Geita: Wachimbaji wadogo wavamia mgodi wa Buckreef

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,221
25,691
Wachimbaji wadogo wa madini wa huko mkoani Geita wamevamia mgodi wa Buckreef. Wamedai kuwa Kibali cha Mwekezaji kilishaisha na wananchi hawakulipwa fidia ya maeneo yao

Mmoja wa wawekezaji katika mgodi huo ni STAMICO. Mkuu wa Wilaya ya Geita,Herman Kapufi amewataka wachimbaji hao wadogo kuondoka mgodini hapo ndani ya siku tatu kupisha maelekezo ya Serikali

Chanzo: ITV Habari
 
mlimshangilia sasa ngoja kiki ziishe aseme wote wenye nyumba zenye mabati ya "sauzi" ni majizi na hawana vibali vya kuezeka kwa mabati hayo...hapo ndipo mtakapotuelewa kwa nini tuna mashaka na bwana yule.
 
Hilo ni eneo la stamico; wakaingia joint venture na kampuni nyingine. Tatizo linaonekana wote hawana mtaji kuliendeleza. Sasa nahisi leseni yao imepita mida yote ya extension. Na kama nihivyo kisheria inabidi wapokonywe. Nipo tayari kusahihishwa
 
Wachimbaji wadogo wa madini wa huko mkoani Geita wamevamia mgodi wa Buckreef. Wamedai kuwa Kibali cha Mwekezaji kilishaisha na wananchi hawakulipwa fidia ya maeneo yao

Mmoja wa wawekezaji katika mgodi huo ni STAMICO. Mkuu wa Wilaya ya Geita,Herman Kapufi amewataka wachimbaji hao wadogo kuondoka mgodini hapo ndani ya siku tatu kupisha maelekezo ya Serikali

Chanzo: ITV Habari
Petro, nimesoma huko nadhani ghana/nigeria??? (nitacheki if true) kampuni hizi za kigeni zimeenda mahakamani kuzishitaki serikali kwa kushindwa kuwapatia ulinzi wa mali zao na kuruhusu wanachi wavamie migodi yao. Serikali zililipa kwa uzembe wa kutotoa ulinzi! haya mambo watu wanashangilia yataleta taabu!
 
tatizo ilisemwa hakunaga formula ya kukamata mwizi!! Sasa kunamhindi anauza spea bei kubwa ya wizi...ngoja tukamshike kwafomula yetu!! Viongozi wachunge kauli zao
 
Tumeruhusiwa bwana, tumeambiwa hawa ni wezi hawana hata leseni wala usajili brela.... Hahahahaha tz bwana..
 
Back
Top Bottom