Gazeti la uhuru wanakwepa kusimamia ukweli au kuwajibika? - ona maoni waliyoacha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la uhuru wanakwepa kusimamia ukweli au kuwajibika? - ona maoni waliyoacha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 6, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika hali ya kushangaza gazeti la uhuru wamekanusha kuendesha maoni yaliyokuwa yanahoji utendaji wa serikali. Kwa sasa imeondolewa. Na wanasema hawaendeshi maoni ya aina hiyo.
  Cha ajabu ni kwamba bado katika tovuti yao kuna kura nyingine ya maoni kuhusiana na Utunzaji wa Mazingira hapa Dar es Salaam. Aina ya maswali yaliyoko hapo ni yale yale yaliyokuwa yakiuliza uongozi.
  Je haya ya mazingira nayo yamechakachuliwa? Kama si kwa nini yanafanana mtindo wake?
  Kama yamechakachuiwa mbona wameyaacha.

  Jioneee mwenyewe hapa chini
  Ni wajibu wa Kila Mwananchi 3 37.5%
  Itafutiwe Mzabuni 2 25%
  Manispaa Ziwajibishwe 2 25%
  Ni wajibu wa Manispaa za Jiji 1 12.5%
  Inaridhisha na Ibaki ilivyo 0 0%

  Number of Voters : 8 First Vote : Tuesday, 05 October 2010 16:42 Last Vote : Wednesday, 06 October 2010 02:54
  Uhuru Publications Ltd - Gazeti Uhuru, Mzalendo na Burudani
  Kama imechakachuliwa basi pia wanahitaji kuwajibika. Inakuwaje mtandao unaoangaliwa kila siku uwe unatoa maoni ukurasa wa mbele hadi wafikie wageni mamia watendakazi wasione?
  Kuna haja ya kuwajibika aidha kuwa wakweli na kusimamia ukweli. AU KUWAJIBIKA KWA UZEMBE KATIKA KAZI.
  KWA VYOVYOTE KUNA MASWALI YA KUJIBU.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  au ndo kuajiliwa kwa mtoto wa mjomba, mimi sikubaliani nalo kwa hili inawezekanaje watu wakafika zaidi ya 100 kutoa maoni wewe unasema umehujumiwa. Je tz ni nchi ya wasanii!? Shame on you uhuru!
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hiyo poll iliyoondolewa ni ya kwao Uhuru na inawezekana kabisa walishinikizwa kuweka kura hiyo na Wakubwa wa CCM (kama walivyofanya kwenye Daily News na baada ya kuonyesha kuwa Dk Slaa mshindi wakishinikizwa kuandika maoni ya ajabu kwenye gazeti la Daily News) sasa kwa kuwa maoni ya Watanzania yameonyesha kuwa Rais ni Dk Slaa wakubwa wao watakuwa wamewajia juu sasa wanatafuta mlango wa kutokea wakati wameshachelewa.
   
Loading...