Geita: Mapambano makali polisi, raia mgodini - raia mmoja auawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Geita: Mapambano makali polisi, raia mgodini - raia mmoja auawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Oct 7, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MTU MMOJA ASADIKIWA KUFA KWA KUPIGWA RISASI YA USO NA POLISI
  POLISI wilayani Geita, mkoani Mwanza wamelazimika kutumia risasi za moto kupambana na wananchi zaidi ya 200 ambao ni wachimbaji wadogo wa madini ambao wanadaiwa kuvamia machimbo ya madini katika Kijiji cha Nyaruyeye, Kata ya Nyarugusu, ambayo yalifungwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo hali iliyofanya shughuli za kiuchumi na kijamii kusimama kwa muda. Katika vurugu hizo, mtu mmoja aliyefahamika kama Jahaja Chandarua (27) alikufa baada ya kupigwa risasi na polisi sehemu ya paji la uso ambayo ilimpasua na kutokea upande wa pili, huku Mkuu wa Kituo cha Polisi Nyarugusu (OCS), Ibrahim akijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu ya mkono wake wa kulia na wananchi hao.

  Vurugu hizo ambazo zilianza juzi saa 2:00 usiku ziliendelea hadi jana jioni na kufanya shughuli za kijamii na kiuchumi katika kata hiyo na vijiji jirani na machimbo hayo, kusimama kwa muda huku polisi wakiendelea kutumia nguvu kudhibiti wananchi hao. Hiyo ni mara pili kwa wananchi hao kukosa uvumilivu na kuamua kuvamia machimbo hayo, kwani wiki moja iliyopita wananchi wengine zaidi ya 3,000 walivamia machimbo hayo kupinga kupewa mwekezaji huku wao wakishindwa kunufaika na rasilimali hizo za taifa.

  Chanzo cha wananchi kuvamia
  Tangu Serikali ilipofunga machimbo hayo, wananchi ambao walikuwa wakiyategemea kufanya shughuli zao za kiuchumi, wamekuwa wakiahidiwa kila mara kwamba, yangefunguliwa baada ya muda fulani, lakini imeshindwa kufanya hivyo.

  Kutokana na danadana hizo, ndipo juzi usiku wananchi hao walipoamua kukusanyika na kuandamana hadi kwenye machimbo hayo ya Nyaruyeye na kuanza kupambana na polisi wanaolinda eneo hilo.
  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nyarugusu, Thobias Ikangala alisema wachimbaji hao baada ya kufika eneo hilo walivunja uzio uliowekwa na mwekezaji kabla ya kutawanywa na polisi wanaolinda machimbo hayo na ndipo mapambano yalipoanza kati yao na polisi.


  Mwananchi
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  madini yetu yamekua laana kwetu
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wanasiasa wa Chama cha magamba wanaendelea na kazi ile ile ya kufanya ujambazi wa kisiasa mpaka kwenye machimbo na kuendelea kuwafanyia usanii wa siasa hadaa kila kukicha hadi wananchi wanakosa uvumilivu. Hadi lini tutaendelea hivyo?
   
 4. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hao wananchi hawana akili, kama madai yao yapo serikalini kwanini wavamie mgodi? Hii ndiiyo shida ya miafrika kuchukulia kwamba chanzo cha matatizo yetu ni wawekezaji. Mwekezaji naye ana kila haki ya kujilinda na nadhani kuna umuhimu wa kujenga ukuta ili kuepuka usumbufu wa aina hii.
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  mwita na candida, kwani serikali ikifanya maamuzi haraka na kuwa-organise wananchi kwa ajili ya kufanya uchimbaji ingekuwaje? na nyie mnaona suluhisho ni wawekezaji kwenye kila kitu?
   
 6. moblaze

  moblaze JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  I now doubt your citizenship...nyie ndio waamiaji haramu! umetoka Rwanda au Burundi bichwa tofa???
   
 7. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole yao Mungu atawasaidia na Siku nchi hii itapopata UHURU watafaidi Matunda ya nchi yao
   
 8. R

  RMA JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo mengine watanzania mnajitakia wenyewe! Hiyo serikali mnayoilalamikia inawasumbua na kuua raia si mliiweka madarakanni kwa kura zenu wenyewe? Tesekeni tu hadi mtakapopata akili!
   
 9. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mali tuliopewa na muumba inakua yakutuuwa
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Mbunge wao ni nani? Wa chama gani?

  Tuanzie hapo kwanza.
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Wakiwachiwa wavamie bila sheria nchi itakuwa haikaliki, kila ataetamani akionacho atataka kukivamia bila kufata sheria na kanuni zilizopo.

  Fitna moja kubwa katika dunia ni "mali".

  Kinachotakiwa ni Serikali kuwa makini katika kugawa sehemu za wachimbaji wakubwa na sehemu za wachimbaji wadogo, ambako kila mmoja atafata sheria na kanuni zilizo wazi. Na nna uhakika sheria na kanuni hizi zipo, kwa kuwa zipo, tatizo ni nini? Amma usimamizi usiotosha, amma kucheleweshwa kwa kutolewa vibali, hukumu na miongozo ya malalamiko kwa sehemu husika amma kuna kikundi cha watu kilichoandaliwa kuanza kuchochea hizi fujo,

  Hili la mwisho lina maana zaidi na kama kipo kitajulikana, watajulikana na watasulubiwa kwa mujibu wa sheria.
   
 12. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha kuona watu wanakufa lakini upande wa pili inafurahisha kuona watu wakitambua na kudai haki zao. Tutafika tu, kila mtu kwa nafasi yake.
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Kwenye movie ya SARAFINA walimkamata yule kibaraka wakampa kipigo halafu wakachoma moto, nadhani kuna mijitu humu ndani inastahili the same punishment! Haiwezekani tunaongea kitu halafu mpuuzi mmoja anahoji ujinga, laiti ungejua!
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Bibie kwanza niambie sheria ni nini na ni kwa ajili ya nani.
  Hawa ndugu zetu walikuwa wakichimba hapo bila bughdha kabla ya Mkapa kusema waondolewe kwa nguvu na apewe kaburu aka Sinclair aka Barrick. Kwa hapa sheria ni ubabe wa serikali inayotetea maslahi ya wazungu? Serikali inaposhindwa kulinda maslahi ya raia walioiweka mamlakani lazima umma ujichukulie sheria mkononi kwa sababu hakuna wa kuwalinda.
   
 15. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Angalia vizuri chanzo cha tatizo. Wananchi wananyang'anywa their source of income halafu anapewa mwekezaji, unategemea wafanye nini? This government is testing the patience of Tanzanians, and from the look of it, it's wearing thin. Wajue tu kuwa amani inaletwa na raia na sio majeshi.
   
 16. k

  king11 JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pole wananchi mnaonyanyaswa kwenye nchi yenu muda si mrefu mwanga mtauona....salamu za pole toka kwa lowassa

  tutapambana pamoja kuona mnanufaika na nchi yenu si kuwa wapagazi katika nchi yenu
   
 17. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  bora umetujuza wewe siyo mwenzetu, sasa sijui wa bara gani ASIA, AMERIAKA, ULAYA AU AUSTARALIA? Ndo maana huna uchungu na nchi yako. bora modes wakufutilie mbali, kwani hufikirii kuikomboa tz bali kuendelea kuiba na kupeleka huko kwenu.

  nakushauri uache kutumia jina la Kikurya, kwani sidhani kamawatani zangu wapo wenye mawazo kama wewe
   
 18. KIDESELA

  KIDESELA Senior Member

  #18
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Hawa watu wa geita na kanda ya ziwa mimi wala siwahurumii wacha wapigwe tu maana wao hawajajihurumia,make mkijua kanda ya ziwa ndio ngome ya ccm mara zte ushindi wa ccm unatoka kwao sasa hayo wanayopata ndio fadhila waliyoitaka,na bado
   
 19. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kuna maoni yanayotakiwa:- yale yasiyovunja katiba ya nchi na yasiyotakiwa yanayovunja katiba ya nchi. Wewe unavunja katiba ya nchi kwa kushawishi rasilimali za nchi zitumike si kwa manufaa ya uma bali ya wawekezaji unaowatetea.
  Pia huwezi kutumia uhuru wa maoni mfano kwa kutumia Katiba ya JMT, kutoa maoni serikali ipinduliwe, ubainike uone kitakachokupata. Kitakachokupata hakina tofauti na kuwekwa exile na modes
   
 20. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  I was just about to say the same....haraka haraka niliposoma ile post ya Mwita25 ikanijia ile scene ya kwenye Sarafina.....Sooooo disgusting these kinds of people...Thank God I don't know the real him!
  I don't condone violence....much as I hate the sight of desparate poor Tanzanians sufferings just because their land has got gold in it! What a shame!!!
   
Loading...