Geita: Mume amchinja mke wake na kisha yeye kujichoma kisu tumboni

exalioth

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
2,189
3,684
Imetokea katika wilaya ya Mbogwe kata ya Lulembela mkoani Geita, ambapo tukio limetokea mida ya saa 6 mchana.

Wawili hao wenye watoto saba imegundulika baada ya mtoto kutoka shule na kukuta nyumba imefungiwa ndani huku mziki ukiwa unapigwa (sabufa) badae mtoto akaenda kuita majirani baada ya kubomoa mlango wakakuta maiti ya mwanamke akiwa amejinjwa shingoni na pia maiti ya mwanaume huyo akiwa na alama ya kisu shingoni na tumboni kilipokuwa kisu.

Tayari polisi wameshafika eneo la tukio.


IMG_20211011_170915_450.jpg
MME KAMCHINJA MKE WAKE
 
Huko kaskazini mna mambo ya ajabu Sana endeleeni kuuwana ....tu ...maana mnajiita matajiri ...

Shubamit
 
Mungu atusaidie wazazi kuwa na hekima, kuacha ubinafsi na kutambua kwamba kuna watoto ambao tumewaleta duniani na wanatutegemea kwa malezi na makuzi yao kwa asilimia 100%

Sasa unaua mama na wewe unajiua unamwachia nani watoto 7

Pole sana kwao watoto jamani
 
Shinyanga; Geita; Tabora maeneo ya kuangalia kwa jicho la tatu kwa masuala ya mahusiano na kifamilia. Inatakiwa awareness ya hali ya juu sana kwa hayo maeneo.

Iundwe Kanda Maalum ya Ustawi wa Jamii wakatie kambi huko Mfumo dume umetamalaki waondolewe ujinga uliowajaa vichwani.

Hata wamasai wanaoonekana kama makatili lakini wanaheshimu sana ndoa zao na wanawake kwa ujumla; husikii Masai kachinja mke au mpenzi pamoja na kwamba sime haiko mbali ni hapo kiunoni tu! Kanda ya Ziwa tunakwama wapi.
 
Back
Top Bottom