Geita: Wafuasi wa CCM wavamia mkutano wa CHADEMA na kumjeruhi vibaya Askari Polisi

nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
1,104
559
Imetokea jioni ya leo kijijini Nyambogo jimbo la Geita Mjini ambapo Mgombea wa CHADEMA Rogers Luhega alikuwa na Mkutano wa Kampeni.

Wakiongozwa na Balozi wao walianza kushambulia watu kwa mawe na kumlazimu askari aliyekuwepo kujaribu kuwadhibiti na kumzidi nguvu wakamjeruhi na kuharibu pikipiki yake na sasa kakimbizwa kituo cha afya Kasamwa kwa Matibabu.

Wiki iliyopita mgombea huyo pia msafara wake ulishambuliwa Mjini Geita wakati akipiga kampeni za mtaa kwa mtaa.

Majuzi pia alifanyiwa vurugu Kijiji Cha Buhalahala.

Kwa ujumla hali Ya CCM ni mbaya Jimboni humo.

UPDATES

Hali ya afande ni mbaya yupo ICU hospitali ya mkoa wa Geita Muda Huu.Taarifa Mpya Nikwamba Watuhumiwa 5 Wamekamatwa,ng Pia Vurugu Zingine Zilitokea Jana Kijiji Cha Igate Jimbo La Geita Vijijini Ambapo Mgombea Wa Ccm Ni Ndg.Musukuma Kufika Kijijini Hapo Akiwa Na Kundi La Vijana Wake Kuwaamuru Washushe Bendera Za Chadema Na Kuzuka Mapigano Makali Kwa Wafuasi Wa Vyama Hivyo Na Kupelekea Majeruhi Kadhaa.
 
Imetokea Jioni Ya Leo Kijijini Nyaseke Jimbo La Geita Mjini Ambapo Mgombea Wa Chadema Rogers Luhega Alikuwa Na Mkutano Wa Kampeni.Wakiongozwa Na Balozi Wao Walianza Kushambulia Watu Kwa Mawe Na Kumlazimu Askari Aliyekuwepo Kujaribu Kuwadhibiti Na Kumzidi Nguvu Wakamjeruhi Na Kuharibu Pikipiki Yake Na Sasa Kakimbizwa Kituo Cha Afya Kasamwa Kwa Matibabu,wiki Iliyopita Mgombea Huyo Pia Msafara Wake Ulishambuliwa Mjini Geita Wakati Akipiga Kampeni Za Mtaa Kwa Mtaa,na Majuzi Pia Alifanyiwa Vurugu Kijiji Cha Buhalahala.Kwa Ujumla Hali Ya Ccm Ni Mbaya Jimboni Humo.
Hiyo tabia yao hawajaanza leo au jana , ni kitambo sana .
 

Attachments

  • attachment-5.jpeg
    attachment-5.jpeg
    12 KB · Views: 1,930
Nadhani Alidhani Watamsitahi Kama Mwenzao,but Wakamchenjia Ghafla

crowd control yoyote ile haihusishi askari mwenye bunduki, ni kwa nia njema kabisa naamini. maana kama angekuwa na bunduki, story hapa ingekuwa ya kulaani ile mbaya
 
crowd control yoyote ile haihusishi askari mwenye bunduki, ni kwa nia njema kabisa naamini. maana kama angekuwa na bunduki, story hapa ingekuwa ya kulaani ile mbaya
mbona ile crowd ya iringa walitumia mzinga kumuua mwangosi?
 
mbona ile crowd ya iringa walitumia mzinga kumuua mwangosi?

Pale hapakuwa na mkutano ulioruhusiwa unaohitaji crowd control, ni chadema kulazimisha hivyo vyombo vya dora wakatumia nguvu kuwazuia kufanya shughuli za kisiasa.

Kama huamini, anza leo kuchunguza kuanzia mikutano ya wagombea urais, ubunge na udiwani. Ukiona kuna askari mwenye bunduki yuko kwenye crowd control, piga picha kisha nitafte inbox mkuuu
 
na hao wahusika wa hizo vurugu hawatachukuliwa hatua kamwe. na tume itasema ni mikogo tu ya kampeni. kwa uchaguzi wa mwaka huu bila ccm kubebwa na dola haishindi....
 
Wanategemea hesabu fake za vituo hewa wapate kura za ziada!!
Tafadhari NEC msiruhusu hii kitu kuleta balaa.
Idadi ya vituo halisi iwekwe wazi sio kanyabwoya from 53,000 to 72,000 polling posts???
Msituletee balaa wandugu kuweni wakweli, mtu akishinda ashinde kwa kura halali, sio magumashi!!
 
Wagombea Wa Chadema Wa Majimbo Ya Geita Mjini Ndg Rogers Na Mangilima Wa Geita Vijijini Wameitwa Ofsini Kwa RPC wa Geita Wanahojiwa Muda Huu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom