GEITA: Diwani asiyejua kusoma wala kuandika asimamishwa baada ya kutohudhuria vikao tangu Disemba

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,495
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita limemsimamisha Diwani wa Kata ya Senga Joel Ntinginya kutoendelea na nafasi yake baada ya kutohudhulia vikao vya baraza tangu kuapishwa kwake Disemba mwaka jana.



Diwani huyo amekuwa akituhumiwa kutokujua kusoma wala kuandika.

Baada ya kupoteza sifa ya kuendelea kuwa Diwani wa Kata ya Senga, mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita amesema tayari ameshapeleka barua TAMISEMI kwa ajili ya hatua zaidi.
 
Yamekuwa hayo tena, km sheria inaruhusu basi mwenyekiti yuko vizuri kuendelea na hatua nyingne stahiki, hata hivyo vijana wasomi wako wengi sana apishe tu akaendelee na Shule ajue kusoma na kuandika walau.
 
Diwani asiyejua kusoma wala kuandika huko Geita Joel Ntinginya amesimamishwa kazi, diwani huyo hajahudhuria vikao vya madiwani mara tatu mfululizo bila idhini
Diwani huyo aliripotiwa na madiwani wenzake kwani hata fomu zake hakujaza
 
Kwa sababu mteja ni mfalme basi kuna haja ya kuangalia upya mahitaji ya mlaji na sio mahitaji ya muuzaji
 
Duuuh only in black continent....

Huyu ndiye anategemewa kupitisha budget ya wilaya au kumuwajibisha mkurugenzi Kwa ufisadi...
 
Diwani asiyejua kusoma wala kuandika huko Geita Joel Ntinginya amesimamishwa kazi, diwani huyo hajahudhuria vikao vya madiwani mara tatu mfululizo bila idhini
Diwani huyo aliripotiwa na madiwani wenzake kwani hata fomu zake hakujaza


Diwani huyo ndio huyu au mwingine?

Duuuuh. Huyu diwani ni balaa.
 
Back
Top Bottom