Geita Gold Mine kuchangia Tshs 22mil kuwaondoa wananchi eneo la hifadhi ya misitu ni sawa?

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,881
1,124
mimi nachanganyikiwa kidogo naombeni msaada,sikubaliani na wananchi kuvamia eneo la misitu lakini kwa kuwa hiyo ni kazi ya serikali.
ggm inadaiwa na wananchi fidia haijalipa na imechakachua makadirio,sasa kwa serikali kuchukua hela za ggm na kuzitumia kulipia polisi na kununulia viberiti kuchomea wananci nyumba zao walizojenga zaidi ya miaka 20 si sawa.
chadema wakipeleka m4c huko mtadai wachochezi?
naombeni kina ritz,rejao na wengine wa ccm mtuambie hiyo ni sawa?
 
si sawa kwa kweli. Wasukuma wa Geita nao ni makondoo tu. madini yao lakini wanateswa utadhani ni wakimbizi, tangu madini yaanze kuchimbwa hapo kuna faida gani za msingi wananchi wa Geita walizopata zaidi ya kupigwa na vumbi?
 
nashangaa bwana shomari na cha ajabu wale wananchi wameishi pale zaidi ya miaka 20.
na mbaya zaidi kwa kuchoma nyumba moto wameonyesha ukatili wa hali ya juu.
 
Wameondolewa kwa kuchoma nyumba moto ILI WAZUNGU waweze kuchimba dhahabu,imeniuma sana!
Hao watu wa haki za binadam wako wapi?
 
lile eneo litakuwa na MADINI Make hwa wazungu hawawezi poteza pesa zao bure kisa kulinda mazingira, mbona wao ndo wanaongoza kwa kuhalibu mazingira
 
Wazungu wameshaona deposit ya dhahabu hapo very soon tutaachiwa mahandaki hapo na madhara ya kemikali watu waanze kuchubuka
 
Hapo kuna dhahabu GGM wanataka kuanzisha pit nyingine wametumia mgongo wa serikali dhaifu ili kukwepa kuja kuwalipa wananchi fidia
 
JONAS,MARIRE,CHASE,BASHADA NAMSOLOPAGAZI.
mmeona jinsi serikali yetu ilivyo na matatizo,watu wakilalamika wanasema kuna wachochezi.
vitabu vitakatifu vinasema rushwa inapofusha macho,hawa ccm hawaoni tena hata kunusa pua imeshakufa ganzi.
hawawezi kuona hata kama zoezi ni halali kufadhiliwa na ggm ambayo ina migogoro kibao na wananchi hawataeleweka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom