Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,143
2,000
Baraza la Madiwani Geita limeukataa Mkoa wa Chato. Je, Hayati Magufuli angekuepo wangeweza kukataa hiki kitu. CCM wakikusifia au wakikubaliana na wewe ujue wana maslahi au ni Unafiki tu.

Wanajitahidi kufuta Legacy ya Shujaa wetu. Sio sahihi Hata kidogo.

=======

Baraza Maalum la Madiwani Halmashauri ya Wilani Geita Mkoa wa Geita wamepinga wilaya mpya ya Busanda pamoja na hifadi ya Taidfa ya Kisiwa cha Rubondo kuchukuliwa na mkoa mpya wa Chato unaotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni wakidai kuwa itasababisha wananchi kusafiri umbali wa kilomita 200 kwenda kutafuta huduma na na kusababisha mkoa wa Geita kukosa sifa kiutawala.

"Tunaenda kupata huduma hii Chato -- kilomita zaidi ya 200. Sasa, ni namna gani tunazidi kuwaongezea wananchi wetu mzigo wakati wakihitaji huduma. Mimi naona mapendekezo haya yaheshimiwe..." Bw. Salehe Juma, Diwani wa Kata ya Nyarugusu

Kisiwa cha Rubondo wakiache katika mkoa wa Geita kwasababu mkoa mpya ambao unaenda kuundwa, mkoa wa Chato, ukiangalia Ngara kuna misitu

Mkuu wa wilaya ya Geita Fadhili Juma amaesema amepeleka mapendekezo Serikalini ya kukataa mpango huo wa kuchukua maeneo ya wilaya hiyo kwenda Chato kwakuwa yatasababisha athari kwa wananchi.

"Maazimio ambayo natoka nayo hapa na muhtasari, topo ridhaa kuacha kisiwa cha Rubondo lakini hatutakubali. Bora mkoa usipatikane kuliko wilaya ya Busanda kuingia kwenye mkoa mpya. Tuliwapa sababu zote kwamba ukitoa wilaya ya Busanda kwenye mkoa wa Geita maana yake mkoa wa Geita unakosa sifa za kuwa mkoa."

Zaidi soma; Geita yakubali kuundwa Mkoa wa Chato; Kakonko, Biharamulo na Ngara kumegwa. Sengerema kwenda Geita..

 

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,953
2,000
Kuweka kila kitu Chato, si jambo lililomfurahisha kila mwenye akili, wakiwemo hao madiwani.

Kuna wakati unajiuliza juu ya uwezo wa marehemu katika kufikiri na kufanya maamuzi, unashindwa kuelewa kama alikuwa sawa wakati wote maana kuna mambo ambayo hata average brain, hawezi kufanya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom