Geita Buseresere: Usafiri unaotumika kusafirisha abiria ni hatarishi!

Lugano5

R I P
Jul 15, 2010
4,520
755
1.jpg

Gari Aina ya Pro Box ikiwa tayari kusafirisha abiria

Wakazi wa mkoa wa Geita maeneo ya Buseresere na Katoro, wapo katika hatari kubwa ya maisha yao kutokana na usafiri wanaoutumia kutoka eneo moja kwenda jingine.

Mwakilishi wa kikundi cha Usalama Barabarani, Fungo Agustus, ametutumia tukio hili ambalo ni hatari kwa abiria mkoani Geita.

Gari ndogo aina ya Pro Box zimeingia kwa wingi mkoani Geita na kutumika kubebea abiria katika mazingira ambayo si salama na ni hatarishi kwa abiria hao.

Abiria wamekuwa wakipakiwa kwenye mabuti ya kuwekea mizigo tena kwa msongamano mkubwa.

Zifuatazo chini ni picha za kinachoendelea kwenye usafirishaji eneo la Buseresere.

236.jpg

Abiria wakiwa wamekusanywa kwenye buti eneo la kubebea mizigo huku wakiwa sambamba na watoto wadogo

3.jpg


4.jpg

Aina nyingine ya Gari ndogo inayotumika kubebea abiria.

5.jpg

Mizigo na Watoto wakiwa wamekusanywa pamoja na mizigo nyuma ya Gari hiyo.

6.jpg

 
Serikali iko wapi?Mbona hii ni hatari sana?Ukizingatia pia gari liko wazi na vumbi lile hata kiafya ni deadly
 
Hiyo kitu common sehemu nyingi Bongo mkuu.... Hata pale Morogoro, Stendi ya Dodoma, magari yaendayo Dumira dakawa ni mtindo huo.
 
Huyo mwakilishi wa usalama barabarani amechukua hatua gani?! Kazi yake ni kuhakikisha usalama barabarani, afanye kazi yake.
 
Pia niiiona barabara ya kutoka mafinga iringa kuingia mfindi huko, na mbele kidogo yanapoita haya magari kuna traffic kuanzia saa 12 asbh hadi saa 12 jion...magari yote yanapita yamebeba kwenye buti abiria....dereva akifika pale anapak anapeleka posho, anaendelea......yupi rais wa kubadili haya??
 
umaskini na ujinga bado ni tatizo hapa tz,,mtu anakaa huko kwa buti af unaeza kuta analipa nauli ile ile
 
Back
Top Bottom