Geita, Chato: Mwili wa Monica Magufuli, wazikwa katika Makaburi ya familia

Mama aliolewa na mumewe yupo hai na watoto wapo pamoja na wajukuu zake lakini amezikwa kwa kaka yake kwa nini.?

Labda sijui mila za wasukuma.!
Hapa Wasukuma wote humu ndani watapita kama vile hawaoni hivyo naomba na mimi niulize tena...je ni kawaida kwa mama aliyeolewa kuzikwa kwa kaka yake wakati mumewe na watoto wapo? Je mumewe akifariki atazikwa wapi? Je mila za Kisukuma ndivyo zinavyotaka?

Najua kwa Wakristo, wawili wakioana (wakifunga ndoa) wanakuwa mwili moja, na binti huwa anaagwa kabisa na familia yake na kuungana na familia ya mumewe, je kwa Wasukuma hali ikoje. Naomba nielekweke kwamba katika kuuliza sina nia mbaya ila naomba tu kupewa elimu.
 
Naomba kujua, hivi huyu mama(Dada yake Magufuli) ndiye mama yake na Katibu wa Wizaraya Mipango na Fedha Bw. Doto James pia ndiye mama yake na Mwenyekiti wa UVCCM taifa Bw. Kheri James?

Nataka nijue maana nilisikia kuwa hawa ni wapwa wake na JPM na kama huyu ndiye mama yao au la!!
 
Labda kifohiki kitamzindua Jiwe ajue kuna kufa vyote hivi akaviacha. Hivyo akapunguza dhulma.
Pambana na hali yako wewe mwenyewe utakufa usipende sana kuhesabu mabaya ya wenzio na kujiona wewe ni mwema la hasha wote ni wakosefu mbele za mwenye enzi kuu na tutahukumiwa sawa na matendo yetu wewe tenda wema tu
 
Hapa hatuoni mume au watoto au WAJUKUU ni vipi? AU kuna shida gani? Mume au mke na watoto huwa wanakuwa na heshima ya pekee wakati wa kuzikana.
 
Hiyo lazima mzee hadi mzee anastaafu ni protocol tuu zipo wanamuacha mda wa kulala tuu ndo maana hata anapokua Ofisini kwake pale ikulu unakuta kolido zote wamezikamata

Urais mtamu ndo maana Lowassa anapambana ili aupate na Mda umeshamuishia hivyo ardhi inamuita.
una maneno wewe.
 
Sasa hao maafisa usalama wanafuata nini? Hata kwenye msiba, tena nyumbani kwa mkuu mwenyewe wao wammganda mkuu utafikiri kumbi kumbi!
Kuna vitu vinashangaza kweli kweli, Huu ulinzi ni wa miaka ya nyuma, leo unaona Trump kama hana ulinzi kumbe hatari ata panya hasogei mambo ya kumkamata kama luba mkuu wetu wa dola sio poa mpaka watu waanze kuulizana Rais ndo Yupi pale.
 
Sawa, lakini kama mwanamke kaolewa huwa ikitokea kafariki anazikwa kwenye ardhi ya mumewe/kwao mumewe, iweje huyu ambaye ana mme watoto na wajukuu azikwe kwao
Sio lazima iwe ivo mkuu, Apo ni wanafamilia wamekaa na Kuamua ivo wewe ni nani mpaka utake kuwapangia itoshe kujua kuwa hayo ni maamuzi binafsi ya familia yao.
 
Back
Top Bottom