Geita: Auawa akidaiwa kujaribu kumbaka mwanafunzi

Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 18 hadi 22 ameuawa na mwili wake kuchomwa moto na wananchi wakidai kuwa alijaribu kutaka kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili katika Sekondari iliyopo Kata ya Bombambili mjini Geita.

Tukio hilo limetokea leo Alhamisi Februari 24, 2022 saa 12.30 asubuhi wakati mwanafunzi huyo akiwa njiani kwenda shule.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa mwanafunzi huyo alitoka nyumbani alfajiri kuwahi shuleni na akiwa njiani ndipo alipokamatwa na kijana huyo akimvutia kichakani kwa lengo la kumbaka.

“Alipomkamata mwanafunzi alipiga kelele na wananchi walikusanyika na kumzingira. Walianza kumuokoa mwanafunzi na kumpeleka shule kisha kumshambulia kijana huyo hadi kumuua na mwili wake kuchomwa moto,” amesema Kamanda Mwaibambe.

Kufuatia tukio hilo, Mwenyekiti wa mtaa huo Salum Maige anashikiliwa na Polisi kusaidia kufahamika kwa wote waliohusika kwenye mauji hayo.

“Marehemu alishazingirwa hatuoni sababu za kumuua zaidi ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria. Kwa kuwa mauaji yamefanywa na wananchi wa eneo hilo tunamshikilia mwenyekiti ili asaidie polisi kuwapata wahusika,” ameongeza.

Chanzo: MWANANCHI
 
Sasa kati ya wewe uliyeua na huyu aliyetaka kubaka, wapi ilipo dhambi kuu!! Huu ni utoto tu na huwenda walikubaliana kiutoto na wakakubaliana kuamka mapema
 
Kaka yangu ni mlemavu wa akili (down's syndrome) jumapili alichomwa moto akiwa mzima hadi kufa walidhani ni mwizi ukimuangalia vizuri unamjua kabisa huyu ni tahaira.
Lakini cha ajabu waliofanya tukio ilo wameachiwa huru wapo uraiani licha ya kuwepo ushaidi wa video
Pole sana kwa kuondokewa na Kaka yako, hapo hilo suala lifikishe juu zaidi kwa waziri na IGP na humu humu jukwaani endelea kulisema hili naamini litafanyiwa kazi.
 
Na huyo mwanafunzi akamatwe asije kua alikula hela ya nauli.



Ova..
 
Hawa polisi wetu liniwataanza kutumia akili na sio mabavu kwenye utendaji wao?why wamshikilie Chairman kama hawajamlink na crime scene?tuelewe Kuna Ile sheria ya kumshikilia suspect only for 48hrs na baada ya hapo ni mahakamani au aachiwe, police walitakiwa ndio wapeleleze na sio kumtwisha mzigo huu chairman.Nikiupata urais wa 24 hrs wizara hii nitaiweka Sawa within 4hrs ikiwa ni pamoja na kuivunja na kutengeneza wizara mbili,police na home affairs, na uajiri mpya kwa all homicide detectives na training zao ndani ya Botswana na equipments zote from US.
Kuna uwezekano Mwenyekiti ili kujinusulu anaweza akataja watu ambao hawakuwepo au akataja ambao alikua na ugomvi nao.. Hawa polisi wetu wa hovyo kweli kweli
 
Back
Top Bottom