Geita: Marufuku kwa watumishi kufuga ndevu na kuvaa t-shirt kazini

As Salafiyyu91

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
2,537
2,526
Kwa watumishi wote kutoka kwa RS - GEITA ni Marufuku kwa Watumishi wa Umma kufuga ndevu na kuvaa T-shirt sehemu za kazi.

Imeelezwa kuwa tabia ya kufuga ndevu na kuvaa T-shirt inaendekezwa na Wanaume huku wakijua kuwa ni ukikwaji wa kanuni za kiutumishi wa Umma

Hivyo hatua Kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa wafugaji wa ndevu na wavaaji T-shirt sehemu za Kazi

Tafadhali pindi uonapo tangazo hili mjulishe na mwenzio asijepata matatizo kazini.
IMG_20190521_135626.jpg

Source : Clouds- TV
 
Serikali ya Zanzibar wanakataza watu kufungua biashara kisa ni Ramadhani, Waislam wameliunga mkono kwa nguvu kubwa

Ila Waislam hao hao wanalalamikia hili kuwa serikali inakandamiza uhuru wao wa Dini, very funny

Kuna kipindi walikuja juu sana baada ya shule moja binafsi kukataza hijab

Ila wamiliki wa shule za Kiislam analazimisha kila mwanafunzi kuvaa hijab, na wanaliunga mkono kwa nguvu zote
 
hahhahahaa kuna ustaadh kamuudhi na mtu hapo geita
Yani huyo mtu aliyekataza Ana bahati huu ni mwezi mtukufu lakini ungekuwa sio mwezi mtukufu Waislam wangemshatika kwa Mwenyezi Mungu yeye ndio anajua atamfanya nini kiumbe uyo jeuri, kiburi aliyelewa na madaraka
 
Hanyoi mtu hapa Waraka wa mavazi kwa watumishi wa Umma uko wazi sana na haujakataza kufuga ndevu bali umekataza kuwa na ndevu chafu zisizo na matunzo sasa watumishi wafuate Waraka au yeye ?
Ni vizuri mkafata waraka wa mavazi, Kama unatunza ndevu zako vzr sidhani km italeta shida. Na kwanini isiwe nchi nzima? Jamaa kaamua tu kuwakera
 
Hiyari ya mtu hao jamaa ndio sheria zao kwa wanaojua uzito wa kufuga ndevu hawawezi kwenda huko
Na kwenye sheria za Utumishi wa umma pia wamekataza kufuga ndevu na baadhi ya aina za mavazi. Hivyo ni either kuzifuata kwa hiari na kuwa mtumishi serikalini, Au kuamua kufuga ndevu na kujiajiri au kutafuta katika sekta na mashirika binafsi yanayokubali kufuga ndevu.
 
Back
Top Bottom