Gazeti mwananchi halijaitendea haki Chadema - limenisikitisha sana!!

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Wadau,

Nilipata mshtuko mkubwa niliposoma habari ya mgogoro baina ya kambi ya Zitto na Mbowe leo asubuhi.Habari ile iliandikwa kama vile ni gazeti la uhuru au Jambo leo. Wakati napitia ile habari niliamua kutoimalizia baada ya kumsoma mwandishi wa habari aliyeripoti ile habari.Huyo mwandishi ni mfuasi na shabiki mkubwa wa Zitto Zubeir Kabwe.

Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti na ili kuthibitisha haya ninaomba wadau mrudi nyuma hadi kipindi cha wabunge kususia hotuba ya Rais bungeni,mwandishi aliandika habari kuonyesha kwamba kuna mgogoro mkubwa kati ya wabunge wa kambi ya mbowe na Zitto.Kipindi cha uchaguzi wa chama mwaka 2014 mwandishi huyu alimshabikia sana Zitto na kuonyesha kuna mgogoro mkubwa sana na chama kimegawanyika mapande mawili.

Mwandishi huyu habari zake ni za kushangaza hasa inapoonekana kuna tofauti ya mawazo kwenye vikao na hupenda yeye kuita mgogoro.

Hivi kweli kwa mfano wa suala la Shibuda kung'olewa ilipigwa kura na wajumbe 18 wakaunga mkono huku 1 akipinga,mwandishi anapata wapi ujasiri wa kusema kambi ya Mbowe imemfukuza Shibuda.?? Inaonekana mwandishi huyu ana malengo maalum na hiyo habari aliandikiwa na mjumbe aliyekuwepo kwenye kamati kuu ili kuleta chokochoko kwa wanachama.Ni wazi mtakuwa na jibu ni nani aliyempa hiyo habari ya uchochozi.

Ushauri:

Gazeti la mwananchi ni miongoni mwa magazeti yanayopendwa na kuaminiwa sana na wananchi kutokana na habari zake.Namshauri mhariri asipoteze imani hii na azihariri mara mbilimbili habari zinazoletwa na huyu mwandishi kuhusiana na chadema kwani ana kikundi anachokipigania kwa maslahi fulani......

Nawasilisha....
 
It is not a balanced story, that is what I can say. Nilitegemea habari kama hiyo itoke kwenye gazeti la Uhuru au Mtanzania, au hata Jambo Leo!
 
lakini na sisi chadema tupunguze migogoro hii ni imezuka mpaka,
ukisoma vizuri chanzo ni LEMA

HABARI YENYEWE HIYO HAPO
http://www.mwananchi.co.tz/componen...ews-story/11524-moto-wawaka-tena-chadema.html
Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha Kamati Kuu na kuthibitishwa na baadhi ya wajumbe wa kikao hicho zinasema kuwa mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, ndiye alianzisha mvutano wa kutaka Zitto ang'olewe kutokana na kupinga wazo la kununua magari chakavu kutoka India.

Chanzo chetu cha uhakika kilidokeza kuwa mashambulizi dhidi ya Zitto yalianza pale alipounga mkono hoja ya Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo ambao walinukuliwa wakisema kwamba, isingekuwa sahihi kwa chama hicho kinachopinga ufisadi kufanya ufisadi kwa kununua magari chakavu wakati wamekuwa wakiibana serikali isifanye hivyo.

Baada ya Zitto kuunga mkono hoja hiyo, vyanzo hivyo nifafanua kuwa ndipo vurugu zilipoanza kwani Lema alianza kumrushia vijembe akisema kwamba Zitto ni tatizo na kwamba amekuwa akimtetea Shibuda.

Habari zinasema baadhi ya wajumbe walisema hoja ya Lema haikuwa na nguvu ya kumshutumu Zitto kwani Shibuda ni mbunge halali wa Chadema.

Duru zaidi za kisiasa kutoka ndani ya kikao hicho zinasema wakati mvutano huo ukiendelea, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alikuwa kimya huku kwa mara ya kwanza Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akiwa mmoja wa wajumbe waliomtetea Zitto.

"Wakati Lema akisema hivyo, Dk Slaa wakati wote alikuwa kimya na hakusema chochote. Mnyika alisimama na kumtetea Zitto kwa mara ya kwanza, na katika utetezi pia alikuwepo Grace Kiwelu," kiliweka bayana chanzo hicho.

Katika majibizano hayo inadaiwa ulifika wakati Zitto alisimama na kumwambia mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwamba mpango mkakati wake huo wa kujenga mtandao utakuja kumgharimu katika siku za usoni."Zitto alimwambia Mbowe mpango wake huo wa kujenga mtandao ungekuja kumletea matatizo hapo baadaye, "kilisema chanzo hicho kikimnukuu Zitto ndani ya kikao.

MY TAKE: kama hukusoma habari yote umekuja na hii hoja kutoka wapi? soma habari nzima ili uwe na uchambuzi wa kutosha, haya mambo ya watu siku hizi kujifanya mimi sitaki kusoma hiki kisha unajifanya kuelemisha watu kwa hoja uliyokataa kuisoma sio akili kabisa, si ni ili gazeti kila siku tunalisifia na lina aminika na watanzania wote, hata kwenye uchaguzi lilitusaidia sana chadema kwa kuandika habari huru na ukweli, tung'oe mzizi wa fitina kuna kitu ndani ya chama hakiko sawa na kukubali marekebisho nao ni ukomavu.
huu sio wakati wa kulazimisha vyombo vya habari kuegemea upande wetu wakati kuna madudu yanafanyika.
kama huyo lema hatopewa elimu ya jinsi ya kuongea na watu basi kuna mengi yatatokea, yeye anadhani ni shujaa wa taifa ili na hiyo ni uruka mbaya, lazima wote tusimame pamoja
 
Wadau,
nilipata mshtuko mkubwa niliposoma habari ya mgogoro baina ya kambi ya Zitto na Mbowe leo asubuhi.Habari ile iliandikwa kama vile ni gazeti la uhuru au Jambo leo.Wakati napitia ile habari niliamua kutoimalizia baada ya kumsoma mwandishi wa habari aliyeripoti ile habari.Huyo mwandishi ni mfuasi na shabiki mkubwa wa Zitto Zubeir Kabwe.
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti na ili kuthibitisha haya ninaomba wadau mrudi nyuma hadi kipindi cha wabunge kususia hotuba ya Rais bungeni,mwandishi aliandika habari kuonyesha kwamba kuna mgogoro mkubwa kati ya wabunge wa kambi ya mbowe na Zitto.Kipindi cha uchaguzi wa chama mwaka 2014 mwandishi huyu alimshabikia sana Zitto na kuonyesha kuna mgogoro mkubwa sana na chama kimegawanyika mapande mawili.
Mwandishi huyu habari zake ni za kushangaza hasa inapoonekana kuna tofauti ya mawazo kwenye vikao na hupenda yeye kuita mgogoro.
Hivi kweli kwa mfano wa suala la Shibuda kung'olewa ilipigwa kura na wajumbe 18 wakaunga mkono huku 1 akipinga,mwandishi anapata wapi ujasiri wa kusema kambi ya Mbowe imemfukuza Shibuda.?? Inaonekana mwandishi huyu ana malengo maalum na hiyo habari aliandikiwa na mjumbe aliyekuwepo kwenye kamati kuu ili kuleta chokochoko kwa wanachama.Ni wazi mtakuwa na jibu ni nani aliyempa hiyo habari ya uchochozi.
Ushauri:Gazeti la mwananchi ni miongoni mwa magazeti yanayopendwa na kuaminiwa sana na wananchi kutokana na habari zake.Namshauri mhariri asipoteze imani hii na azihariri mara mbilimbili habari zinazoletwa na huyu mwandishi kuhusiana na chadema kwani ana kikundi anachokipigania kwa maslahi fulani......Nawasilisha....

Ukweli unauma mwandishi alicho fanya ni kuandika ukweli mtupu. Ndio maana hata gazeti lenu la Tanzania Daima halikugusia habari hizo kwa vile limewaumbua kambi ya boss wao Mbowe
 
Osama is killed, Gaddafi is on pipeline!

Hii sasa itakua amekufa kwa mara ya nne, ukiacha ile aliyokufa kwa ugonjwa wa homa ya mapafu sijuui mwaka gani ule, na ile aliyouawa Pakistan kwenye msafara uliokua ukihama Peshawar, ana bahati ya kufa mara nyingi, duh!</SPAN>
 
nimetoa comment mwananchi la leo ktk habari "Moto wawaka Chadema, NI VITA YA KAMBI ZA MBOWE, ZITTO" na nimemlaani sana huyu mwandishi ameupotosha uma kwa makusudi..kupitia kichwa cha habari nadhani kamati ya gazeti imuadhibu haraka sana analiua lile gazeti taratibu, hili gazeti limeingiwa mdudu siku hizi maana kunahabari za ajabu sana utafikiri ni gazeti la kasheshe,ijumaa,sani ukiingia ndani habari ni tofauti kabisa

Mchungaji Mwasapila apinga dawa yake iwe ya vidonge
Rais Kikwete akubali nyongeza za mishahara
Kanisa Katoliki latoa maamuzi mazito
Tanzania yataka watangazaji wa Kiswahili UN waongezwe
 
Moto wawaka Chadema, NI VITA YA KAMBI ZA MBOWE, ZITTO

C

................ huku kwa mara ya kwanza Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akiwa mmoja wa wajumbe waliomtetea Zitto.

"Wakati Lema akisema hivyo, Dk Slaa wakati wote alikuwa kimya na hakusema chochote. Mnyika alisimama na kumtetea Zitto kwa mara ya kwanza, na katika utetezi pia alikuwepo Grace Kiwelu," kiliweka bayana chanzo hicho.

Oh My God, kwa mara ya kwanza!!!!!????? mwandishi/msemaji anataka nielewe nini hapa jamani?
 
swali, je aliyoandika ni ya uongoo?.. Kama ni ya Uongo mwaga ukweli hapa, Ila ukiishia tuu kumlaumu mwandishi wa habari eti kisa 'Zitto' katajwa humo unakua kama mkurupukaji tuu!..
 
Chadema uchu wa madaraka utawamaliza. Acheni usultani wenu msimamie demokrasia ya kweli kama lilivyo jina na chama chenu.
 
Ina maana mlikuwa hamujui uandishi wa Semtawa???
Muda wot mlikuwa hamjamstukia mpaka mlipkuja kugundua kuwa ni mpambe wa Zitto? Hii inadhihirisha kuwa ni namna gani hampo fair katika kujadili matatizo yaliyo ndani ya jamii yetu, yaani wakiumizwa wengine kwenu sawa, ila ukiumizwa upande mliosimamia hapo ndiyo mnagundua kuwa hakuna haki......kama ni kweli mnajinadi kuwa ni great thinkers hamtakiwa ku-side na kokote bali muwe rationally ili mutoe mawazo ambayo ni constructive.....Jibadilisheni ili mufanane na maana halisi ya Great Thinkers else mtaishia kuwa followers, kitu ambacho ni sawa na tusi ukilinganisha na namna mnavyotaka kuwa.
 
Tatizo lenu mnadhani Tanzania yote ya kwenu peke yenu.Chadema imenufaika sana na uungaji mkono usio wa haki kutoka media. Wakati wa uchaguzi mlipewa coverage kubwa kuliko vyama vingine vya upinzani. Hii mliona sawa tu. Mpaka mkafikia mahali mkadhani mnayo haki ya kuamua nani ni mpinzani na nani si mpinzani!
Sasa vyombo vya habari vikiwatupa mkono kidogo (tena kwa kuripoti ukweli) mnalalamika!
Ijengeni kampuni yenu hiyo (CDM) vizuri! Msiwaache wahuni (Cha Arusha) waharibu mafanikio mliyoyapata!
 
Gazeti limesema uongo wa kutisha kwani hata kusema kuwa Mnyika alisimama na kumtetea Zitto ni uongo kw2ani hakuwepo kwenye kikao kutokana na Mnyika kuwa nje ya nchi kwa safari za kibunge (kamati yake ya nishati na madini) sasa huyu mwandishi ametoa wapi hayo anayosema?

Ramadhan Semtawa alipelekwa masomni nchini Uingereza kusoma na kulipiwa na kundi la mapacha watatu , ila account ilioyokuwa inatumika kutuma fedha ni ya Andrew Chenge, mpaka hapo unaweza kuelewa nini kinaendelea kati yake na kundi la mapacha watatu.

Watapata aibu sana itakapokanushwa hii taarifa yao na ukweli kuwekwa hadharani.

Haja ya kununua magari haikuwepo kabisa kwani suala hilo lilishafanyiwa maamuzi kikao cha tarehe 19 March 2011 na iliamuliwa yanunuliwe magari mapya tena sio kutoka Japan wala India , sasa hawa labda hiyo source yake ilikuwa inashiriki kikao kilichonunua Mahidra zile za Jeetu..........
 
Acha uongo wewe! Kitila Mkumbo ni member wa hicho kikao na hakukana yote hayo. kaangalie post ya "shibuda Out"!
Ukipenda tumia na akili wewe!
 
Acha uongo wewe! Kitila Mkumbo ni member wa hicho kikao na hakukana yote hayo. kaangalie post ya "shibuda Out"!
Ukipenda tumia na akili wewe!

Kitila ni member, mwambie aje aseme kuwa ;
  1. KUWA MNYIKA ALIKUWEPO KWENYE KIKAO.
  2. KUWA KULIKUWA NA HOJA YA KUNUNUA MAGARI NA YEYE ALIITETEA
  3. ZITTO alisimama na kumwambia Mbowe suala sijui la mitandao ama chochote kile kwani hakukuw2a na majibizano kati ya Zitto na Mbowe hata kidogo sasa Semtawa kayatoa wapi haya?
 
Ametumia taaluma yake..... mwacheni jamani, sometimes wana CDM mkubali kumeza hata kama chungu
 
Back
Top Bottom