Gazeti RAI lailipua CCM kuhusu njama dhidi ya CHADEMA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti RAI lailipua CCM kuhusu njama dhidi ya CHADEMA.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, May 24, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Gazeti la RAI linalomilikiwa na Habari Cooperation limefichua njama kubwa zilizoandaliwa na Chama cha Mapinduzi dhidi ya Chama kikuu cha upinzani Tanzania CDM.Gazeti hilo toleo la leo alhamisi limedai mkakati huo kabambe uliosukwa kwa muda mrefu na kwa ustadi mkubwa tayari umeiva na hatua ya kwanza imeanza kwa kuwatumia baadhi ya makada walioko ndani ya CDM ambao ni mbunge wa Maswa Mashariki John Shibuda na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CDM-BAVICHA Bi Juliana Shonza.Gazeti hilo limezidi kudai kwamba mkakati wa CCM ni kuhakikisha inawatumia makada hao kuisambaratisha CDM.
   
 2. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ni ukweli ulio wazi hata kipofu bila kuona anaamini ni mbinu chafu za matumizi ya hela na madaraka kuuwa upinzani
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Tulianza na MUNGU tutamaliza na kifo cha Ccm
   
 4. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tafadhali leta habari kamili.weka hilò gazet hapa.
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ku-deal na Shibuda ni rahisi sana, viongozi wa CHADEMA hawatakiwi kuumiza kichwa. Dawa yake ni kum-ignore.

  Viongozi wa CHADEMA wakianza kujibizana na Shibuda atawatoa kwenye hoja za msingi na hivyo kupoteza focus ya 2015.

  Hizo ndio gharama za zoa zoa, maana wakati mwingine unaweza kuzoa hata nyoka ukidhani umenasa samaki!
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  ccm

  Kuzaliwa 1977

  Kufa 2015
   
 7. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Ukifanya kosa nyumbani ukaona mzazi amekaa kimya si kwamba amedharau ila anatafakari, huwezi kupata jibu bila kujua tatizo na utatuzi wake nini, je umewahi kusikia viongozi wa chama wakitolea neno kuhusu shibuda au juliana? Ukiona kobe kainamisha kichwa ...........
   
 8. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,847
  Trophy Points: 280
  nawakubali sana chadema..wametulia kama hawapo vile..ila mwisho wa siku kitaeleweka tuu
   
 9. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Namuunga mkono Keil. Shibuda ni kum-ignore halafu cdm isonge mbele kufungua matawi hasa vijijini.
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  CDM ni chama kubwa viongozi wake hawana papara Sio kama NCCR manunuzi au TLP au CUF vilivyosambaratika kama Uyonga
   
 11. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kama madiwani wa Arusha walishindwa hao hawatupi presha
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Anayeweza kuscan aliweke hapa jamvini.Kwa sababu nimeandika tu kwa kifupi na website yao bado hawajaingiza.Ukisoma habari yote hakika inatisha na ni aibu kubwa kwa demokrasia yetu changa
   
 13. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM inadhihirisha ni kiasi gani imezeeka na kwamba inashindwa ku-focus kwenye mambo ya msingi yanayolikabili taifa kwa sasa na kupeleka nguvu zake nyingi kuwaza na kujipanga namna ya kuendelea kutawala. Ni viongozi wenye mawazo MGANDO kama akina Nape na Wassira ndio ambao wanaona kuwa CHADEMA ni tatizo kwa ccm kuendelea kutawala nchi hii. Lakini kwa sisi ambao tunafahamu mambo yanavyokwenda, tunaamini kuwa tatizo kubwa na ambalo linaingusha sisiem, siyo Chadema, Ni ccm yenyewe kushindwa kutatua matatizo ya MSINGI ya wananchi kama, KUPAA KWA BEI ZA BIDHAA MUHIMU, KUKOSEKANA KWA HUDUMA ZA AFYA, ELIMU, MAJI SAFI NA SALAMA NA mengine mengi.

  Watapanga mipango yote, lakini mwisho wa siku watashindwa kwa sababu kuibomoa CHADEMA, hakurudishi imani ya wananchi kwa CCM, ila kuongeza chuki dhidi ya viongozi wake. Kuiongea CHADEMA kila siku, ni kuingezea umaarufu na kuifanya izidi kupendwa zaidi. Hata mwalimu alisema, CCM HAIKUMZAA, na wala ccm haijamzaa Mtanzania yoyote yule...! Kama bado wanatumia mbinu za 1947 katika dhama hizi za sayansi na teknolojia, ni aibu.

  Washauri na viongozi wakuu wa ccm wameishia, hawana maono tena, hawana dira wala mwelekeo kama chama chenyewe. Yaani akili zao zimezeeka kama chama chenyewe. Mwalimu aliwaambia, "wananchi wataendelea kuichagua ccm na mabaya yake, kama hakutakuwa na chama kingine cha upinzani ambacho kinaweza kutatua matatizo yao!!!" Sasa hivi kuna mbadala, kama ccm ina mpango wa kuua upinzani Tanzania, Watanzania tutakuwa tayari kuongozwa na jeshi, kuliko kuicha ccm madarakani kwa miaka mingine mitano, ni kifo chetu na vizazi vyetu.

  Lakini, kikubwa na kizuri, ccm wamechoka kufikiri na akili zao zimedumaa, nashukuru kuwa tumeanza kuzifahamu mbinu zao mapema, hii ni katikati ya 2012, bado tuna miaka karibu mitatu na nusu kufika uchaguzi 2015, tunajipanga zaidi kukabiliana na mbinu zao, na tunazidi kutangaza sera zetu kwa wananchi hadi vijijini. Kasi hii ya elimu kwa umma ikiendelea hadi 2015, hakuna ubishi kuwa ccm haitashinda uchaguzi wowote ule ki halali, na ni imani yangu kuwa, hata polisi na wanajeshi watatuunga mkono, kwani ni askari wachache sana ambao wananufaika na uongozi wa ccm, wengi ni walalahoi tu kama waalimu, madaktari na watumishi wengine wa umma, tatizo ni kwamba wao hawawezi kugoma.

  STK ONE,
  TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED.....YES WE CAN, GOD BLESS CDM!!!!
   
 14. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kuwa Shibuda ni Bangusilo tu. Nyuma yake wapo Vilongola ambao wanasubiri muda muafaka kufanya vitu vyao. Nyimbo za ujana zinazoimbwa kila siku na baadhi ya wana CDM kibwagizo chake kitasikika kwa kisshindo 2014.
   
 15. T

  Tata JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,741
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Ushauri kwa Chadema: Anzeni kuandaa wagombea wa ubunge na udiwani kwa majimbo yote nchini sasa hivi. Hii itawapa muda wa kuwachunguza kama kweli wanawakilisha maono na matarajio yenu. Ule mkakati wa kungojea watu walioshindwa kwenye "rushwa" za maoni za chama tawala na kisha kuwapa fursa ya kugombea sio mkakati endelevu.
   
 16. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hako kabinti kamekosea tu, Shibuda anatakiwa apelekwe hospitali, msije mkamuonea bure.
   
 17. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Rai rai rai should stop searching for cheap popularity
   
 18. h

  hans79 JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  wameanza kufa bado kuzikwa kabla ya 2015 watakuwa wameishazikwa.
   
 19. k

  kkitabu Senior Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hawatuwezi tumeanza na Mungu na ataendelea kuwa upande wetu mpaka hapo ushindi utakapopatikana
   
 20. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  ukifikiri kwa kina utagundua hili gazeti la ccm linataka kukuza mgogoro,read between the lines you will realize this
   
Loading...