Geita: Wafanyabiashara wafunga maduka wakishinikiza mwenzao mgeni kulipa kreti ya soda kama kiingilio

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wafanyabiashara kijiji cha Nyamigana kata ya Kagu wilayani Geita wamefunga maduka yao na kugoma kuendelea na biashara baada ya mfanyabiashara mgeni aliyehamia kijijini hapo kugoma kutoa kreti moja ya soda kama kiingilio.

Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Mugwe Sabuni amesema wafanyabiashara hao zaidi ya 20 wamefunga maduka yao kwa siku nne sasa wakishinikiza mfanyabiashara huyo, Frank Lucas kulipa Sh12, 000 ya kreti ya soda kama kiingilio kitakachomwezesha kuendelea na biashara.

Sabuni amesema amefanya jitihada kutatua mgogoro ili wananchi zaidi ya 300 wa kijiji hicho wapate huduma bila mafanikio baada ya pande zote mbili kuwa na msimamo usiobadilika.

Mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo Robart Chale amesema wana utaratibu wao wa kulipia kiingilio kinachojenga umoja.

"sisi tunataka alipe kama halipi aondoke kwenye eneo letu maana huu ni utaratibu wetu akileta kreti ya soda wote tunakunywa" amesema.

Amesema wapo wafanyabiashara 40 na kila mmoja lazima alipe kiingilio kwenye kikundi na ambae hayupo tayari kulipa aondoke kwenye kijiji hicho.

Mfanyabiashara anayetakiwa kulipa Sh12,000, Frank Lucas amesema hayupo tayari kulipa kiingilio hicho kwa kuwa hakipo kwenye utaratibu wa malipo ya Serikali.

“Nililipa Sh20,000 kama kiingilio cha kijiji na mtendaji alinipa taratibu zote, kwenye hizi taratibu hakuna kiingilio cha wafanyabiashara," amesema Frank.

Mkazi wa kijiji hicho, Eliakim Kasoga amesema mgomo huo umewaathiri wananchi kwa kuwa hadi maduka ya dawa za binadamu yamefungwa na hawawezi kununua kitu chochote, kulazimika kwenda katika vijiji jirani.
 
Naungana na mfanyabiashara mgeni. Kama hataki kujiunga na umoja wao kwa nini wamlazimishe? Hao watu ni wapumbavu. Jamaa afungue duka lake apige kazi. Tena kipindi hiki ata make sana.
Wewe mdanganye tuuu.
Unayajua maisha ya Kijijini wewe. Atatengwa mpaka ahame yeye mwenyewe, hapo ndio atajua kati ya 12,000 na Umoja na Mshikamano kipi bora. Kuuushi Utamaduni ni jambo jema kuliko kuuukana.
 
Huu ujinga ndiyo nausikia leo. Hao wafanyabiashara waliofunga maduka ni wa kuwafutia leseni za kufanya biashara ili waende wakalime. Wasukuma matoroli ni watu ambao elimu imewapita kushoto
 
Wewe mdanganye tuuu.
Unayajua maisha ya Kijijini wewe. Atatengwa mpaka ahame yeye mwenyewe, hapo ndio atajua kati ya 12,000 na Umoja na Mshikamano kipi bora. Kuuushi Utamaduni ni jambo jema kuliko kuuukana.
Ndiyo maana maendeleo yapo mjini. Vijijini ni shida tu hakuna lolote, watu hawana elimu wanaishi ilimradi siku ziende. Huku mjini kila mtu yupo huru hakuna huo ujinga
 
Wafanyabiashara kijiji cha Nyamigana kata ya Kagu wilayani Geita wamefunga maduka yao na kugoma kuendelea na biashara baada ya mfanyabiashara mgeni aliyehamia kijijini hapo kugoma kutoa kreti moja ya soda kama kiingilio

Amesema wapo wafanyabiashara 40 na kila mmoja lazima alipe kiingilio kwenye kikundi na ambae hayupo tayari kulipa aondoke kwenye kijiji hicho.
Wafanyabiashara wapo 40, kreti moja la soda lina chupa 24, je wanagawana soda kwenye vikombe?
 
Hawa bado wanaishi primitive communalism. Nawaza huu uchumi wa kati tutafikaje kama wananzengo wengine bado wanaishi maisha ya karne ya 16?
 
Back
Top Bottom