Geita (gold exploration in Tanzania) hazina iliyofichika. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Geita (gold exploration in Tanzania) hazina iliyofichika.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Taifa_Kwanza, Jul 18, 2011.

 1. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Miaka kama kumi na moja iliyopita, nilikutana na jamaa fulani maeneo ya Mwanza
  kwenye counter ya Bar moja tukipata moja moto moja baridi.

  Ghafla, tulizoena na kuanza kuongea mambo meeeengi sana, Mojawapo ni experience
  yake ya kufanya Kazi kwenye Mgodi wa Geita Gold Mining akiwa ni mmoja kati ya watanzania
  wa kwanza kabisa kuajiriwa katika Mgodi huo.

  Yeye aliajiriwa kama Driver, elimu yake ikiwa ni form four, aliniambia alikuwa ni mmoja wa watanzania
  wa kwanza kabisa kuendesha mamitambo ya kuchimba ardhi kuzamia Dhahabu chini ya Ardhi.

  Katika mengi aliyonieleza leo naomba kupata uhakika wa hili kwa wenye details husika, Kwamba,
  mji wa Geita maana yake ni Gold Exploration in Tanzania, Ulipewa jina hili na watafiti wa madini wa
  Kizungu miaka mingi iliyopita kama sio nyakati za vita vya kwanza vya dunia.

  Alinieleza kwamba, habari hizi alipewa na Kijana wa kizuru ambaye ndio alikuwa trainer wao
  kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, na kwamba hiyo ilikuwa ni siri kubwa sana miongoni
  mwa jamii za kizungu, Kwamba ufahamu aliokuwa nao ni kwamba, Geita ni eneo lenye utajiri
  wa Dhahabu kuliko eneo lolote lile duniani, na kwamba eneo hilo liko Marekani na wamarekani
  hawakuwa tayari kuchimba dhahabu hiyo mpaka pale dhahabu itakapopongua maeneo
  mengine duniani hasa South Africa, Ghana n.k, kwamba hakuwahi kufikiria geita
  inaweza kuwa sehemu yoyote katika Ardhi ya Africa kutokana na msimamo ambao uliishapitishwa
  wa kutochimba dhahabu eneo hilo.

  Mzuru huyo, kwa namna iliyokuwa ikiashiria kwamba anatoa siri kubwa sana moyoni, mwake
  alimueleza rafiki yule kwamba, yeye Binafsi machozi yalimtoka alipokuja kukuta kwamba Geita
  ni sehemu ya ardhi ya Africa, tena Wakazi wa eneo hilo wakionyesha kwamba hawakuwahi
  kujua kabisa kwamba chini ya ardhi hiyo kulikuwa na ADHINA ILIYOFICHIKA KWA MIAKA
  MINGI SANA KWENYE MIOYO YA WAZUNGU.

  Ninaandika maelezo haya, huku roho ikiniuma sana, Hasa nikikumbuka majuzi John Mnyika
  aliuliza bungeni kama Madini yenu yana laana.

  Mwenye taarifa zaidi naomba anisaidie. Ninakusanya hasira.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Adhina? ni nini?
  In 19th Century or during WWI kulikuwa hakuna nchi inayoitwa Tanzania
   
 3. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hata ukiwa na hasira zaidi ya watu wa nyamongo wanaopigwa risasi na kuambiwa ni majambazi haisaidii.nchi hii ni tajili sana ila kumbuka usemi huu nakama unauamini utakupoza 'penye miti mingi hapana wajenzi'.pole ndugu.
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  pole sana mapujds hali hiyo naona sasa ndo inaenda ukingoni so keep on waiting for a bit change is coming..
   
 5. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Unachosema ni kweli, mji wa Geita wote umejengwa juu ya dhahabu. Lilishawahi kutolewa pendekezo kwamba mji wa Geita uhamishwe, lakini tatizo ni kwamba wapi pa kuuhamishia, na pia fidia kubwa sana inayohitajika kulipwa kuwahamisha watu.
   
 6. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Noted: Hii inaweza kuwa moja ya fact kwamba the story is faked.
   
 7. M

  MantaLine Member

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Geita has been associated with minerals particularly gold long time ago

   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Ulipokosea ni pale tu ulipoweka Tanzania badala ya Tanganyika, it makes sense or mere coincidence!
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wabongo bana hii tabia ya conspiracy theories sijui itaisha lini? Anyways asili ya jina Geita ni geti lililokuwepo hapo enzi za mkoloni katika barabara ya Biharamulo-Mwanza, geti lilikuwa likiitwa Get A ambayo kwa ndugu zangu wasukuma wakawa wanaitamka Geeeta. Sasa huyo aliyekuambia kwamba sijui ni Gold Exploration Tanzania simply alikudanganya. Sehemu ambayo kuna proven gold reserve nyingi na ndiyo panapochimbwa kwa sasa ni Nyankanga. Sasa hiyo ya Geita mjini sijui exploration ilifanyika lini na nani? Ikumbukwe pia wakati makampuni kama Samax na Sutton resources yalipokuwa yanafanya explorations miaka ile ya tisini geita town ilikuwa na population ya watu kama 2000 tu, na hicho unachosema kama kingekuwa kweli mji ungehamishwa tu. Ila so far hiyo ni habari ya kijiweni na inaishushia hadhi JF

  Yaani huu ni uongo ambao tulikuwa tunaelezwa enzi za kikomunist mara ooh Tanzania inaongoza duniani kwa upelelezi, mara pale Dar Airport kuna madini ya kumwaga, mwanza airport pia. Nashangaa to this date tunasema tuko kwenye information age lakini bado uongo uongo kama huu unakuwa entertained. Yaani Geita ina dhahabu kuliko South Africa, kuliko Kalgoorlie, Mali???????????? Duh!!! cry my beloved country. And just for a fact and your information nilikuwepo Geita toka mwaka 1992 mpaka 2001. Hakujawahi kuwa na trainer wala mfanyakazi mzulu. There was only a zulu guy with Stanley Drilling company and he was just a driller not a trainer. Na such info is usually not understood or known by drillers but geologists. Let's move on....
   
Loading...