Gazeti la mwananchi vipi?

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
1,241
251
Toleo la leo 'Mwananchi' kuna habari wameandika, 'Kigogo wa CCM mbaroni kwa tuhuma za mauaji ' lakini hawakumtaja jina, wanaogopa nini? Mbona gazeti la wenyewe wenye nchi wamemtaja? The Daily news wameandika, 'POLICE have arrested the CCM Rukwa Regional Ideology and Publicity Secretary, Mr Patrick Maufi (48), for allegedly beating his wife to death'.
 
Duuuu kazi ipo!!! Lakini nji hii unaweza kuta sa hii yupo mtaani anagonga bia na kujisifu kuwa serikali ipo mfkoni mwake
 
basi kumbe jibu ulishalipata..

na kingine hilo gazeti walishasema lina tabia za kimbea zaidi wakipewa 10000 wao wanaandika jinsi mtoa hela kawaambiaje..
 
Mimi nilishaachaga kulinunua hilo gazeti toka mwaka jana, sana sana huwa nalinunua kwa ajili ya katuni za Masudi Kipanya.
 
Mbona hiyo ya kutotaja majina ndio zao kwa Mwananchi? Nimeishasoma mara mbili ama tatu ambapo Mtu amemfanya vibaya mtoto lakini jina lake linahifadhiwa nagazeti hilo huku magazeti mengine yakimtaja wazi!! Sijui ndio woga ama ni kutojiamini tu???
 
Nadhani wamelewa umaarufu sasa wanajisahau..Hawajui kwa nini Gazeti lililokuwa linaitwa mfanyakazi na umaarufu wake miaka ya 90 limetoweka imebaki historia .Pia kwa nini nipashe linaporomoka kila kukicha...
 
aise nipo sumbawanga jamaa kamuua mkewe baada ya kufuma sms za mapenzi ni hatari
 
Ni kweli hata miimi nimesoma hiyo story hawajatoa jina kabisa hapo au ndo ule msemo uliosemwa kwamba kuna baadhi ya pesa zimeandaliwa na Chama Cha Mafisadi nchini katika uchaguzi wa Igunga kuwahonga waandishi?Nadhani itakuwa hiyo tuu haiwezekani wafanye upuuze kama ule jamani kwa Gazeti kubwa kama lile nchini
 
Ajali ya Zanzibar wale wataalam kutoka South Afrika wamechemka bwana kisa kina kirefu si mchezo jamani kwa hiyo ndugu zetu bado wako kwenye maji huko chini hadi sasa.Hii ndo serikali tunayoikubali hadi sasa tutafanyeje kiasi kwamba hata nahodha hawamjui na mmiliki pia,tutatoka kweli hapo?
 
Ni kweli hata  miimi nimesoma hiyo story hawajatoa jina kabisa hapo au ndo ule msemo uliosemwa kwamba kuna baadhi ya pesa zimeandaliwa na Chama Cha Mafisadi nchini katika uchaguzi wa Igunga kuwahonga waandishi?Nadhani itakuwa hiyo tuu haiwezekani wafanye upuuze kama ule jamani kwa Gazeti kubwa kama lile nchini
 
...wanaogopa nini? Mbona gazeti la wenyewe wenye nchi wamemtaja? The Daily news wameandika
Majuzi nilichana gazeti immediately niliposma ripoti yao ya timbwili la Makongoro Nyerere againts magamba. Wakasema "Makongoro ambae aliwataja kwa majina..." lakini Mwananchi hawakuwataja, I was like which dunderheads write the news in bongo? Makongoro aliwataja kwa majina, Nape aliwataja kwa majina, Chiligati aliwataja kwa majina, LOWASSA, CHENGE, ROSTAM...nini cha kuogopa?
 
Wazee jamaa ananyie debe till now na issue hakuwa mke wake alikuwa ni mpango wa kando (nyumba ndogo yake) mke wake alifariki last 6 months
 
Back
Top Bottom