Gazeti la Uingereza laimulika serikali ya Magufuli na kusema inaelekea kwenye uimla na kuua upinzani isikosolewe

Kama hii tuhuma ya Rais kulindwa na Wanyarwanda ni ya kweli maana yake hana imani na jesh letu kwa sababu anazozijua yeye. Na kama hana imani nalo inakuaje azuie wapelelezi kutoka nje kuchunguza matukio ya vifo na mashambulio vya wapinzani kma yeye hta jesh letu haliamini?.
 
Kiongozi wa watanzania,Rais wetu,analindwa na wanyarwanda? Hawa wanyarwanda hawa?wanaingia ikulu wanavyotaka? Vijana wa kitanzania wamehitimu mafunzo ya usalama wanawekwa pembeni wanachukua nafasi wanyarwanda?

Hawa wanyarwanda waliokuwa wanamlinda baba yake na Rais wa Congo Lurent Kabila,alipokosana na Kagame wakamwua ikulu ?

Tumeenda kufanya urafiki na mtu ambaye ana tuhuma za kumpindua Nkurunzinza?

Mtu ambaye naye ni jadi yake kuwauwa wapinzani wake kama Gen. Kayumba Nyamwasa,na hata sasa ka binti ka miaka 30,Diane Rwigara anakasumbua na kesi,kisa kaligombea urais,kweli binti wa miaka 30 naye anakandamizwa? Achilia mbali kuuwawa kwa baba yake mzee Rwigara kwa ajali ya kutengenezwa na kagame kisa tu walitofautiana kisiasa? Pia tukumbuke,Mzee Rwigara alikuwa mfadhili wa kagame akiwa msituni,na baada ya kutofaitiana kagame akaanza kuvunja maghorofa ya familia hiyo mjini Kigali na kuwanyanganya Mali zao
aisee... noma sana!
 
Yaani itokee sisi hapa nchini tupate jarida la kuiandika Uingereza au nchi yoyote ile mnadhani nchi hiyo ndo itatishika kwa kuandika kwetu?ndo watabadilisha mtazamo wao na mfumo wao eti tu kisa kuna majungu tumesema?kwanza jarida linaweza toka kwetu lakini kumbe limechapishwa na mwana siasa mwenzao huko huko ila kalifyatulia Tanzania kwa lugha ya kiswahili.
 
hii ya wanyarwanda kuongezewa kwenye ulinzi haiwezekani, uenda hisia, tuna imani na Wetu, ukichukua wa jirani halafu mkapishana mbeleni si balaa
 
Mabepari at work! Hawa hata siku moja hawawezi kufurahia kazi ya serikali hii ya awamu ya 5, imewaumbua vya kutosha..Hicho wanachoandika tulikitarajia.
 
Na nukuu serikali inaweza kuongeza mafanikio ya kiuchumi. Rais Magufuli kama anaweza kuleta mafanikio ya kiuchumi ndicho kila mtanzania anapenda kukiona.
 
Msalika yupo kwa kazi maalum ya kuua....nadhani Kipilimba hatakubali kutumika kuchafua mikono yake maana ni born again,,,,,sasa kuua kwa sababu kutawala si suala muafaka kwa Kipi naamini hivyo...ila kwa Msalika naamini atafurahia sana....maana hana wokovu na hajali h ubinadamu!!
 
Saizi mtu anapo izungumiza tanzania anaogopa hata kusema tanzania ni nchi ya amani. Kwanza ananzia wapi ikiwa watu wanapigwa risasi mchana kweupe.

Hii post yako imenichekesha sana...hao polisi walioua Black Americans huko USA vepeee..na hao 58 waliokufa juzi Las Vegas kwa risasi ni mbwa si ndiyo..Of all those events ushasikia wamarekani wanasema nchi yao siyo ya amani???? Only in Tanzania where fools believes in western security systems
 
Hii post yako imenichekesha sana...hao polisi walioua Black Americans huko USA vepeee..na hao 58 waliokufa juzi Las Vegas kwa risasi ni mbwa si ndiyo..Of all those events ushasikia wamarekani wanasema nchi yao siyo ya amani???? Only in Tanzania where fools believes in western security systems
Endelea kucheka
 
Tuhuma za rais kulindwa na watu kutoka nchi nyingine ni dharau kwa watanzania wazalendo. Kama ni uongo kwanini serikali isikanushe tuhuma hizo!
 
Jamani mwambieni dereva wa lori asimame tuweke turubai, mvua imeanza tunalowa huku jama. Tunapiga kelele kapandisha mziki sana
 
Mabepari at work! Hawa hata siku moja hawawezi kufurahia kazi ya serikali hii ya awamu ya 5, imewaumbua vya kutosha..Hicho wanachoandika tulikitarajia.
Hakuna mtu anayeitwa "bepari"sasa hivi...hilo neno halitumiki badala yake tunasema wawekezaji.Wameundiwa na kituo maalum na serikali kinaitwa TIC.Kazi ya kituo hiki ni pamoja na kuvutia hao unaowaita "mabepari"Waje kuwekeza kwani ndio wenye mitaji.
Kama ulisoma zamani basi elimu yako ime expire na ndio maana huelewi hata mfumo wa uchumi ulivyo duniani kwa sasa.
Labda ungeweza kuwauliza serikali,kwa nini wameweka kituo cha kuvutia "mabepari?"
 
Kuweni watu wazima. Gazeti la uingereza limeandikwa na watu kama sisi na hayo ni mawazo yao. Msijishushe kihivyo!
 
Back
Top Bottom