GEITA: Wanafunzi 3 wamefariki baada ya kuzama ziwani, 21 waokolewa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Wanafunzi 3 wa shule ya msingi Butwa iliyopo kata ya Izumacheli, mkoani Geita wamezama katika kisiwa cha Butwa katika Ziwa Victoria walipokuwa wanatoka shuleni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa wilaya ya Geita, Herman Kapufi, kati ya wanafunzi hao 24 waliozama wakiwa ndani ya mtumbwi, 21 wameokolewa jana usiku lakini watatu bado wanatafutwa.

Taarifa zinaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 10 jioni baada ya mtumbwi huo kupinduka katika Ziwa Victoria.

Hata hivyo, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga imeelekea kwenye eneo la tukio kushiriki zoezi la uokoaji.
 
Tukiwa tumevaa mwamvuli wa viwanda tujue tumeruka mambo ya muhimu ikiwemo miundombinu na huduma bora za jamii tutafikaje kwenye cherehani 4 ni kiwanda?
Mungu tusamehe unatuumbua tunaojiona miungu watu
 
Pole kwa waanga wote wa jambo hilo ni vyema serikali ikatoa kipaumbele kwa miunfombinu tz ikiwemo maeneo ya pembezoni mwa nchi au kwenye maziwa na bahari kwani mitumbwi itmikayo kusafiria ni hatar sana
 
Dah! hapo ccm wanasikitika kwa hao 21 kuokolewa maana wangezama wote ilikuwa ni mwanzo mzuri wa kupata rambirambi za kujenga daraja eneo hilo.. chanzo cha mapato kimepungua.
 
Hivi ni wanaojadili humu ndani hawana akili au ni pumbavu kama pumbavu wengine kila siku mungu kawapenda walale salama waweke mahali pema badala kujadili tatizo linalosabisha na kuandamana kupinga ujinga huu watu wanaojadili Na kuandika ujinga tu
 
Back
Top Bottom