Gazeti la Raia Mwema lafungiwa kwa siku 30

Alafu wakasema DC anadaiwa milioni 100,kumbe kashastaafu!ndio nimejua jana,bada ya Msigwa kusema,wengine tunafwatilia vichwa vya habari tu,hawa wamepewa adhabu ndogo,wangepigwa miezi mitatu.
 
📸Huyu hapa Msemaji Mkuu wa Serikali Ndugu Gerson Msigwa akitoa sababu za msingi za kulifungia Gazeti la Raia Mwema.

Tukumbuke kabla ya kulifungia Gazeti hilo, Tayari liliwahi kufungiwa mwaka 2017 kwa miezi mitatu kwasababu ya makosa yanayojirudia ya kuvunja sheria, kukiuka misingi ya uandishi wa habari, kufanya uchochezi wa mara kwa mara na kuchonganisha Serikali na wananchi wake.

Serikali imefikia hatua hii baada ya jitihada kubwa, za mara kwa mara na za muda mrefu za kuwaandikia barua kuwaonya, kukutana nao kuzungumza nao, kuwapigia simu, kuwakumbusha sheria na misingi, maadili na weledi wa taaluma ya uandishi wa habari lakini Gazeti la Raia Mwema limeendelea kuvunja taratibu hizo kwa makusudi kabisa.

Msikilize huyu hapa Msemaji Mkuu wa Serikali akieleza kwa undani sababu ya kulifungia Gazeti hilo.
 

Attachments

  • VID-20210905-WA0006.mp4
    54.3 MB
Back
Top Bottom