyo yanayokusudiwa katika mwaka ujao wa Fedha na kuendelea"Aliseongeza Kichere.

Jengo hilo ambalo limefunguliwa leo lilianza kujengwa mnamo tarehe 13 Julai, 2016 na kumalizika tarehe 12 Juni, 2017 ambapo kazi ya ujenzi ilihusisha ujenzi wa jengo la ghorofa moja kama ambalo lina nafasi ya kutosha kutoa huduma zote za kodi pamoja na huduma za kibenki ili kuwapunguzia adha walipakodi kwa kupata huduma zote mahala pamoja.

Kampuni ambayo imejenga jengo hilo ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)na mjenzi ni kampuni ya Mayanga Constructions ambapo katika ujenzi huu zimetumika kiasi cha Takriban Shilingi Bilioni 1.4.

Credit kwa Mkuu Maduka
 
Yani nawaonea wivu watakaopangwa kaz hapo...... Wewe unaweza fanya hata kazi mbili kwa siku au ukawa unafanya mishe zako sengerema jioni unarudi Chattle.......

Tax officer Chattle watainjoi Sana....
Hapa kazi tu..... Kupanga ni kuchagua
 
jengo limegharimu billion 1.4 halafu mapato ya Mwezi chatu shs million 5, hiyo akili au matope
Itajilipa tu huko mbeleni vumilieni mkuu.
Mh. Kikwete alipojenga kiwanda cha kisasa Chalinze cha kutengeneza dawa za kutokomeza mbu mlibeza na kulia sanaaa. Leo hii wote tunaona faida yake. Vumilieni mkuu huwezi jua unaweza kuhitaji huduma ya TRA Chato siku za mbeleni. Karibu Uji wa iliki yakhe.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom