Gazeti Raia Mwema na tuhuma zake kwa CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WanaJF leo niko mbali sana ya mji lakini kuna jamaa yangu kaniambia kama kawaida tena leo gazeti la RAIA MWEMA lilikuwa na habari isiyopendeza inayohusu kinachoitwa mgawanyiko ndani ya chadema kuhusu uchaguzi Igunga.

Na nimeelezwa kama kawaida yao wameiweka kwenye Habari kuu Front page.

Aliyesoma tafadhali atuthibitishie na kutueleza kilichoandikwa.
 
Kwahiyo na wewe ni kama ccm unataka kila siku cdm ipambwe hata kama inakosea! Jamani msipokuwa makini mtakuwa kama ccm na mtaanza kuandama magazeti kwa mbinu zile zile za ccm!

Kanusha habari iliyoandikwa si kulalamika kuwekwa front page!
 
Acha Mwazo mgando, cdm wasifiwe tuu kwani hawakosei?
Unazidi kuthibitisha kuwa wakiingia madarakani watafuata nyayo zilezile za magamba.
Acheni ushabiki wa kibubusa, mpongeze yoyote anapostahili hatakama ni adui yako
na mkosoe yoyote panapo stahili hatakama ni mpenzi wako.
Jibu Hoja kwa Hoja sio Kulalama.
 
ni ukweli na uwazi tu CDM nao sio miungu wakikosea wanakosolewa tu kani wao ni kina naaaaaani???
 
Duh, Cdm Walishaona Kama Ni Kichaka Cha Kujificha Kama Leo Wameachwa wazi Ni Nafasi yao Kujirekebisha.
 
Magazeti mliyokuwa mnayanukuu hapa kila kukicha yalikuwa Raia Mwema,Mwanahalisi na Mwananchi sasa wiki mbili tu mumekosolewa tayari mtasema yamenunuliwa.
 
Magazeti mliyokuwa mnayanukuu hapa kila kukicha yalikuwa Raia Mwema,Mwanahalisi na Mwananchi sasa wiki mbili tu mumekosolewa tayari mtasema yamenunuliwa.

Chadema kukosolewa na magazeti ama watu binafsi sio jambo la ajabu. Kwani raia mwema wameandika habari gani dhidi ya chadema?

Manake naona mashambulizi tu dhidi ya chadema bila habari yenyewe, tupeni summary ya habari hiyo, wengine hatukufanikiwa kulisoma.
 
jamani, jamani acheni majungu RAIA MWEMA is one among of the best News papers in Tanaznia
Sio kidogo tu wakiandika habari inayoonekana iko CONTRARY na cdm basi ndo wamenunuliwa.
Wahenga walisema Mgema ukimsifia sn tembo hutia maji
 
kukosolewa ni lazima ili demokrasia iweze kukua nchini tanzania,kama chadema wamesemwa au hawajasemwa na wao hawajajibu kitu chochote basi wanafanyia kazi mawazo ya wahariri ambao wanaheshimu mchango wao kwa hali na mali mfano said kubenea
 
WanaJF leo niko mbali sana ya mji lakini kuna jamaa yangu kaniambia kama kawaida tena leo gazeti la RAIA MWEMA lilikuwa na habari isiyopendeza inayohusu kinachoitwa mgawanyiko ndani ya chadema kuhusu uchaguzi Igunga.

Na nimeelezwa kama kawaida yao wameiweka kwenye Habari kuu Front page.

Aliyesoma tafadhali atuthibitishie na kutueleza kilichoandikwa.
Kukosolewa ni kitu kizuri sana. Sioni ubaya wowote kwa Raia Mwema kuikosoa Chadema
 
WanaJF leo niko mbali sana ya mji lakini kuna jamaa yangu kaniambia kama kawaida tena leo gazeti la RAIA MWEMA lilikuwa na habari isiyopendeza inayohusu kinachoitwa mgawanyiko ndani ya chadema kuhusu uchaguzi Igunga.

Na nimeelezwa kama kawaida yao wameiweka kwenye Habari kuu Front page.

Aliyesoma tafadhali atuthibitishie na kutueleza kilichoandikwa.

Leo gazeti lenu wenyewe limewageuka, hapo ujue huko sio kwenyewe, hamia hamia hamia CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom