Geita: Kijana wa miaka 20 ahukumiwa kwenda jela maisha baada ya kumbaka binamu yake

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
1,223
2,000
Mkazi wa kijiji cha Katoro mkoani Geita, Jackob Thomas (20) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kumbaka mtoto wa miaka (8) ambaye ni binamu yake.

Hukumu hiyo ilisomwa na hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Chato, Erick Kagimbo baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu kagimbo amesema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa na Upande wa Jamhuri pamoja na maelezo ya kukiri kosa la mshtakiwa, mahakama hiyo imelazimika kutoa adhabu ya kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kutenda ukatili huo.

Awali muendesha mashtaka wa serikali Anosisye Erasto akishirikiana na mwendesha mashtaka wa Polisi Semeni Nzigo waliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo baada ya kumtembelea mjomba wake katika kijiji cha Nyarutu wilayani Chato.

”Baada ya kufikishwa kituo cha polisi mshtakiwa alihojiwa na kukiri kutenda kosa hilo ambapo alidai kwamba mtoto huyo ni mtu wa sita katika idadi ya wanawake aliowahi kuwabaka kwa nyakati tofauti” amesema Erasto

Hatahivyo Hukumu ya kifungo cha maisha ni ya tatu tangu kutolewa na mahakama hiyo katika kipindi cha miezi minne tangu kuanza kwa shughuli za mahakama mwaka 2020.
 

Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,054
2,000
Miaka 20 michache angepigwa 30 kama sheria inavyosema!! ameshindwa kwenda mtaani kukamata "swala" wa buku 2 au 3??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom