Geita: Wamachinga wametakiwa kuhama maeneo yasiyo rasmi kabla ya Novemba 10, 2021

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amewataka wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga kufuata utaratibu wa kuelekea maeneo ambayo yamepangwa kwaajili ya biashara zao na kwamba ifikapo Novemba 10, 2021 watafunga maeneo yote ambayo sio rasmi kwaajili ya biashara zao.

"Ndugu zangu wafanyabiashara wa soko la Maua niwaombe mfuate utaratibu uliowekwa na serikali kwa kufuata maeneo sahihi yaliyopangwa, ni muda mrefu sasa tukizungumza nanyi ikiwa ni pamoja na kuwaomba muondoke eneo hili maana sio rasmi kwaajili ya biashara"RC Rosemary Senyamule
 
Back
Top Bottom