Geita: Mke wa mfanyakazi wa GGM anyongwa

Hapo kwenye sadaka hilo halipo kwao sadaka kwanza na ndiyo muhimu mkuu halafu unajua hawa wachungaji nao ndiyo wanachangia kuweka haya mawazo ya kishirikina kwa waumini wao.

Utasema mimi muongo sasa wewe siku jaribu kufuatilia kile kipindi cha yule jamaa Mwamposa yaan asilimia 95 kama sio na zaidi anawaaminisha wafuasi wake kuwa mambo mabaya yanayowatokea ni nguvu za Giza utasikia mara katapika nyoka mara paka cjui amekufa mara mtu ametoa haja yenye hirizi sasa unategemea nini mkuu hiyo dhana haiwezi kuisha.
Sio hao wachungaji tuu, mashehe nao wanahubiri majini freemason na wengine wana vipindi kwenye tv. Haya ni madude unapandikiza kwenye vichwa vya watu
 
Sio hao wachungaji tuu, mashehe nao wanahubiri majini freemason na wengine wana vipindi kwenye tv. Haya ni madude unapandikiza kwenye vichwa vya watu
sasa kwa mtindo huu unafikiri hii dhana itakuja isha hakuna mchungaji anamuaminisha mfuasi wake haya mambo na huyo mfuasi naye anaenda kuwaambie na kuwaaminisha watoto wake kile kile alichoambiwa hapo cheni tayar mzunguko unaenda hivyo vizazi na vizazi
 
Bado kamanda Ziro yupo ofisini? Anasubiri mpaka tufe wote abaki mwenyewe?
 
Bado kamanda Ziro yupo ofisini? Anasubiri mpaka tufe wote abaki mwenyewe?
Mnamuonea sana siro utadhani anawatuma,, uhalifu kama huo hauwezi kutabiri utatokea wapi na saa ngapi,,,
Kila abiria achunge roho yake,,
Mchina amesaidia kutuletea camera za surveillance za bei nafuu, zitasaidia at least hata ukiuliwa wamkamate mhalifu,,
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linaendelea na uchunguzi kufuatia tukio la mauaji ya mke wa mfanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa GGM, aliyekutwa amenyongwa nyumbani kwake jana Februari Mosi, 2022, majira ya saa 8:00 mchana.

Taarifa ya mauaji hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe na kusema tukio hilo limetokea mtaa wa Majengo, Kata ya Kanyara, halmashauri ya mji Geita, ambapo mwanamke huyo aitwaye Anjela Anteli (43), alikutwa amenyongwa.

Kamanda Mwaibambe, amesema kuwa mtu wa kwanza kugundua alikuwa bodaboda ambaye aliagizwa kupeleka maziwa nyumbani hapo na alipofika akagonga mlango bila mafanikio.
Duh pole familia
 
Pia kwa mujibu wa clouds,mkurugenzi wa shule inayomilikiwa na Meya wa Arusha ameuawa kwa kukatwa kichwa chake,chanzo hakieleweki na polisi wanaendelea na uchunguzi..

Haya mambo yamekuwa kama kipindi cha maalbino au kuna kundi la kihalifu linataka kuitikisa serikali.
 
Yuko wapi Zerro na intelenjisia yake au inaishia kwa Mbowe tuu?
Mauaji kila Kona nchini na mapolisi kama alivyosema M/rais nao wanashiriki kikamilifu.
Zerro kazi imekuwa mzigo sana kwake ni wakati astaafu Sasa.
 
ni mfanyabiashara wa mgodi au mfanyakazi wa mgodi.maana huo mgodi ufanyi biashara na wafanya biashara wa madini.
GGM ina weza kukupa tenda ya manunuzi ya vitu vingine na sio biashara ya wanacho kifanya
kweli wewe ni chizi com
 
Hivi vifo vinaonyesha wazi yule BEPARI walimuuaga na kama ile ya POPO BAWA mpaka watangaze ndio hivi vifo vya kuuwana VITAKOMA.. tangazeni jamani tutaisha
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linaendelea na uchunguzi kufuatia tukio la mauaji ya mke wa mfanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa GGM, aliyekutwa amenyongwa nyumbani kwake jana Februari Mosi, 2022, majira ya saa 8:00 mchana.

Taarifa ya mauaji hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe na kusema tukio hilo limetokea mtaa wa Majengo, Kata ya Kanyara, halmashauri ya mji Geita, ambapo mwanamke huyo aitwaye Anjela Anteli (43), alikutwa amenyongwa.

Kamanda Mwaibambe, amesema kuwa mtu wa kwanza kugundua alikuwa bodaboda ambaye aliagizwa kupeleka maziwa nyumbani hapo na alipofika akagonga mlango bila mafanikio.
Hapa naona aliyefanya tukio ni mtu wa karibu na hii familia
 
Back
Top Bottom