Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,883
MTU MMOJA ASADIKIWA KUFA KWA KUPIGWA RISASI YA USO NA POLISI
POLISI wilayani Geita, mkoani Mwanza wamelazimika kutumia risasi za moto kupambana na wananchi zaidi ya 200 ambao ni wachimbaji wadogo wa madini ambao wanadaiwa kuvamia machimbo ya madini katika Kijiji cha Nyaruyeye, Kata ya Nyarugusu, ambayo yalifungwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo hali iliyofanya shughuli za kiuchumi na kijamii kusimama kwa muda. Katika vurugu hizo, mtu mmoja aliyefahamika kama Jahaja Chandarua (27) alikufa baada ya kupigwa risasi na polisi sehemu ya paji la uso ambayo ilimpasua na kutokea upande wa pili, huku Mkuu wa Kituo cha Polisi Nyarugusu (OCS), Ibrahim akijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu ya mkono wake wa kulia na wananchi hao.
Vurugu hizo ambazo zilianza juzi saa 2:00 usiku ziliendelea hadi jana jioni na kufanya shughuli za kijamii na kiuchumi katika kata hiyo na vijiji jirani na machimbo hayo, kusimama kwa muda huku polisi wakiendelea kutumia nguvu kudhibiti wananchi hao. Hiyo ni mara pili kwa wananchi hao kukosa uvumilivu na kuamua kuvamia machimbo hayo, kwani wiki moja iliyopita wananchi wengine zaidi ya 3,000 walivamia machimbo hayo kupinga kupewa mwekezaji huku wao wakishindwa kunufaika na rasilimali hizo za taifa.
Chanzo cha wananchi kuvamia
Tangu Serikali ilipofunga machimbo hayo, wananchi ambao walikuwa wakiyategemea kufanya shughuli zao za kiuchumi, wamekuwa wakiahidiwa kila mara kwamba, yangefunguliwa baada ya muda fulani, lakini imeshindwa kufanya hivyo.
Kutokana na danadana hizo, ndipo juzi usiku wananchi hao walipoamua kukusanyika na kuandamana hadi kwenye machimbo hayo ya Nyaruyeye na kuanza kupambana na polisi wanaolinda eneo hilo.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nyarugusu, Thobias Ikangala alisema wachimbaji hao baada ya kufika eneo hilo walivunja uzio uliowekwa na mwekezaji kabla ya kutawanywa na polisi wanaolinda machimbo hayo na ndipo mapambano yalipoanza kati yao na polisi.
Mwananchi