AmaniKatoshi
Senior Member
- Mar 31, 2009
- 158
- 14
WanaJF nimestushwa na habari iliyoandikwa na gazeti la UHURU toleo la leo jumatano tarehe 8 Dec, 2010. Nimeangalia magazeti mengine, hakuna hata moja lilioandika walichoandika GAZETI HILI LA SEREKALI. TAfadhali soma habari hii hapa chini
Mbunge ahamasisha machinga kuchoma mali za halmashauri
Wednesday, 08 December 2010 07:55 newsroom
* Pia, ataka viwanda, hoteli za wana-CCM zichomwe
* Ni iwapo CHADEMA itashindwa kiti cha umeya wa Jiji
NA PETER KATULANDA, MWANZA
ìTunasikia maofisa wa Jiji wanataka kuja kupima viwanja katika baadhi ya maeneo kwa lengo la kuwaondoa na kuwauzia matajiri, msikubaliane nao na waambieni waondoke, wakiwabishia basi mchome magari yao kuonyesha kuwa hamkubaliani nao kupora ardhi yenu,î alisema. Alidai kwamba baadhi ya wana-CCM wanawashawishi madiwani wa CHADEMA wamchague Meya wa Jiji kutoka CCM, hivyo wananchi wasikubaliane na matokeo yatakayotangazwa Desemba 17, mwaka huu, iwapo Meya hatatoka CHADEMA.
Mbunge ahamasisha machinga kuchoma mali za halmashauri
My take:
Linganisha habari hii na habari iliyoandikwa na gazeti la majira la leo www.majira.co.tz
Pia najiuliza kama ni kweli amesema hayo ni maneno ya uchochezi na ya kuvunja sheria. Sasa kama polisi walikuwepo mkutanoni hapo si wangemkamata?
Pia, ingewezekana hadi leo vyombo vingine vya habari au serekali isingetoa tamko?
Pia kwa nini hawajamquote Wenje na kuandika maneneo aliyotamka bila kuchakachua?
Huyu Jumanne Maghembe ndie waziri wa serekali yetu?
KAMA NI KWELI WENJE AHOJIWE NA KUCHUKULIWA HATUA< KAMA SIO KWELI >CHADEMA LAZIMA WAJIPANGE NA KUMUWAJIBISHA MWANDISHI HUYU NA GAZETI HILI LA UHURU ILI IWE FUNDISHO

MBUNGE wa Nyamagana kupitia CHADEMA, Ezekia Wenje, anadaiwa kuanza siasa chafu kwa kuhamasisha wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga wachome mali za Halmashauri ya Jiji la Mwanza kama chama hicho hakitatwaa kiti cha umeya. Wenje pia anadaiwa kuwahamasisha wafuasi wa CHADEMA kuchoma viwanda na hoteli za baadhi ya matajiri ambao ni wanachama wa CCM kama watakikosa kiti hicho. Alitoa maelekezo hayo juzi saa 11.00 jioni, wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Sahara kata ya Pamba, wilayani Nyamagana. Akizungumza kwenye umati uliojitokeza kumsikiliza, alisema wananchi wasikubali maeneo yao yapimwe na maofisa ardhi wa jiji
watakaokwenda kupima kwa lengo la kuwalipa fidia ili wauze viwanja hivyo, wachome moto magari yao .
watakaokwenda kupima kwa lengo la kuwalipa fidia ili wauze viwanja hivyo, wachome moto magari yao .
ìTunasikia maofisa wa Jiji wanataka kuja kupima viwanja katika baadhi ya maeneo kwa lengo la kuwaondoa na kuwauzia matajiri, msikubaliane nao na waambieni waondoke, wakiwabishia basi mchome magari yao kuonyesha kuwa hamkubaliani nao kupora ardhi yenu,î alisema. Alidai kwamba baadhi ya wana-CCM wanawashawishi madiwani wa CHADEMA wamchague Meya wa Jiji kutoka CCM, hivyo wananchi wasikubaliane na matokeo yatakayotangazwa Desemba 17, mwaka huu, iwapo Meya hatatoka CHADEMA.
Tumewaeleza madiwani wetu kuwa siku hiyo tutapiga kura za wazi kumchagua Meya wa Jiji la Mwanza, atakayetusaliti tunaanza naye kisha tunawafuata matajiri wa CCM na kutatahakikisha mali zao tunaziharibu au kuzichoma ili wajue hatuko tayari kuibiwa,î alisisitiza Wenje.
Aliwataka wafanyabiashara ndogo ndogo waendelee kufanya biashara zao popote bila kubugudhiwa na mgambo wa jiji. Wenje pia alikaririwa akiwaonya walimu wa sekondari na shule za msingi kutowatoza wanafunzi michango yoyote, huku akisema anamshukuru mfanyabiashara mmoja mzalendo kutoka Dar es Salaam kwa alichodai kumsaidia kuwa mbunge. Kutokana na kauli hizo, baadhi ya wananchi akiwemo Jumanne Magembe na wengine ambao hawakutaka kutajwa majina yao waliponda kauli za Mbunge huyo na kudai kwamba ni uchochezi wa kisiasa ambao utasababisha uvunjifu wa amani hapa.
ìHuu ni uchochezi na siasa chafu, Wenje amezungumza maneno ya uchochezi anapaswa kukemewa na mamlaka husika kabla mambo hayajawa kama Kenya na kusababisha machafuko kwa manufaa ya wanasiasa wasiokuwa na uchungu na damu ya Watanzania,î alisema Magembe. ìNyie waandishi, hayo ndiyo maneno ya kuja kuwaeleza wananchi kama si kuleta uchochezi?" alihoji mkazi mwingine na kuongeza: "Hii ni hatari kwa wananchi na wafuasi wa vyama vya siasa, jiji lina sheria zake na pia kila jambo lina utaratibu wake wa kisheria."