GEITA: Papa Francis amteua Padre Flavian Kassala kuwa Askofu

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg


28/04/2016 09:49

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Flavian Matinde Kassala kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Geita, Tanzania.

Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Kassala alikuwa ni mkurugenzi wa Kitivo cha Stella Maris, Mtwara, Chuo kikuu cha Mtakatifu Agostino cha Tanzania.

Askofu mteule Kassala alizaliwa tarehe 4 Desemba 1967, Parokia ya Sumve, Jimbo kuu la Mwanza. Alipata masomo yake ya Sekondari kutoka Seminari Ndogo ya Mtakatifu Pio wa X, iliyoko Makoko, Jimbo Katoliki la Musoma.

Alijiendeleza zaidi kwenye Seminari Ndogo ya Sanu Jimbo Katoliki Mbulu. Akapata majiundo ya falsafa kutoka Seminari ya Mtakatifu Anthony wa Padua, Maarufu kama Ntungamo, iliyoko Jimbo Katoliki la Bukoba.

Askofu mteule Kassala alijipatia majiundo yake ya kitaalimungu kwenye Seminari kuu ya Mtakatifu Paulo, maarufu kama Kipalapala iliyoko Jimbo kuu la Tabora.

Baada ya safari hii ndefu katika maisha na wito wa kipadre, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 11 Julai 1999 kama Padre wa Jimbo Katoliki Geita.

Baada ya Upadrisho kati ya mwaka 1999 hadi mwaka 2002 alikuwa ni Paroko usu, Parokia ya Sengerema, Jimbo Katoliki la Geita. Mwaka 2002- 2004 alikuwa ni mlezi na Padre wa maisha ya kiroho Seminari ndogo ya Bikira Maria Malkia wa Mitume, Jimbo Katoliki Geita pamoja na kuwa ni Mkurugenzi wa Jimbo Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa.

Askofu mteule Flavian Kassala kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2012 alitumwa na Jimbo kujiendeleza zaidi katika utume wa vijana na katekesi katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Wasalesiani, kilichoko mjini Roma na hapo akajipatia shahada ya nguvu ya uzamivu.

Akiwa mjini Roma kwa miaka kadhaa alishiriki kuandaa makala ya vijana Radio Vatican, makala zilizokuwa zinagusa maisha na changamoto za vijana wa kizazi kipya.

Kunako mwaka 2013 Askofu mteule Kassala akarejea Jimboni Geita na huko akapewa dhamana ya kuratibu miradi ya Jimbo.

Kuanzia mwaka 2013- 2015 akepewa dhamana ya kusimamia na kufundisha Chuo Kikuu cha SAUT, Kitivo cha Utalii, Arusha. Kunako mwaka 2015, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania likamhamishia Kitivo cha Stella Maris, Mtwara kama mkurugenzi.

Itakumbuka kwamba, Jimbo Katoliki Geita limekuwa wazi kuanzia tarehe 14 Machi 2014, baada ya Baba Mtakatifu Francisko kumhamisha na kumpandisha hadhi Askofu Damian Dallu kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
Cc:
Padre Richard A. MjigwaChuo kikuu cha SAUT

Askofu mkuu Damian DalluJimbo Katoliki Geita, Tanzania

Askofu Flavian M. Kassala28/04/2016

09:49Mitandao ya kijamii:
RADIO

=======================

Habari wanaJF,

Hatimae kiongozi wa Wakatoliki duniani Papa Francis amteua mhadhiri wa Chuo Kikuu kishiriki cha Stella Maris Mtwala, Flavian Kassala kuwa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Geita.

View attachment 343035

Kila la kheri Askofu Flavian Kassala katika utendaji wako kwa nafasi hiyo mpya.
 
Kanisa likiwa lina Demokrasia ya kuchaguana huwa linakumbwa na migogoro ya mara kwa mara...Napenda mfumo wa kanisa katoliki akiteuliwa mtu hakuna anayehoji...
 
Habari wanaJF,

Hatimae kiongozi wa Wakatoliki duniani Papa Francis amteua mhadhiri wa Chuo Kikuu kishiriki cha Stella Maris Mtwala, Flavian Kassala kuwa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Geita.

ddddd.jpeg


Kila la kheri Askofu Flavian Kassala katika utendaji wako kwa nafasi hiyo mpya.
 
Kanisa likiwa lina Demokrasia ya kuchaguana huwa linakumbwa na migogoro ya mara kwa mara...Napenda mfumo wa kanisa katoliki akiteuliwa mtu hakuna anayehoji...
Huu mfumo unaondoa ngumi za hapa na pale kama za kule Mwanga ambako ilimbidi wakati ule Mrema akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani aingilie kati ugomvi wa Watani zake Wapare
 
Nimependa kiswahili cha Padre nwandishi wa wasifu wa askofu mteule. "Majiundo ya kitaali mungu"
 
Hao mdio rc bwana, wanapigwa vita, wanatukanwa, wanakebehiwa ila wao wanaziba masikio na kusonga mbele kimwili na kiroho, hongera askofu mteule
 
Kila la heri Askofu Mteule Flavian.

Naombeni wenye kuelewa hiki kiswahili wanisaidie...."majiundo"...."kitaalimungu"...haya maneno yanamaanisha nn?
 
leo mkuu wa chuo hapa stella maris-mtwara mida ya sa8 alituita wanafunz na walimu wote, moja ya habari tulizoambiwa n kuhusu uteuz wa huyu askofu. nae alikuwepo na ameongea neno kidogo. tumefurahi sana.
 
Mungu amwekee mkono wake Mtakatifu ampake mafuta na amjaze baraka na kumpa nguvu yakuifanya kazi aliyomtuma.Amina.
 
Kila la heri Askofu Mteule Flavian.

Naombeni wenye kuelewa hiki kiswahili wanisaidie...."majiundo"...."kitaalimungu"...haya maneno yanamaanisha nn?
Majiundo= Malezi ya kiroho ktk kuufikia wito wa Upadre

Kitaalimungu= Theolojia/Taihudi(Elimu ihusuyo mambo ya Mungu)
Mkuu Kinyungu umenipata?
 
Baba, Papa Francis, tunakushukuru kwa kumchagua mtumishi waMungu aliye mwema mbere zako, na mbere zangu, na mbere za Mungu wetu, namtakia kira la heri Kissala.
 
Kuna vitu kama mheshimiwa padre, paroko usu na kitivo cha Stella Maris hapo sikuelewa vizuri.
 
Plato wakati anaanzisha chuo kikuu cha kwanza duniani kilichofahamika kama "Academy" lengo Lake kubwa lilikuwa ni kuwajengea watu uwezo wa kufikiri kwa mantiki. Nafarijika kuona mwalimu wa kuwasaidia wengine kufikiri kwa mantiki anapewa nafasi ya kuongeza kondoo wa Bwana.

Tunainua mikono juu na kumshukuru yeye alie juu akakusimamie "Mhashamu Baba Askofu" ukatende kwa unyenyekevu mkubwa haki kwa wale watakaopata huduma yako.
 
Back
Top Bottom