Gazeti la raia mwema mbinuzenu ni za kitoto za kuingamiza chadema

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Wakuu nimekuwa nikifuatilia Gazeti hili la Raia na nimeendelea kugundua kuwa gazeti hili halina nia nzuri na CHADEMA ninaamini lina makakati wa chini kwa chini wa kuibomoa CHADEMA. Kwa mfano leo limetoka na taarifa yenye kichwa cha habari SPIKA ANNE MAKINDA MATANI.

Baada ya kumalizia kuelezea jinsi Spika alivyojishushia hadhi kwa kushupalia posho gazeti limechomeka kuwa kambi ya upinzani imejadili posho hizo na kutetea posho mpya kwa kumtaja mmoja wa wabunge machachari ambaye pia ni mwanasheria amesema hakuchaguliwa kuwa masikini.

Kilichoniacha hoi zaida ni pale liliposema kuwa wanaopinga suala la posho ni Januari Makamba kwa CCM na Zitto kabwe kwa CHADEMA tu wengine wanawapiga vita, tumekuwatukimsikia John Mnyika ndani ya Bunge na nje ya bunge na Dr Slaa wakisisitiza kupinga ongezeko la posho nguvu zote wala hakuwataja wala hata kuchuakua hatua ya kuwauliza misimamo yao juu ya hayo aliyoandika.

Niwaambie tuu wanapoteza muda wao, sisi Watanzania wa leo si wale wa jana tumeamka kisawasawa tunasoma mapaka nyuso kabla hata hajazungumza.
 
Na generali ulimwengu yupo ndani ya hii njama?subiri nizitafute kwanza!
 
Ni moja ya magazeti ambayo hayako bias...ngoja niklinunue saa hii.Nitarudi
 
Mbona Gazeti la Raia Mwema limeeleza vizuri, ni kweli Chadema nzima anaepinga posho kwa vitendo ni Zitto Kabwe, peke yake..

Chadema acheni kulia lia kama watoto wadogo mnataka msifiwe tu.
 
wabunge wote wanalia njaa baada ya kukopa magari walihadiwa na mtoto wa mkulima na bi kiroboto wataongezewa posho zitawasidia kupunguza mkopo. Siku zinayoyoma.
 
Yaani kwangu hilo gazeti limepoteza mvuto kabisa. Yaani limekuja na mtindo ule ule wa RAI wakati ule likimpamba Kikwete. Yaani nimeamini kichaa huwa haponi. Yaani waandishi mahiri kama hawa wanarudia mambo ya kizamani!!!
 
Kumbe mlikuwa hamjafahamu bado? Basi kwa taarifa yenu, kuelekea 2015 raia mwema ni pro membe na kundi lake!
Mwanahalisi linaelekea kumbeba lowassa na timu yake .
Mwananchi itaangalia zaidi maslahi ya kenya kwenye kinyanganyiro hicho.
Na nyie wabongo mlio baki mtaendeleza ushabiki wenu kama kawa.
........... Ndio waliwao
 
Back
Top Bottom