Gazeti Ujerumani laandika ukiukwaji wa "demokrasia" na "Uhuru wa habari" ktk Serikali awamu ya Tano

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
image.jpeg
image.jpeg
"Khofu dhidi ya uhuru wa kujieleza" ndivyo kisemavyo kichwa cha habari cha makala hii ya Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle, Andrea Schmidt, ambayo imechapishwa kwenye jarida la [HASHTAG]#Weltzeit[/HASHTAG] na ambalo safari hii maudhui yake makubwa ni uhuru wa vyombo vya habari chini ya kaulimbiu "Make the Media Great Again".

Kwa tafsiri isiyo rasmi, anaandika kwenye utangulizi: Maendeleo ya kidemokrasia nchini Tanzania yamerejea nyuma katika maeneo mengi: kuna zuio dhidi ya mikutano, maandamano, matangazo ya moja kwa moja kupitia vikao vya bunge na kuna hatua nyengine kali dhidi ya upinzani."

Sehemu ya chini ni maelezo mafupi ya mwandishi wa habari Salma Said juu ya namna anavyokabiliana na ugumu wa ufanyaji wa kazi zake, likiwemo tukio la Machi 2016 alipotekwa na "watu wasiojuilikana".

Hisani ya M.Ghassani
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,562
2,000
Alafu hapa ndani ya nchi magazeti yetu hii habari hawaipi uzito wa kwanza.

Nawapongeza gazeti la The citizen kuifanya hii habari kuwa ndio leading story katika toleo lao la siku ya leo.
Kuna sekta mbili zinazoongoza kwa woga Tanzania, ualimu na sekta ya habari.

Kwa sasa ukiongeza sheria mpya iliyosainiwa juzi waandishi wa habari wanaweza kuwapiku walimu kwa woga.
 
twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,060
2,000
Alafu hapa ndani ya nchi magazeti yetu hii habari hawaipi uzito wa kwanza.

Nawapongeza gazeti la The citizen kuifanya hii habari kuwa ndio leading story katika toleo lao la siku ya leo.
Wataiitaje nzito wakati ni nyepesi...wao ndio wako nchini wanaujua ukweli...hao maadui wa nje ndio unawalinganisha na magazeti yetu ya hapa nyumbani...nyie hasara kweli
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,619
2,000
Absurd!...hawa wajerumani waliokuwa wanalia kudukuliwa kwa simu za Chancellor Angela? mbona hawakufurahia CIA kuwa walikuwa na nia ya demokrasia? uwazi?.
 
mahutu

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
766
1,000
Kwenye kuelekea mafanikio lazima punda aumie ili mzigo ufike...so nahapa tz ili kufika kwenye mafanikio lazima watu waumie laaa sivyo ni njogi tuu
 
kandukamo1

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
1,059
2,000
Kuna sekta mbili zinazoongoza kwa woga Tanzania, ualimu na sekta ya habari.

Kwa sasa ukiongeza sheria mpya iliyosainiwa juzi waandishi wa habari wanaweza kuwapiku walimu kwa woga.
Daah......Mkuu hapo kwenye ualimu kisu chako kimegota kwenye mfupa wangu wa ugoko. Kwa namna moja au nyingine upo sahihi cz walimu tu watu duni sana kwa kipato. Hali hiyo inapelekea wengi wetu kuwa duni kifikra.

Seriously, nikikumbuka tukio moja niliwahi peke yangu kutosimama kumsalimia mkuu wa wilaya ambaye alituweka toka asubuhi akaja jioni, watu hatujala twamsubiri yeye tu. Sitosahau nilivyonangwa na wenzangu, kutishiwa kuoteshwa nyasi kibarua. Lile jambo lilinifanya niwahurumie sana walimu.
 
Kobe

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
1,791

Pole sana kiongozi nimeona hilo hata jamaa zangu ambao nilisoma nao kwa sasa ni walimu huwa nawashangaa namna walivyo tukikutana kupiga stori mbili tatu yaani wamejiweka kwenye tabaka la uwoga kutojiamini kabisa, kwa hii hali mpk najiuliza wanafundishaje huko darasani ili kuwapa confidence watoto wetu? Mfuko huh ukiendelea mbele zaidi tutaja kuwa taifa za lenye watu mithili ya uze..ta.
 
Kibo255

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
4,408
2,000
[HASHTAG]#freemaxencemelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TunamtakaBenAkiwaHai[/HASHTAG]
[HASHTAG]#JusticeForLema[/HASHTAG]
[HASHTAG]#usirudiekosa2020[/HASHTAG]
 
Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,492
2,000
Alafu hapa ndani ya nchi magazeti yetu hii habari hawaipi uzito wa kwanza.

Nawapongeza gazeti la The citizen kuifanya hii habari kuwa ndio leading story katika toleo lao la siku ya leo.
kuna paralysis kubwa sana ...wewe hujui tu
 
Rich Pol

JF-Expert Member
Oct 11, 2013
7,836
2,000
Wakaandike kwanza ya Uganda na Rwanda, watuache na nchi yetu bado tunatumbua majipu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom