Gazeti la mwananchi ndani ya kashfa nzito ya ufisadi

ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,957
1,327
GAZETI LA MWANANCHI NDANI YA KASHFA NZITO YA UFISADI..

WAKATI Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi,Mwananspoti na The Citizen, ikikabiliwa na tishio la wafanyakazi wake kuhamia Kampuni ya News Habari 2006, inayochapisha Magazeti ya Mtanzania,Rai,The African na magazeti ya michezo ya Dimba na Bingwa, Uongozi wa Kampuni hiyo unatajwa kwa kashfa nzito ya ufisadi, baada ya kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa maslahi dhidi ya Waandishi wa Habari wasiokuwa na mikataba ya ajira,(Correspondent).

Waandishi hao wameingia kwenye mgogoro huo na Kampuni hiyo, baada ya kupewa mikata feki ambayo walidai kuwa ni mikataba ya kifisadi,Wakizungumza na Habarimpya.com kwa nyakati tofauti, huku wakitoa masharti ya majina yao kutotajwa mtandaoni walisema kwamba, Mwananchi imekuwa ikifanya ufisadi mkubwa katika suala la maslahi ya waandishi wa Habari wasiokuwa na mikataba ya ajira kwa kipindi kirefu

"Uongozi wa MCL umekuwa ukifanya ufisadi mwingi katika maslahi ya Corespondent, ambao ndiyo wanaochangia mapato ya Kampuni kwa kiwango kikubwa ni miaka mingi sana tumekuwa tukilalamikia maslahi yetu, Correspondent tunalipwa kulingana na kazi tunazozifanya lakini cha kushangaza ni kwamba, hatujui kiwango sahihi cha pesa tunayolipwa kwa kila habari moja tunayoandika, ama kila picha moja inayotoka kwenye gazeti,"alisema mmoja wa waandishi hao.

Mwandishi mwingine ambaye pia alionyesha kukerwa na kile walichokiita kuwa ni ufisadi alisema kwamba,Kampuni hiyo imekuwa ikijigamba kwamba waandishi wao hawaruhusiwi kupewa nauli ama hata bahasha za maji ya kunywa, kutoka vyanzo vyao vya Habari kama ilivyo zoeleka kwa tasnia ya habari Tanzania (Mshiko), kwa kutangza kwenye magazeti yao huku waandishi wao wasiokuwa na mikataba ya ajira, wakiendelea kufanyakazi bila kujua kiwango sahihi cha malipo ya kazi zao.

"Kila mara tunatangazwa kwenye magazeti yao, kwamba haturuhusiwi kuchukuwa bahasha yoyote kutoka kwa wadau wetu wa habari, kwa madai kwamba hiyo ni rushwa na kwamba wao hawanunui habari bali wanauza habari, lakini sisi kama waandishi tunaishi kwa shida huku watu wachache wakineemeka kupitia kazi zetu, ukianza kuhoji undani wa maslahi yako unaishia kufukuzwa kazi,pili tunafanyakazi bila mikataba yoyote na baada ya kudai hilo kwa kipindi kirefu wakaleta mkataba mpovu, ambao kama ungetolewa na taasisi nyingine, wangeandika habari katika ukurasa wa kwanza kwa maandishi makubwa ya Ufisadi wa kutisha,"alisema mwandishi huyo kwa huzuni, huku akimwomba mwandishi wa Habarimpya.com nauli ya kurudi nyumbani kwao baada ya kutoka ofisini.Taarifa za ndani kutoka katika Kampuni hiyo zinadai kwamba, Correspondent wengine wamekuwa wakifukuzwa kazi bila kujali ni muda gani waliokaa ndani ya Kampuni hiyo, wala mchangao wao.

"Kuna waandishi wamewahi kufukuzwa kazi hapa kwa madai kwamba, Kampuni inapunguza wafanyakazi ili wabakize wafanyakazi wacheche watakaoweza kulipwa mishahara mizuri, lakini ukweli ni kwamba watu wengi wanafukuzwa kwa majungu baada ya kudai maslahi yao.

Uchunguzi uliofanywa na Habarimpya.com kuhusu maslahi ya waandishi katika Kampuni hiyo unaonyesha kwamba, kati ya mwaka 2009 hadi 2013 zaidi ya waandishi 30, waliofanya kazi katika Kampuni hiyo bila kuajiriwa kati ya miaka mitatu hadi mitano, wamefukuzwa kazi baada ya kudai maslahi yao. Chat Room Baadhi ya Waandishi waliowahi kufukuzwa kazi katika kipindi hicho ni pamoja na,Mussa Mkama,Gidius Rwiza,Ummy Muya,Aziza Nangwa,Patricia Kimelemeta (huyu alifanyakazi zaidi ya miaka saba),Prisca Mussa,Nora Damian,Jesca Nangawe,Festo Polea,Frank Aman,Clara Alphonce,Icer Kimaro,Said Powa,Aziza Mosoud,Bakari Kiango na wengine wengi,wakati baadhi ya waandishi waliofukuzwa kazi ama kuacha kazi kwa majungu ni pamoja na Mwasu Sware,Joyce Mmasi (huyu baadaye aliajiriwa tena),Mwanamkasi Jumbe (baadaye alipelekwa idara ya matangazo),Mnaku Mbani,Josta Mwangulumbi,Kidanka,Sarehe Ally,Daniel Mbega na Machira.

Akizungumzia suala hilo mmoja wa Wahariri wa Habari wa Kampuni hiyo, aliyeomba jina lake lisiandikwe mtandaoni alisema kwamba,"Kiujumla mwenendo wa Kampuni hii kwa Correspondent, si sahihi hata kidogo, kwani hata sisi ambao tuko katika ngazi ya wahariri tumesha shauri sana lakini hakuna kinachofanyika,badala yake unashangaa kuona watu wanafukuzwa kazi kila wanapodai maslahi yao, kwakweli hili si jambo zuri hata kidogo, hatuoni sababu ya kukaa na mfanyakazi kwa zaidi ya miaka mitano kwa ahadi ya kumwajiri kisha unamfukuza kazi, baadaye una ajiri watu wengine kwa mshahara makubwa hii ni kinyume hata kwa sheria za nchi, tena kwa gazeti ambalo linaongoza kwa sera ya kutetea maslahi ya watanzania wengine huku watetezi wenyewe wakinyanyaswa kiasi hiki".

Oktoba mosi mwaka huu wafanyakazi hao walipewa mikataba ya makubaliano ya kufanyakazi kwa mara ya kwanza, huku ikiwa na mapungufu lukuki na wakitakiwa kuisaini haraka ili utekelezaji wake uanze Oktoba 15 mwaka huu, moja ya mapungufu makubwa yaliyowashangaza waandishi hao ni pamoja na kiwango cha malipo ya kazi zao, ama mshahara wao kutotajwa katika mkataba huo wa makubaliano, sababu nyingine inayotajwa kwamba ni ufisadi ndani ya Kampuni hiyo ni kitendo cha mkataba huo ulioitwa wa siri kumtaka mwandishi kutojihusisha na kazi yoyote ya habari nje ya Kampuni hiyo.

Mkataba huo pia unamtaka mwandishi kutojihusisha na machapisho ya habari sehemu yoyote, ama kwa Kampuni yoyote ama kwa mtu yeyote anayefanya kazi zinazofanana na kazi za Mwananchi, wakati hawaja ajiriwa wala hawajui kiasi cha malipo yao kwa kila kazi wanazofanya, badala yake kila mwisho wa mwezi wanaambulia kati ya tsh 20,000 hadi 100,000, huku wakitakiwa kuandika habari mbili za kipekee (Exclusive Stories) kwa kila siku pamoja na makala mbili kila wiki ambazo hazijulikani kiasi cha malipo yake.

Habarimpya.com ilimtafuta Meneja Mwajiri wa Kampuni hiyo ambaye ndiye aliyesaini mikataba hiyo, Aika Masawe kupitia simu yake ya mkononi ambayo iliita bila kupokelewa.Hivi karibuni iliandikwa habari juu ya kuwepo kwa mikakati ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo kuhamia New Habari 2006, hata hivyo aliyekuwa mhariri wa Habarimpya.com wakati huo, kabla ya kuacha kazi aliambulia vitisho vingi kutoka kwa baadhi ya watu ndani ya Mwananchi.

-Habarimpya.com
 
Hili si kwa Mwananchi tu]

Fuatilia Tanzania Faina,Uhuru,Habari Leo & Daily News!

Huko kuna ufisadi wa kutupwa,mi kuna mdogo wangu ni mwandishi na alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya Daily News kwa miaka mitano hakuna alichopata!

Tangu nimemchukuwa na kumuwek kwenye masuala yetu ya Madini leo ana mwaka na nusu ana nyumba na magari!

Bado kuna unyanyasi mkubwa sana kwenye sekta ya habari nchini,waandishi wananyanyaswa sana na hasa wale wa mikoani!
 
Mleta mada ni mlamba viatu wa ZIMMWI KABWE,Zitto na mhariri wa mwananchi ni waskaji'_Mleta mada akili zako Zina tatizo
 
Umeanza kwa kusema wanatishio la waandishi kuwakimbia.............soko ni huria waende tu!
 
Mleta mada ni mlamba viatu wa ZIMMWI KABWE,Zitto na mhariri wa mwananchi ni waskaji'_Mleta mada akili zako Zina tatizo
Wewe ni kibaraka wa lema lazima uamini kuwa mleta ni mfuasi wa zitto. Ht ivo akili ya zitto peke yake ni sawa na kamati kuu nzima ya chadema kwa hiyo lazima awe na wafuasi wenye akili sio vilaza km ww
 
Mnaanza kuandikana sasa! Nasikia hata huko wanakotaka kwenda mshahara uwa unadundulizwa hata miezi 6, tena kwa wenye mikataba! Poleni.
 
Wewe ni kibaraka wa lema lazima uamini kuwa mleta ni mfuasi wa zitto. Ht ivo akili ya zitto peke yake ni sawa na kamati kuu nzima ya chadema kwa hiyo lazima awe na wafuasi wenye akili sio vilaza km ww

ivi chakavu huwa wanawalipa sh ngapi kwa hii kazi mnayoifanya ya kushinda hapa JF?
 
Haya makampuni ya watu shida tupu yamekuja kuchuma tu hapa kwetu ,we angalia hata kwenye hutu tu benki twa siku hizi kama tu saccos watu wanaambulia kuvaa vizuri tu eti kachomekea lakini ni wanyonyaji wakubwa sana mishahara kidonyo sana ajabu ,wao wanamake million(s) daily na kuzihamishia kwao huko ulaya lakini unashangaa mfanyakazi wao kutwa kupiga mizinga ya nauri hata kabla ya tar 20 ya mwezi.
 
Mbona hujasema kuwa mapato nayo yameshuka kwa asilimia 40.Sasa kama mnataka kuhamia kwenye neema mnasubiri nini ati? mfukuzwe kama Nchimbi na wenzie.
GAZETI LA MWANANCHI NDANI YA KASHFA NZITO YA UFISADI..

WAKATI Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi,Mwananspoti na The Citizen, ikikabiliwa na tishio la wafanyakazi wake kuhamia Kampuni ya News Habari 2006, inayochapisha Magazeti ya Mtanzania,Rai,The African na magazeti ya michezo ya Dimba na Bingwa, Uongozi wa Kampuni hiyo unatajwa kwa kashfa nzito ya ufisadi, baada ya kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa maslahi dhidi ya Waandishi wa Habari wasiokuwa na mikataba ya ajira,(Correspondent).

Waandishi hao wameingia kwenye mgogoro huo na Kampuni hiyo, baada ya kupewa mikata feki ambayo walidai kuwa ni mikataba ya kifisadi,Wakizungumza na Habarimpya.com kwa nyakati tofauti, huku wakitoa masharti ya majina yao kutotajwa mtandaoni walisema kwamba, Mwananchi imekuwa ikifanya ufisadi mkubwa katika suala la maslahi ya waandishi wa Habari wasiokuwa na mikataba ya ajira kwa kipindi kirefu

"Uongozi wa MCL umekuwa ukifanya ufisadi mwingi katika maslahi ya Corespondent, ambao ndiyo wanaochangia mapato ya Kampuni kwa kiwango kikubwa ni miaka mingi sana tumekuwa tukilalamikia maslahi yetu, Correspondent tunalipwa kulingana na kazi tunazozifanya lakini cha kushangaza ni kwamba, hatujui kiwango sahihi cha pesa tunayolipwa kwa kila habari moja tunayoandika, ama kila picha moja inayotoka kwenye gazeti,"alisema mmoja wa waandishi hao.

Mwandishi mwingine ambaye pia alionyesha kukerwa na kile walichokiita kuwa ni ufisadi alisema kwamba,Kampuni hiyo imekuwa ikijigamba kwamba waandishi wao hawaruhusiwi kupewa nauli ama hata bahasha za maji ya kunywa, kutoka vyanzo vyao vya Habari kama ilivyo zoeleka kwa tasnia ya habari Tanzania (Mshiko), kwa kutangza kwenye magazeti yao huku waandishi wao wasiokuwa na mikataba ya ajira, wakiendelea kufanyakazi bila kujua kiwango sahihi cha malipo ya kazi zao.

"Kila mara tunatangazwa kwenye magazeti yao, kwamba haturuhusiwi kuchukuwa bahasha yoyote kutoka kwa wadau wetu wa habari, kwa madai kwamba hiyo ni rushwa na kwamba wao hawanunui habari bali wanauza habari, lakini sisi kama waandishi tunaishi kwa shida huku watu wachache wakineemeka kupitia kazi zetu, ukianza kuhoji undani wa maslahi yako unaishia kufukuzwa kazi,pili tunafanyakazi bila mikataba yoyote na baada ya kudai hilo kwa kipindi kirefu wakaleta mkataba mpovu, ambao kama ungetolewa na taasisi nyingine, wangeandika habari katika ukurasa wa kwanza kwa maandishi makubwa ya Ufisadi wa kutisha,"alisema mwandishi huyo kwa huzuni, huku akimwomba mwandishi wa Habarimpya.com nauli ya kurudi nyumbani kwao baada ya kutoka ofisini.Taarifa za ndani kutoka katika Kampuni hiyo zinadai kwamba, Correspondent wengine wamekuwa wakifukuzwa kazi bila kujali ni muda gani waliokaa ndani ya Kampuni hiyo, wala mchangao wao.

"Kuna waandishi wamewahi kufukuzwa kazi hapa kwa madai kwamba, Kampuni inapunguza wafanyakazi ili wabakize wafanyakazi wacheche watakaoweza kulipwa mishahara mizuri, lakini ukweli ni kwamba watu wengi wanafukuzwa kwa majungu baada ya kudai maslahi yao.

Uchunguzi uliofanywa na Habarimpya.com kuhusu maslahi ya waandishi katika Kampuni hiyo unaonyesha kwamba, kati ya mwaka 2009 hadi 2013 zaidi ya waandishi 30, waliofanya kazi katika Kampuni hiyo bila kuajiriwa kati ya miaka mitatu hadi mitano, wamefukuzwa kazi baada ya kudai maslahi yao. Chat Room Baadhi ya Waandishi waliowahi kufukuzwa kazi katika kipindi hicho ni pamoja na,Mussa Mkama,Gidius Rwiza,Ummy Muya,Aziza Nangwa,Patricia Kimelemeta (huyu alifanyakazi zaidi ya miaka saba),Prisca Mussa,Nora Damian,Jesca Nangawe,Festo Polea,Frank Aman,Clara Alphonce,Icer Kimaro,Said Powa,Aziza Mosoud,Bakari Kiango na wengine wengi,wakati baadhi ya waandishi waliofukuzwa kazi ama kuacha kazi kwa majungu ni pamoja na Mwasu Sware,Joyce Mmasi (huyu baadaye aliajiriwa tena),Mwanamkasi Jumbe (baadaye alipelekwa idara ya matangazo),Mnaku Mbani,Josta Mwangulumbi,Kidanka,Sarehe Ally,Daniel Mbega na Machira.

Akizungumzia suala hilo mmoja wa Wahariri wa Habari wa Kampuni hiyo, aliyeomba jina lake lisiandikwe mtandaoni alisema kwamba,"Kiujumla mwenendo wa Kampuni hii kwa Correspondent, si sahihi hata kidogo, kwani hata sisi ambao tuko katika ngazi ya wahariri tumesha shauri sana lakini hakuna kinachofanyika,badala yake unashangaa kuona watu wanafukuzwa kazi kila wanapodai maslahi yao, kwakweli hili si jambo zuri hata kidogo, hatuoni sababu ya kukaa na mfanyakazi kwa zaidi ya miaka mitano kwa ahadi ya kumwajiri kisha unamfukuza kazi, baadaye una ajiri watu wengine kwa mshahara makubwa hii ni kinyume hata kwa sheria za nchi, tena kwa gazeti ambalo linaongoza kwa sera ya kutetea maslahi ya watanzania wengine huku watetezi wenyewe wakinyanyaswa kiasi hiki".

Oktoba mosi mwaka huu wafanyakazi hao walipewa mikataba ya makubaliano ya kufanyakazi kwa mara ya kwanza, huku ikiwa na mapungufu lukuki na wakitakiwa kuisaini haraka ili utekelezaji wake uanze Oktoba 15 mwaka huu, moja ya mapungufu makubwa yaliyowashangaza waandishi hao ni pamoja na kiwango cha malipo ya kazi zao, ama mshahara wao kutotajwa katika mkataba huo wa makubaliano, sababu nyingine inayotajwa kwamba ni ufisadi ndani ya Kampuni hiyo ni kitendo cha mkataba huo ulioitwa wa siri kumtaka mwandishi kutojihusisha na kazi yoyote ya habari nje ya Kampuni hiyo.

Mkataba huo pia unamtaka mwandishi kutojihusisha na machapisho ya habari sehemu yoyote, ama kwa Kampuni yoyote ama kwa mtu yeyote anayefanya kazi zinazofanana na kazi za Mwananchi, wakati hawaja ajiriwa wala hawajui kiasi cha malipo yao kwa kila kazi wanazofanya, badala yake kila mwisho wa mwezi wanaambulia kati ya tsh 20,000 hadi 100,000, huku wakitakiwa kuandika habari mbili za kipekee (Exclusive Stories) kwa kila siku pamoja na makala mbili kila wiki ambazo hazijulikani kiasi cha malipo yake.

Habarimpya.com ilimtafuta Meneja Mwajiri wa Kampuni hiyo ambaye ndiye aliyesaini mikataba hiyo, Aika Masawe kupitia simu yake ya mkononi ambayo iliita bila kupokelewa.Hivi karibuni iliandikwa habari juu ya kuwepo kwa mikakati ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo kuhamia New Habari 2006, hata hivyo aliyekuwa mhariri wa Habarimpya.com wakati huo, kabla ya kuacha kazi aliambulia vitisho vingi kutoka kwa baadhi ya watu ndani ya Mwananchi.

-Habarimpya.com
 
Waandishi wa habari Tanzania wameacha nyumba zao zinateketea kwa moto wamekimbilia kuzima moto nyumba za majirani. mi nawaona kama ccm vile. wanaumaskini mkubwa wa akili.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom