kakuruvi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2009
- 770
- 258
Nasoma gazeti la Mwananchi hapa la leo ukurasa wa tatu kuna kichwa cha kidogo cha habari ''historia ya Dar es Salaam'' nimepitia orodha ya watu waliowahi kushika Umeya wa Dar, nagundua kwamba mwandishi hajakidhi kichwa cha habari kwani bora angesema baadhi ya ya watu waliowahi kushika Umeya wa Dar ingekuwa sawa lakini kutaja majina hayo yote umsahau Meya Ramadhani Nyamka, umsahau Meya Kitwana Kondo, hao wawili ni miongoni mwa Meya waliowahi kuwa mashuhuri na wenye ushawishi mkubwa ndani ya jiji hili.