Geita: TAKUKURU yawadaka wafanyakazi watatu wa TRA wakiomba rushwa ya zaidi ya Tsh milioni 100 kutoka kwa wafanyabiashara

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
874
1,000
Watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Geita wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa mahojiano kwa tuhuma za kuwafanyia makadirio ya juu wafanyabiashara na badaye kuwashawishi kutoa rushwa ili wawakadirie kadirio la chini.

Kaimu Ofisa Takukuru mkoa wa Geita, Mwamba Masanja akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Juni 18,2019 amewataja wanaoshikiliwa ni Sadick Lutenge, Amza Rugemalira na Elias Msula

Amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kinyume na kifungu cha 15(1) (a na b) na (2) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Miongoni mwa tuhuma zinazochunguzwa na Takukuru ni maofisa hao kuomba rushwa zaidi ya Sh100 milioni kutoka kwa wafanyabiashara watatu tofauti kwa kipindi cha Aprili na Juni mwaka 2019.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumekuja siku chache baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kukutana na wafanyabiashara na kuelezwa changamoto zao ambapo miongoni mwa changamoto walizozieleza ni kukadiriwa kodi kubwa na maofisa wa TRA.

Chanzo: Mwananchi
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
5,666
2,000
Sukuma ndani.
Ingekua Dar wangepelekwa Keko halafu mle keko wanapangiwa chumba kimoja na wahuni walioshindikana. BW. Jela akitaka rushwa kutoka kwa watuhumiwa wenye pesa anawapanga na wahuni. Watakachokiona humo kesho lazima watoe rushwa ili watoke sehemu ngumu kwenda sehemu ya kawaida japo wako ndani ya jela.
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
53,548
2,000
TRA staff ni waroho wezi walafi
Juzi juzi tu ikulu kulikuwa na mkutano rais akiwemo wamesemwa sana!
Hawa Inabidi sasa tuwatandike bakora hadharani

Ova
 

Easy E

JF-Expert Member
Feb 19, 2012
1,368
2,000
Du juzi tu haya masuala yametoka kuzungumziwa..halafu jamaa wanapigaga mihela mirefu...m100 kiraisi raisi tu..
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,201
2,000
Wamekuwa wanafanya hivi kwa muda mrefu.. hawaridhiki na wanachopata.. wao kukomoa tu.. hayo matukio itakuwa watu wameanza kuwashitaki wakijua sasa lawama zitasikilizwa. Kuna wengi tu.. watoe namba watu wapige kama hawatapokea jina la mtu mara hata 500..
 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
14,829
2,000
Inatakiwa kureview sheria na hasa kwa kuwalenga wao peke yao, yule mzee wa Mbeya alisema kabisa serikali inapata fedha kidogo sehemu kubwa wanakula vijana, mwandishi wa habari hii alitakiwa kuandika umri wa hao waomba rushwa tafiti zianzie hapo
 

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
2,000
Inatakiwa kureview sheria na hasa kwa kuwalenga wao peke yao, yule mzee wa Mbeya alisema kabisa serikali inapata fedha kidogo sehemu kubwa wanakula vijana, mwandishi wa habari hii alitakiwa kuandika umri wa hao waomba rushwa tafiti zianzie hapo
Kuna kijana mmoja wa tra huwa anawaambia watu ametumwa na mzazi wake kuja kutafuta fedha . sasa sisi huwa tu nashangaa katumwa na serikali au mzazi wake . hao vijana ni shida
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,232
2,000
Hivi hawa TRA staff hawajifunzi kwa wenzao....
Watajifunzaje wakati wao ndiyo wamechukuliwa kama "shamba darasa" la kufundishia kanuni mpya za maadili?

Walianza kuomba hiyo rushwa mwezi April kabla hata ya kikao cha mheshimiwa na wafanyabiashara.
 

MC44

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
1,550
2,000
Sukuma ndani.
Ingekua Dar wangepelekwa Keko halafu mle keko wanapangiwa chumba kimoja na wahuni walioshindikana. BW. Jela akitaka rushwa kutoka kwa watuhumiwa wenye pesa anawapanga na wahuni. Watakachokiona humo kesho lazima watoe rushwa ili watoke sehemu ngumu kwenda sehemu ya kawaida japo wako ndani ya jela.
Ahahaha kosa la rushwa unatoa rushwa tena
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom