Gazeti la Tanzanite: CHADEMA, yajiandaa kwenda Ujerumani na Marekani mwishoni mwa mwaka: Lengo ni kuomba msaada wa kupambana na Serikali

Kama huzitaki mimi nikufanyaje.
Mkuu fanya kazi usibishane na Mimi. Nina imani wewe na Mimi ni wa kada mbili zenye utofauti mkubwa sana. Sikukatishi tamaa ila nakuagiza fanya kazi. Huu ni muda wa kufanya kazi
 
Mkuu fanya kazi usibishane na Mimi. Nina imani wewe na Mimi ni wa kada mbili zenye utofauti mkubwa sana. Sikukatishi tamaa ila nakuagiza fanya kazi. Huu ni muda wa kufanya kazi
Kama sio mbishi na mshari kwanini uje na hiyo id yako nyingine sijui Doglas Salu na kuanza kunitukana.
 
Nawaza uhalisia na maana ya "Mchumia tumbo" na kutafakari maisha ya mtu ambaye ni mchumia tumbo. Hulka ya mchumia tumbo ni mara nyingi huwaza kuangalia tumbo lake, huwa analenga kumfurahisha mwenye kulijaza tumbo lake. Kamwe hajali madhara tarajali ya anachosema au kutenda, yeye mawazo yake ni tumbo lake tu. Kwa kifupi anawaza kutumia tumbo na sio akili timamu.

Watanzania tuepuke kuwa wachumia tumbo, mzalendo anajulikana na mchumia tumbo anajianika kwa matendo na maneno yake.
 
Kama sio mbishi na mshari kwanini uje na hiyo id yako nyingine sijui Doglas Salu na kuanza kunitukana.
Mkuu sijui unapata faida gani kunisingizia uongo. Sijawahi kuwa na ID mbili hapa JF na ni kwa nini nikutukane? Kwa kipi labda?

Nimekuagiza ufanye kazi
 
CHADEMA kusema kweli mmefeli. Mnaleta upinzani wa hawamu wa kikwete wa kutafuta baya kwenye kila kitu.

Hawamu ya Kikwete kukosoa ilikuwa sawa kabisa. Maana jamaa alizingua. Rushwa ilitawala sana.

Safari hii kwa kuwa jamaa anajitetea kwa kusema anajenga viwanda na kadhalika, mlitakiwa kubadilisha gia.

Yaani nyie kwa sasa ni sawa na mtu analeta kisu kwenye ugomvi wa bunduki.

Fanyeni mpango mlete wawekezaji majimbo yenu. Muwaonyeshe ma CCM kuwa ingawa wanaba, majimbo yao yanaendelea.

Mkifanya hivyo, kura mtapata tu hata wakiiba. Maana wananchi watakuwa wameona mlichofanya.
Lakini nyie mkiamka asubuhi lawama na malalamiko, mchana lawama na malalamiko, usiku tena yale yale.
Yaani kutwa mara tatu. TUMEWACHOKA EHH...

Na akili kama hizi eti wangeenda ISIS ndo kabisaa mnaonekana kama siasi zimewashinda mnataka kumwaga sinia la ubwabwa kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu haya unayosema unafikiri CHADEMA hawafahamu..... Nakumbuka kina lwakatare na bulaya walienda kugawa madawati na vifaa vya hospitali kwa nyakati tofauti ila walivyofika mlangoni vikakataliwa na wakuu wa hizo taasisi kwa maagizo kutoka juu!! Wote tumeona mradi wa UKAWA wa maendeleo ya jiji la DSM ulivyoporwa na CCM na Meya Boniface alitolea ufafanuzi.... Je hayo yote sio mambo ya maendeleo?? Kupigania miswada ya rasilimali yenye tija kupitishwa bungeni hayo sio maendeleo??

2.Mikutano ya ndani ya kutafuta wawekezaji inafanyika muda gani wakati ilishapigwa marufuku imekuja kuruhusiwa mwaka huu tu..... Tena kwa masharti magumu je unategemea hao CHADEMA watajiorganize muda gani?? Mfano zitto alifanya ziara kukagua utekelezaji wa ahadi za ACT ila alizuiwa!! Sumaye alizuiwa ubungo alipoenda kukagua mradi wa maji ambao CHADEMA waliahidi... Hayo sio maendeleo? Huoni wanavyohujumiwa??

3.Kingine wanacholalamika upinzani sio kuhusu muenenendo wa serikali bali wanavyoteswa..... Sasa lisu anapigwa risasi,uongozi wote wa CHADEMA taifa una kesi mahakamani zaidi ya 10, hivi unaposema wanalalamika ulitaka wafanye nni?? Sawa unatafuta wawekezaji ilihali unawaza jinsi ya kukwepa risasi,kuibiwa kura na kupewa kesi??

Ieleweke... Upinzani wanalalamika mazingira ya siasa mabovu wewe unasema suluhisho ni wawekezaji?? Sasa bila mazingira sawa ya kisiasa hao wawekezaji si watawekewa zengwe na kuitwa wahujumu uchumi??
 
Mkuu Mgambilwa ni mntu , with due respect, acha hii tabia ya kutuletea habari kwa njia hii. Kama umenunuliwa scanner ya kutuletea mada zinazokupendeza na kutoka magazeti yanayokupendeza, jua kuwa tupo unaotukwaza. Uwe unaleta hata habari za maendeleo kama uwekezaji na kilimo au hata elimu. Acha kila siku kuleta 'vihabari vya kishabiki'.
bora unisaidia mkuu, kila nikimkosoa hanielewi hadi amejenga imani flani juu yangu.
Hapa ana promote gazeti lake Tanzanite, lkn pia anafikisha ujumbe alioukusudia.
Huyu sio mwandishi bali mwandishi njaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mgambilwa ni mntu , with due respect, acha hii tabia ya kutuletea habari kwa njia hii. Kama umenunuliwa scanner ya kutuletea mada zinazokupendeza na kutoka magazeti yanayokupendeza, jua kuwa tupo unaotukwaza. Uwe unaleta hata habari za maendeleo kama uwekezaji na kilimo au hata elimu. Acha kila siku kuleta 'vihabari vya kishabiki'.

Hahahahaha Mkuu. Jamaa harudi tena huyo
 
View attachment 849963
Viongozi Waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wapo katika maandalizi ya kufanya Ziara kabla ya mwishoni mwa mwaka huu 2018 kwenda katika Nchi za Ulaya zikiwemo Ujerumani na Scandinavia, pamoja na Marekani, ikiwemo Bunge la Congress kwa lengo la kuomba msaada dhidi ya masuala ya kisiasa na hali yao dhidi ya Serikali.
Viongozi hao wanakwenda kudai kuwa, wanaonewa, hawana haki dhidi ya Nchi yao, wananchi na wabunge wao. Vilevile, watalalamikia juu ya Ukanda Imani was demokrasia ndani ya Nchi. Aidha, watalalamikia juu ya vitisho na usalama wa uongozi wao, nafasi zao na mwenendo wa uchaguzi kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Je, CHADEMA wakienda huko watapata nafasi ya kuongea kwenye Bunge la Congress? Endapo wataipata hiyo nafasi, nini athari zake kwa Siasa za Tanzania hasa kuelekea 2020. Je, Marekani atataka kutulima tena kwenye misaada? Je, unadhani Magufuli anaweza kuogopa ghadhabu za Marekani, Ujerumani na Scandinavia (Norway, Sweden, Finland, Denmark na Iceland)? Je, Norway (Statoil/Equinor) na Nchi nyingine yanakotokea Makampuni ya gesi, wanatuvizia baada ya mwenendo wa kobe katika makubaliano ya kujenga LNG nchini?

View attachment 849962
Tangu nasoma taarifa za hili gazeti hasa zinazohusu shutuma za wapinzani hakuna hata siku moja mwandishi amewapata kwenye simu kujibu shutuma hizo. Ona hapa alivyomaliza habari yake kwenye paragraph ya mwisho......"Tanzanite lilifanya jitihada za kumtafuta Dkt. Mashinji na Mbowe ili waweze kutoa ufafanuzi wa safari waliyopanga kuifanya katika nchi hizo na madai ya kumtumia Mange ili awasemee juu ya kesi yao, simu zao hazikupatikana......." ndiyo stori yao ilivyoisha kama kawaida yao.
 
Mkuu Mgambilwa ni mntu , with due respect, acha hii tabia ya kutuletea habari kwa njia hii. Kama umenunuliwa scanner ya kutuletea mada zinazokupendeza na kutoka magazeti yanayokupendeza, jua kuwa tupo unaotukwaza. Uwe unaleta hata habari za maendeleo kama uwekezaji na kilimo au hata elimu. Acha kila siku kuleta 'vihabari vya kishabiki'.
Mselewa mbona unanionea mzee? Endapo ingekuwa inaongelea Serikali ungeyasema haya ama tatizo ni lipi ndugu? Kama humu tunapaswa tu kuandika ya kuikosoa tu Serikali basi tuambiane lakini kama tunapaswa kuandika taarifa yoyote ya kisiasa ambayo ni fikirishi, nina uhakika utaniunga mkono kuwa, lolote linalotokea upande wa Serikali ama upinzani, iwe hearsay lazima tukiweke humu watu wenyewe watachuja pumba na mchele.
Hata hivyo, siandiki tu juu ya Siasa, unaweza kutembelea kwenye majukwaa ya Intelligence na Historia pia niko mzee. Anyway sorry kwa wote ninaowakwaza japo mtakubaliana na mimi tukubaliane kutokubaliana, as long as wote tunataka tujenge nyumba moja, right?
 
Akili zako ndogo sana, pole kwa kutumiwa
Ndugu mi ninatarajia utoe hoja ambayo ni alternative na yangu kwani kusema tu akili tangu nikiwa ndogo, tayari umelazimika kujipima kwa kuwa huwa unajiona una akili ndogo. Utasubili sana ndugu... aaahhh...
 
Matusi ya nini mkuu. Kuwa mvumilivu na ndio siasa ilivyo.Sihitaji kukufukuria propaganda uchwara za ufipa kwa mtu ambaye unashinda jf na unajiita great thinker.Kuna hbr zikiandikwa na ccm kama ni uongo zinaonekana tu na cdm pia hivo lkn siwez simamisha mishipa as if nalipwa.Kila hbr unayoiona humu changanya na zako kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Well said. Tukijidai kupinga baadhi ya taarifa walahi kuna watu watakosa cha kuandika na hiyo itatusaidia wengine tu-focus kwenye vitu vya maendeleo ya kiuchumi. Lakini cha ajabu hao wasiofurahia ndio hao wanaofurahia Dreamliner ikipata hitilafu. Dreamliner ilikamatwa, watu humu walifurahia sana na ikawa inaonekana kama tunafurahia ndege ya Kenya kukamatwa. Hamuwezi kujenga Nchi kwa kukalia kutafuta mabaya tu. Mkitaka watu wote wawaunge mkono basi wekeni balance na mpongeze mazuri ya Serikali na ya Upinzani. Siyo kila kitu mnakosoa tu tena kuliko waliosomea hicho kitu.
 
Back
Top Bottom