Gazeti la RAI lina maslahi Gani na CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la RAI lina maslahi Gani na CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KakaKiiza, Mar 3, 2011.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Mimi nimekuwa nikifuatilia habari na hasa kwenye magazeti ya hapa nchini!kwa bahati nzuri kuna Gazeti la RAI nguvu ya hoja nimekuwa nikishindwa kulielewa hasa kwa kipindi hiki cha takribani miezi miwili tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu hili gazeti limeshindwa kutoa taswila yake kwa jamii nakubaki kama gazeti la kifitini!!Tunajua ni gazeti la RA na mmliki wake ni kada wa CCM lakini kwanini limekuwa likiitia vidole serikali machoni??Na je lina maslai gani na CHADEMA??Au nimpango mahususi wakuibomoa CHADEMA kupitia vyombo vya RA?? Haiwezekani RAI ikaiandika vema CHADEMA??Au nikutujulisha kwamba kwasasa haliegemei sehemu yoyote??Linataka kurudisha nguvu yake ya zamani kabla yakumilikishwa kwa New Habari Cop??Tusaidiane kwa hili!
   
 2. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Kadiri siku zinavyokwenda kila mwenye macho anaona na kuangalia mbele, hivyo hao wamiliki kugawanyika au kuanza kutoa ukweli wa mambo si ajabu kabisa maana wanajua kuwa kesho CDM kesho CCM ,je CDM wakishika usukani wao watafanyaje??? kujihami huko si unajua tena kuuma huku una puliza?
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Waliona wakiiponda cdm watu hawanunui gazeti lao wakaamua kujoin them!
   
 4. c

  carefree JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Wamebaini gazeti ni wasomaji sasa kama utachapa gazeti halisomwi haina maana wanapata wkt mgumu sokoni thats y wameanza kujipopo
   
 5. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Gazeti linapaswa kuwa na maslahi ya chama au ya umma? soma theories of mass communication.
   
 6. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kuna tetesi kwamba eti lilikuwa linaghalamiwa na C.C.M kwa kiasi kikubwa kwa kificho kutokana kupata hasara ya kutouzika lakini kumetokea mfarakano wa kimalipo hivyo limeamua lijikite zaidi katika habari zinazoweza kulifanya lipate mauzo kutoka kwa jamii hii iliyobadirika kifikra. hivyo kwasasa lipo kibiashara zaidi.
   
 7. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana ya hili neno!!mass communication.swali walikuwa wapi mpaka wakapoteza mwelekeo??
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mh!ni vigumu sana kufahamu undani wa jambo hili,linahitaji uchunguzi wa kina!!
   
 9. M

  Marytina JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hata mimi nimeisikia hii.Eti baada ya ruzuku ya CCM kupungua mno na kwa sasa CCM inakabiliwa na ukata kama vyama vingine basi wameamua kuachana na ufadhili wa hili gazeti.
  Vimekuwepo vikao vingi kuhusu ni mkondo gani (umma au CCM) gazeti lisimame mwishowe wameridhia waiponde serikali ila wasimponde JK kama kiongozi wa hii serikali i.e JK aonekane anafanyiwa hujuma na maofisa wa serikali ?????ila sio JK kikwazo serikalini??????shangaaaaa
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Wameona gazeti halina soko, kwa hiyo wanarudi sokoni kwa kasi......
   
 11. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Hao Ndg Kiiza wamepoteza biashara saana walipokuwa wanandika ujinga wao.Swala si CDM,ila ni ujinga waliokuwa wanaandika watu wakajitoa kununua. Huyo mmliki ana angalia maswala ya fedha au gazeti lifirisike lifungwe!!!!!! Hivyo kwa usalama wao wameamua kunywa kloloquine ili wapone (wabaki kwenye soko) kuliko kufa na maralia (kufirisika)!!!
   
 12. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,084
  Likes Received: 15,721
  Trophy Points: 280
  labda wanataka kuibomoa au kuijenga CHADEMA. ila mie napenda waibomea CHADEMA ifie mbali kabisa.
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ikifa(kama inawezekana) itazaliwa kivingine
   
 14. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 853
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 80
  Uangalie tu kihoro kisije kikakuua!!!!!
   
 15. g

  geophysics JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  "Linataka kurudisha nguvu yake ya zamani kabla yakumilikishwa kwa New Habari Cop?" Pia ni mtikisiko wa uchumi kaka Kiiza.... Wakati wa uchaguzi walipewa pesa waharibu sehemu moja yaani upinzani... Sasa wameona wakiendelea kuharibu pesa hakuna...shirika litakufa maana sasa hivi watanzania ni wajanja...walio wengi wanajua ukweli ni upi na uongo ni upi...... wakiandika uongo gazeti lao halitanunuliwa...pesa mfukoni hakuna magazeti yote yanarudi kwa mchapaji.... Hivyo lazima wasome alama za nyakati kuona vipi watapata njia ya kuishi.... Mjini shule... Hivyo kwa sasa wanaangalia pesa tofauti na wakati ule walipokuwa na pesa...
   
 16. A

  Akiri JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Jumapili iliyopita nimenunua gazeti la Mtanzania , nikashangaa kwa jinsi walivyobadilika, waliandika habari bila upendeleo . na ndani ya hilo gazeti kulikuwa na makala kari ya jackton manyerere inayoelezea kifo cha ccm. inashangaza sana unapomkuta mwanahabari makini kama Balile anaamua kuvua taaruma yake ya habari na kuanza kuandika utumbo ulioegemea upande mmoja inashangaza sana. lakini kama wameamka na kuamua kufanya kazi kwa misingi ya kitaaluma tunawapongeza na tutawaunga mkono kununua magazeti yenu. safi Rose kitwage
   
 17. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Vipi kuhusu Tanzania daima na uongozi wa Kikwete and habari zinazohusu CCM? Je mizani inabalance? au Chadema juu hata kama imedondoka. Lisome vizuri kisha tupe hoja.
   
 18. f

  furahi JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ukiona gazeti linapambwa na Clouds Fm kwenye uchambuzi ujue hilo ni la CCM. Hadi sasa Gazeti lenye uhai ni Mwananchi/The Citizen tu. Mengine yote yameshachakachuliwa
   
 19. CPU

  CPU JF Gold Member

  #19
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Chadema inaweza kufa kwa jina tu, kwa matendo watakuwa hai milele
   
 20. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kuna masuala mengi ambayo yanaweza yakafanya chombo kama Rai kupoteza mwelekeo wake. Jenerali Ulimwengu, mnamo mwaka jana aliwahi kuandika kwamba kuna 'Waandishi Feki' wa habari sometimes huweka kando akili zao timamu (hasa wakati wa uchaguzi) na kuingia katika siasa chafu ili wapate chochote. Uchaguzi ukishaisha hurudi katika akili zao timamu na kuandika kile ambacho walikiacha. Waandishi hawa feki ni wengi, hasa kwenye magazeti ya sirikali, sisiemu na New Habari. New Habari ina baadhi ya Watu ambao ni makini (mmojawapo ni Matinyi), ukiacha wachache ambao ni wachumia tumbo.
   
Loading...