Geita: Makada 50 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wasimamishwa Uongozi kwa tuhuma za kuhujumu Chama kwenye Uchaguzi

Wasalaam!! Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Geita imewafukuza uachama makada 50 baada ya kuchangia kupungua kura za Rais Uchaguzi mkuu 2020. Hayo yamesemwa na bwana Masele ambaye alisema waliojitokeza kupiga kura ni 56,000 badala ya 100,000 jambo ambalo lilichangiwa na fitna za makada hao...
Wamewaonea tu,wangewauliza wale waliokuwa wanaingiza kura za kwenye mabegi, hizi kwenye mabox ilikuwa za kuzugia tu
 
Kuna vitu vinaendelea nchi hii mpaka sioni umuhimu wa shule aisee daaah!
Uwezo wetu wakufikiri na kutenda kati ya aliyesoma na asiyesoma ni bure kabisa.Alafu ukute anayejiita msomi alafu akawa ni mwanavhama wa hivi vyama vyetu vinavyojiita vikongwe yaani ni shida tupu.
 
Waambieni Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Geita, Uchaguzi Mkuu umeisha na Dr Magufuli ameshinda kwa zaidi ya 84% hivyo hakuna haja ya kufukuzana.

Kwani Bwashee hizo 84% za ushindi hazikutosha, mlitaka ashinde kwa 110%

Mitano tena 🤣🤣🤣🤣🤣
Naona walitaka hata Lissu ampigie kura Magufuli.
 
Ccm bhana. Kura za kwenye mabegi hazikuwatosha hadi muanze kufukuzana? Mshahara wa dhambi ni mauti. Muda si mrefu mtaanza kuuana kabisa.
Kura zakwenye mabegi si ilikua janjajanja yenu upinzani ilikuchafua taswira ya uchaguzi baada ya kugundua mtagaragazwa kipigo cha ubwa mwiziii?? Hiyo kiki mliitengeneza kishamba saanaa
 
Wasalaam!! Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Geita imewafukuza uachama makada 50 baada ya kuchangia kupungua kura za Rais Uchaguzi mkuu 2020. Hayo yamesemwa na bwana Masele ambaye alisema waliojitokeza kupiga kura ni 56,000 badala ya 100,000 jambo ambalo lilichangiwa na fitna za makada hao...
Bado tunaaminishwa kuwa CCM ilishinda kwa kishindo
 
Wasalaam!! Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Geita imewafukuza uachama makada 50 baada ya kuchangia kupungua kura za Rais Uchaguzi mkuu 2020. Hayo yamesemwa na bwana Masele ambaye alisema waliojitokeza kupiga kura ni 56,000 badala ya 100,000 jambo ambalo lilichangiwa na fitna za makada hao.

Habari zaidi soma Mwananchi online.

Nyoka wanatabia ya kula mijusi ila wakikosa mijusi wanakulana wao kwa wao. Usiku mwema
 
Adhabu za namna hiyo mara nyingi huwa zinatafsiriwa kama uonevu. Kwahiyo hao wanaweza jikuta wakajaa temper mwisho wa siku wakaanza kumwaga Siri za ushindi then Chama kikajikuta Uchi.

Vinginevyo wawe wamelishwa kiapo.
 
Hawana Siri yoyote uporaji wa matokeo ya uchaguzi hayakuwa Siri asilani,Tume na apparatus za usalama zilifanya yao bila aibu. hakuna taasisi yoyote itakayoamua hata wakitoa vilelezo ya video.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Shida hao wanaweza wakawa na ushahidi kabisa mwisho ikaleta taharuki ukizingatia watu wameshaanza kusahau Machungu ya Uchaguzi wenyewe.

Kwahiyo hawa wakijitokeza hadharani na kuanza kuongelea figisu za uchaguzi wakiwa na uthibitisho mkononi watakuwa wanatonesha vidonda
 
Back
Top Bottom