Taifa linapoteza pato kubwa kutoka katika ukwepaji wa kodi wa mgodi huu,kuna manyanyaso kwa wafanyakazi wazalendo kwani wanachukuliwa kama mbwa ndani ya migodi, kuna tofauti kubwa na ubaguzi wa wazi wazi kati ka ngozi nyeupe na sisi weusi.
Kuna uharibifu mkubwa wa mazingira na umwagwaji wa sumu unaoingia kwenye vyanzo vya maji na mazingira.
Na namna ya kuyaziba mdomo yote haya ni hongo kwa magazeti yetu likiwemo Mwananchi linalojinadi kama liko mstari wa mbele katika kuweka wazi mambo yanayoendelea.
Yaani wewe unajiita mzalendo halafu unafumbia macho uozo huo mkubwa kazi yako ni kuja kulaumu gazeti tu? Kama wewe umeshafanya nini kuexpose mambo hayo ukiwa na ushahidi?