Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,808
- 11,973
Miradi 15 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 18.3 Mkoani Geita imebainika kuwa na upungufu wa kutozingatiwa kwa vigezo na masharti ya mikataba, hiyo imesababishwa na kukosekana kwa usimamizi wa wataalamu wa Halmashauri.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imebainisha na kueleza hayo yamebainika katika utafiti wao uliofanyika Januari hadi Machi, 2022, wakieleza kuwa kuna baadhi ya mafundi walioshinda zabuni za ujenzi hawajaonekana eneo la mradi, wamewaacha mafundi wasaidizi bila usimamizi wala maelekezo eneo la ujenzi.
Mkuu wa #TAKUKURU Geita, Leonidas Felix amesema mbali na hapo, kuna miradi minne ya elimu yenye thamani ya Tsh milioni 340 imebainika kuwa na viashiria vya ufujaji na ubadhirifu wa fedha, ameeleza kuwa uchunguzi unaendelea Mkoani hapo.