Gazeti la THIS DAY na gazeti la RAI

TangaKunani

New Member
Sep 12, 2006
4
0
Hivi kati ya haya magaezti mawili lipi ambalo lina status ya kuheshimika?Maana naona gazeti la THIS DAY limekuwa likipata scoops za kila namna lakini halikadhalika kuna taarifa kuwa hili gazeti ni chombo za watu fulani fulani amabao wana ugomvi na liopo madarakani...lakini unaweza kusema the same about gazeti la RAI

Sasa basi kuanzia news mpaka credibility za source za hizo news.Je gazeti la RAI linalo forums? na je mtu uki compare na ku contrast lipi amabalo lina mwelekeao wa kuaminika au yote ni Matabloids tu?
 
tangakunani said:

Ni vigumu kuyalinganisha Rai na This Day kwa sababu kuu moja ya msingi.Rai ni JARIDA la kila wiki wakati This Day ni GAZETI LA KAWAIDA la kila siku (unless ulikuwa unazungumzia KULIKONI).

Pia,RAI linaelemea sana katika makala za wachambuzi binafsi wakati This Day linatawaliwa zaidi na ripoti za waandishi wake binafsi japokuwa kuna mchango mkubwa wa columnists ambao si waajiriwa wa gazeti hilo.

Kwa mawazo yangu binafsi,nadhani Rai lilikuwa gazeti zuri sana,pengine karibu kabisa na lilivyokuwa Family Mirror.Hivi karibuni gazeti hilo naona kama limepoteza mwelekeo,hasa kwa vile baadhi ya wakongwe wa gazeti hilo walikumbwa na kimbunga cha wanamtandao.Nadhani kwa muda huu,This Day (na Kulikoni) ndio the best in the country.Suala la who owns the paper sio muhimu sana kwa vile lazima gazeti limilikiwe na mtu flani,lakini haimaanishi kuwa kila litachoandika ni dhidi ya wapinzani wa mmiliki huyo.Suppose Tanzania ingekuwa haina rushwa,unadhani This Day na magazeti mengine yenye courage ya kuandika wala rushwa yangeandika habari hizo?Yanaandika kwa vile habari hizo zipo,na huwezi kuzikuta Uhuru/Mzalendo au Daily News.
 
Hayana unafuu yote mana wote wanaripoti habari zenye faida kwao na serious issue hazitajiki kirahisi kama si kwa manufaa ya mtu fulani .Forum hii ni bora zaidi ya magazeti hayo
 
Mzeeshughuli....
Ni kweli hizi forums ni bora mara elfu kuliko hayo makaratasi yanayoitwa magazeti. All of them are for their survival.
 
Mzeeshughuli Bwana said:
Hayana unafuu yote mana wote wanaripoti habari zenye faida kwao na serious issue hazitajiki kirahisi kama si kwa manufaa ya mtu fulani .Forum hii ni bora zaidi ya magazeti hayo

What serious issues?Manji kuiba hela za umma sio serious issue?Prof Mhalu kuiba bilioni mbili sio serious ishu?Come on,you cant serious man!Tatizo ni kwamba Manjia amefanikiwa kuwazuga Watanzania kwamba magazeti ya Mengi yanamwandama kwa sababu binafsi,lakini hajafanya jitihada yoyote kuthibitisha kwamba kinachoandikwa dhidi yake ni uzushi mtupu.Hivi tuwe wakweli,magazeti yetu tuliyoyazowea (Uhuru/Mzalendo na Daily News/Sunday News) yalikuwa yanatuambia nini zaidi ya kuripoti hotuba za viongozi?

Watanzania wamezoweshwa sana utamaduni wa habari "za kawaida" na sio investigative journalism.Na wala rushwa wamekuwa wakitumia udhaifu huo wa Watanzania kuhakikisha magazeti yanayofichua walaji yanapata picha mbaya.Mnakumbuka kijarida kiitwacho Sanifu?Pengine hicho hakiwezi kutoa mfano mzuri.Mnalikumbuka Family Mirror?Nilikutana na Mzee Macha aliyekuwa Mhariri wa mwisho wa gazeti hilo na aliyonieleza yananifanya niyaone jasiri sana magazeti yanayoataja majina ya watuhumuiwa na kuripoti skandali.Kwa waliolisahau Family Mirror,hilo ndio gazeti pekee lilikalia kidedea suala la mapunjo ya wazee wetu waliokuwa watumishi wa jumuiya ya afrika mashariki.

Kila anaeyalaumu magazeti ya kisasa anakimbilia kwenye hoja kuu mbili

1.hayaandiki serious issues
2.yanatetea maslahi ya owner.

Hata hivyo,wanaolaumu hawajawahi hata mara moja kutueleza kwamba ni serious issues gani ambazo magazeti hayo hayo yamezipuuza.Yaani kwa mfano,kuna tatizo la gao wa umeme na magazeti hayo yamekaa kimya,au ukimwi unamaliza watu na magazeti hayo hayasemi lolote,au pengine nchi inaliwa na wajanjwa wachache na magazeti hayo yamekaa kimya

Na katika hilo la kutetea maslahi ya owners,walalamishi hawa pia wanashindwa kutupa uthibitisho kwamba This Day limemripoti Prof Mhalu kwa ugomvi kadha na kadha kati yake na Mengi,au hadithi halisi ya "ugomvi" kati ya Mengi na Manji,au ya Mengi na Warioba.

Mwenyekiti Mao alisema "No research,No Right to Speak"
 
Yeah, we are tired of mafumbo mafumbo kind of reporting now. If the issue is true and confirmed, why hide the names, offices and every important hint to the extent that the reader is lost.

While akina THISDAY ni wa kupewa thumbs up, I become a little bit suspicisous when the same issue keeps on being repeated over and over, even when there is no new fact, ... and especially when the issue is related to exposing a perceived rival of one of the owners. It makes me wonder whether it is pure and professional investigative journalism.

Since we have missed this kind of openness before, one would expect there is a lot more to be spilled out than running the same news over and over.
 
Kulikoni said:

They never gonna stop until the government acts on the said allegations,or the accused prove their innocence.
 
Hivi kati ya haya magaezti mawili lipi ambalo lina status ya kuheshimika?Maana naona gazeti la THIS DAY limekuwa likipata scoops za kila namna lakini halikadhalika kuna taarifa kuwa hili gazeti ni chombo za watu fulani fulani amabao wana ugomvi na liopo madarakani...lakini unaweza kusema the same about gazeti la RAI

Sasa basi kuanzia news mpaka credibility za source za hizo news.Je gazeti la RAI linalo forums? na je mtu uki compare na ku contrast lipi amabalo lina mwelekeao wa kuaminika au yote ni Matabloids tu?

ugomvi gani ? tudadavulie ?
 
Back
Top Bottom