Gazeti la Tanzania Daima linatafuta kisingizio cha kufungiwa! Nini kifanyike?

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,532
Kwa observation yangu gazeti hili ni kama vile linataka kufa lakini halitaki kufa kifo cha asili yaani kwa kukosa wanunuzi.

badala yake gazeti hili limeamua kufanya makosa mfululizo ili mkono wa sheria ulishukie na kulifungia pengine kutengeneza kiki ya chama flani.

Ukiwa mwerevu na mfuatiliaji utagundua kuwa gazeti hili haipiti wiki bila kufanya blunder.

Je nini ushauri wako kwa gazeti hili na serikali?
 
Hata vipicha vya kutushawishi hujaweka unataka tujadili maandishi bila ushahidi
Sihitaji kuweka picha...wewe ni Great thinker...go and read the articles of this newspaper..
in past 3 months...utanielewa vyema.
 
Ungetoa mifano ya hizo habari kama reference. Sasa unaposema "go and read..." unafifisha hoja yako!
hoja itafifia kwa mvivu wa kusoma.
Ungekuwa ni GT na msomaji wa magazeti usingeshindwa kuelewa hoja rahisi namna hii.Au labda niseme punguza unafiki!
 
Dawa Ni Kuliacha Litukane Sana, Tusilifungie.. (Hapa nimetetea upande WA serikali, mgao ukiingia usinisahau, uje PM)
 
Kwa observation yangu gazeti hili ni kama vile linataka kufa lakini halitaki kufa kifo cha asili yaani kwa kukosa wanunuzi.

badala yake gazeti hili limeamua kufanya makosa mfululizo ili mkono wa sheria ulishukie na kulifungia pengine kutengeneza kiki ya chama flani.

Ukiwa mwerevu na mfuatiliaji utagundua kuwa gazeti hili haipiti wiki bila kufanya blunder.

Je nini ushauri wako kwa gazeti hili na serikali?
Kama hujaorodhesha makosa hujalitendea haki gazeti.
 
hoja itafifia kwa mvivu wa kusoma.
Ungekuwa ni GT na msomaji wa magazeti usingeshindwa kuelewa hoja rahisi namna hii.Au labda niseme punguza unafiki!
Utakuwa na tatizo upstairs. Hili andishi lako umemletea nani hapa? Utakuwa na tatizo kwa kuwa unadhani akili yako ni sawa na akili za wengine! Yaani wewe kwa vile kila siku unasoma Tanzania Daima kwa nia ovu ya kuvizia makosa unataka wote tuwe na utaratibu kama wako ? Umetushirikisha tuone "udhaifu" wa Tanzania Daima huku huo unaodai kuwa ni "udhaifu" wenyewe unabaki nao mfukoni mwako halafu unatuambia tukautafute then turudi hapa kujadili na wewe. Nenda zako Bashite mkubwa....!
 
Kwa observation yangu gazeti hili ni kama vile linataka kufa lakini halitaki kufa kifo cha asili yaani kwa kukosa wanunuzi.

badala yake gazeti hili limeamua kufanya makosa mfululizo ili mkono wa sheria ulishukie na kulifungia pengine kutengeneza kiki ya chama flani.

Ukiwa mwerevu na mfuatiliaji utagundua kuwa gazeti hili haipiti wiki bila kufanya blunder.

Je nini ushauri wako kwa gazeti hili na serikali?

Tanzania Daima ni gazeti la Chama cha siasa yalivyo Uhuru,tazama na Jamuhuri.Since ni ubaya likiandika habari za chama husika ni kama Uhuru,Tazama na Jamuhuri linavyoandika habari Chama husika.

Ikiwa Magazeti ya Chama cha Mapinduzi ayaishi kutukana na kudhalilisha Viongozi wa vyama vingine vya siasa na hayafungiwi sioni kwanini gazeti la chama kingine cha siasa lifungiwe sababu halijaandika front page Mwenyekiti wa Chama Cha Mauaji.

Kuna vitu mnaweza kuvijadili siyo issue za kipumbavu kama hizi.

Sinunui gazeti lolote la chama cha Mauaji hata kusoma taarifa zake kwa sababu siliamini lakini sioni kwanini lifungiwe kwa sababu tu silipendi.

Hata ukienda kutolewa unaolewa na unayempenda.Usiyempenda humgusi.Sawa na Tanzania Daima hulipendi unalinunua la nini?Nunua Magazeti unayoyapenda na kuyaamini.Tupatie UHURU wa kununua na kusoma Magazeti tunayoyapenda.
 
Utakuwa na tatizo upstairs. Hili andishi lako umemletea nani hapa? Utakuwa na tatizo kwa kuwa unadhani akili yako ni sawa na akili za wengine! Yaani wewe kwa vile kila siku unasoma Tanzania Daima kwa nia ovu ya kuvizia makosa unataka wote tuwe na utaratibu kama wako ? Umetushirikisha tuone "udhaifu" wa Tanzania Daima huku huo unaodai kuwa ni "udhaifu" wenyewe unabaki nao mfukoni mwako halafu unatuambia tukautafute then turudi hapa kujadili na wewe. Nenda zako Bashite mkubwa....!
Hajui kuna watu tunaamka na kusoma New York Times na Wall Street Journal kila siku na hayo magazeti kama "Tanzania Daima" ukiongelea kama tunayasoma kila siku ni kama unatuonea tu.
 
Tanzania Daima ni gazeti la Chama cha siasa yalivyo Uhuru,tazama na Jamuhuri.Since ni ubaya likiandika habari za chama husika ni kama Uhuru,Tazama na Jamuhuri linavyoandika habari Chama husika.

Ikiwa Magazeti ya Chama cha Mapinduzi ayaishi kutukana na kudhalilisha Viongozi wa vyama vingine vya siasa na hayafungiwi sioni kwanini gazeti la chama kingine cha siasa lifungiwe sababu halijaandika front page Mwenyekiti wa Chama Cha Mauaji.

Kuna vitu mnaweza kuvijadili siyo issue za kipumbavu kama hizi.

Sinunui gazeti lolote la chama cha Mauaji hata kusoma taarifa zake kwa sababu siliamini lakini sioni kwanini lifungiwe kwa sababu tu silipendi.

Hata ukienda kutolewa unaolewa na unayempenda.Usiyempenda humgusi.Sawa na Tanzania Daima hulipendi unalinunua la nini?Nunua Magazeti unayoyapenda na kuyaamini.Tupatie UHURU wa kununua na kusoma Magazeti tunayoyapenda.
Hili povu ndio linalotegemewa baada ya Tanzania Daima kufungiwa...Mwenendo wa gazeti lako la chama sio ushabiki wa siasa tu bali ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya uandishi.

ndio maana nikasema linafanya hivi ili kutafuta sababu ya kufungiwa...

sidhani kama kuna muandishi mwenye weledi atakubaliana na maudhui ya sasa ya Tanzania Daima ina all aspects.

Tanzania Daima halifanyi propaganda bali linafanya blunders
 
Back
Top Bottom