Geita inaongoza kuwa na madini lakini ina stendi mbovu

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
820
1,335
F19D833C-771A-47FC-84B7-3CDEBF6ECFA0.jpeg

Geita ndio mkoa unao ongoza kuwa na madini Tanzania.

Lakini pia ndio mkoa wenye Stendi mbaya sijawahi kuona.

Hiyo chini hapo ndio stendi ya mkoa wa Geita.

Wabunge wao kazi ni kugonga meza tu bungeni.

Madini yakwao lakini hayawanufaishi.
 
Yule jamaa nilipingana naye kwa mambo mengi sana, karibia 80% sikukubaliana naye!

Lakini katika jambo ambalo nashindwa kumkosoa ni kuchukua billion 700 (0.7 trillion) na kuziweka Busisi - Kigongo kwa ajili ya daraja.

Ni kweli mbali na hilo eneo kuwa kiunganishi muhimu kibiashara kwa nchi za DRC, Rwanda, Burundi, Uganda, South Sudan nk bado Geita kama Geita imetoa utajiri wake kwa miaka yote 60 jumlisha na ya wakoloni kuitajirisha hii nchi na wao wakabaki masikini.

Bora hilo daraja liwafariji ili ambao wangekimbilia kujibanza Mwanza wawekeze huko huko.
 
Ndiyo maana watu wanataka majimbo. Sehemu fulani (kiasi cha kutosha)ya mapato ya Geita yanatakiwa kubaki hapo kuijenga. Badala yake karibu pesa yote inaenda kujenga flyover Dar, lami hadi vichochoroni nk.
Katiba ya Mzee Warioba na Agustiono Ramadhani (Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema) iliweka bayana haya mambo yote ya kuokoa gharama kubwa za kuendesha nchi hadi mgawanyo mzuri wa madaraka na rasilimali asilia za nchi. Sema kiwango cha ujinga na unafiki hapa kimefikia levels za juu sana, Mungu atusamhe na tukachelewesha hili wazo la katiba. Wala hatuoni aibu kwenda kujifunza Rwanda!

Juzi juzi nilipita kwenye kamji kamoja, wamejenga jengo zuri sana, la kisasa na kubwa kwa ajili ya halmashauri. Kiukweli hilo eneo halina potential yoyote kiuchumi wala kisiasa ila (nadhani) walifanya hivyo kwa vile kuna mkubwa anatokea hapo wakati pana wilaya zinazochangia pakubwa kiuchumi ila ofisi zao ni za kusikitisha.
 
Nafikiri ujinga ndiyo shida kubwa. Na pengine wanaopigia debe majimbo au decentralization hawakuelimisha watu vya kutosha.
 
Ndiyo maana watu wanataka majimbo. Sehemu fulani (kiasi cha kutosha)ya mapato ya Geita yanatakiwa kubaki hapo kuijenga. Badala yake karibu pesa yote inaenda kujenga flyover Dar, lami hadi vichochoroni nk.
Uliza Halmashauri Geita hela za mrahaba wanazipeleka wapi
 
Uliza Halmashauri Geita hela za mrahaba wanazipeleka wapi
Na hapo ndipo chanzo cha tatizo na hili linazidisha uhitaji wa katiba ya wananchi.

Unajua kwa nini, kwa sheria za sasa (nipo tayari kusahihishwa) uwezo wa hizo local governments kusimamia mapato yao ni kama asilimia 10 tu. Wenye nguvu na sauti ya kusimamia pesa ni wateule wa kutoka juu. Hata madiwani hawawezi kuhoji, nadhani unakumbuka issue ya Msukuma na mkurugenzi bahati nzuri ilitokea maeneo hayo

Kwamba wananchi wa eneo wanahitaji nyumba ya walimu walau watano inayogharimu chini ya 50 million lakini kipaumbele kinakuwa ni gari V8 ya ofisa inayogharimu million 300!
 
Geita inaongozwa na watu waliojaa majungu na kutumika nawakubwa kupora hela za mgodi, jitahidini kujenga stend up ya eneo hilo ni kubwa sana na linatosha!
 
Msituchoshe mlichagua uwanja wa ndege Chato na mfugale tower yenu igeuzeni stendi maana ndege huko ng'ooo saii tunawanawisha mauwaziri nk.
 
Na miradi yao ya kimkakati yote imetelekezwa na awamu ya 6.

Safari lazima kinuke
Nasita kukwambia kuwa umesema uongo, badala yake kwa ustaarabu nasema hiyo siyo kweli! Miradi yote ya kimkakati inatekelezwa yote au itatekelezwa yote (kwani utekelezaji ni ON GOING PROCESS!) na hii awamu ya Rais SSH! Au nijuze ni miradi ipi ya kimkakati ambayo imetekelezwa na awamu hii ya sita?
 
Waliiharibu ni wale walipeleka chuo Cha madini Moshi wakati hakuna madini.
Ni ujinga wa hali ya juu,kuweka chuo mbali na eneo la field yenyewe !! Uchimbaji uko kwingine ,chuo kwingine.location imekaa hovyo Sana hii!!,Kilimanjaro wawekage vyuo vya utalii na wanyama pori ok kabisa ,na sio madini !!
 
Ni ujinga wa hali ya juu,kuweka chuo mbali na eneo la field yenyewe !! Uchimbaji uko kwingine ,chuo kwingine.location imekaa hovyo Sana hii!!,Kilimanjaro wawekage vyuo vya utalii na wanyama pori ok kabisa ,na sio madini
Wanafunzi wanaotoka maeneo ya migodi kupelekwa kusoma moshi mambo ya uchimbaji madini ulikuwa wamuzi wa kipumbavu sana! Wakati vyuo kama Mwanza veta ipo ulikuwa ujinga sana!
 
Back
Top Bottom