Gazeti la RAi limepigwa stop kuuzwa leo

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383
Taarifa zilizozagaa mjini na kwingineko ni kwamba Gazeti la RAI Nguvu ya Hoja la leo Machi 14 limepigwa pini na wakubwa ndani ya chama cha mapinduzi lisiuzwe mitaani na kuna maagizo kuwa lichomwe moto mara moja ili habari hiyo 'chafu' isiendelee kutamalaki mitaani.

Kama hujabahatika kuliona Gazeti hilo leo pole yako lakini wale ambao tumeliona na kupata nakala limeandika habari kubwa isemayo LOWASA 'AMSEMA' POLE POLE,habari hiyo ina picha ya Lowassa mwenyewe na pembeni picha ya pole pole.

Mtu aliyezungumza nami amesema habari hiyo imewakera sana wakubwa ndani ya Chama kubwa na kuagiza memejimenti ya RAI kuhakikisha gazeti hilo lisiingie mitaani.

Wauza magazeti Jijjini Arusha na Moshi walipokonywa magazeti hayo leo Alfajiri wakielezwa kuna maelekezo kutoka Juu kwamba hakuna kuuza gazeti la RAI na sasa Gazeti hilo litachapishwa upya na kuuzwa wiki ijayo lakini bila habari ya Lowassa.

Kwenye habari hiyo Lowassa akiwa Monduli ameelezea jinsi Pole Pole alivyokuwa akimsema vibaya kwenye luninga baada ya kuwa nje ya chama hicho tangu mwaka 2015 baada ya kutupwa nje na CCM kwenye mbio za urais na baadaye kukimbilia Chadema kujaribu bahati yake ambako nako aliangukia pua.

Sasa tusubiri kitakachotokea huko RAI,je Rostam atakinukisha kwa walioruhusu habari hiyo ichapishwe ama itakuwaje?,ni suala la muda
 
Screen shoot hiyo habari! iwe kumbukumbu ya daima
 
Hadithi za abunuasi hizi, umeliona gazeti hata kupiga photo tukaona japo heading.
 
Dawa ya tatizo sio kulikimbia au kulizuga bali ni kulitatua because what goes around comes around.
 
Hilo hapo
 
Attachments

  • LOWASA.jpg
    LOWASA.jpg
    100.7 KB · Views: 35
Ha ha ha ha ha
Hii ndiyo serikali ya CCM kila kitu kinaendeshwa kichama chama. Hao jamaa wapo ladhi hata kuua au kumfunga mtu maisha kulinda chama chao.
 
Back
Top Bottom