#COVID19 Gazeti la Mwananchi mmepotosha kuhusu dawa ya kutibu Uviko-19

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,222
5,946
Habari hii iliyoandikwa kwenye gazeti la Mwanachi mtandaoni ina upotoshaji mkubwa. Dawa ya molnupiravir imekuwepo kwa mda sasa ikitumika kuwasaidia wagonjwa wanasumbuliwa na maambukizi ya virusi.

Wataalamu walichofanya ni kuitumia dawa hiyo kwa wagomjwa wa UVIKO 19 na wala si kugundua kama Mwananchi wanavyotaka kutuaminisha.
===

Jaribio la wanasayansi kubaini dawa ya homa ya Uviko-19 linaelekea kuzaa matunda baada ya kuwapo kwa taarifa za matumaini makubwa vidonge vya ‘Molnupiravir’ kufanya kazi kwa ufanisi kutibu ugonjwa huo.

Dawa hiyo iliyofanyiwa majaribio na kampuni ya kimataifa ya kutengeneza dawa ya Merck iliyopo nchini Marekani inaweza kuleta suluhu katika kupatikana kwa dawa ya Uviko-19.

Taarifa iliyotolewa na jana na mtandao wa euronews, wagonjwa 775 waliofanyiwa majaribio kupitia dawa hiyo wamepona kikamilifu na sasa kampuni hiyo, inasubiri idhini ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Marekani (FDA) ili ianze kutumika nchini humo.

Kulingana na wanasayansi dawa hii inaweza kupunguza vifo kwa kiwango kikubwa zaidi.

Kampuni hiyo imetengeneza kidonge cha kwanza kinachosemekana kuwa bora dhidi ya virusi hivyo na endapo watapewa idhini dawa hiyo aina ya ‘Molnupiravir’ itakuwa ya kwanza kutibu Uviko-19.

Mwanasayansi Peter Hotez kutoka kampuni hiyo amesema, “Majaribio ya kliniki yanaonyesha kuwa dawa hii ina uwezo wa kufikia idadi kubwa ya watu ikilinganishwa na matibabu ya hivi sasa ya kingamwili ya ambayo hutumiwa kwa kawaida. Katika matumizi dawa hii mgonjwa anapewa kipimo cha vidonge viwili kila siku kwa siku tano.”

Wanasayansi wanasema dawa hiyo ina viwango vya juu vya kuishi kwani hakukuwa na vifo vilivyoripotiwa kwa walioitumia kwenye majaribio ya kliniki.

Kwa mujibu wa mtandao huo, kidonge hicho kinatarajiwa kupatikana nchini Marekani na kitapatikana kote ulimwenguni mwishoni mwa mwaka huu.

Mapema wiki jana, Marekani pia ilianza majaribio ya dawa inayolenga kuwalinda watu wanaoishi na mtu aliyeambukizwa virusi vya ugonjwa huo kwa watu 2,660 ikiwa ni miezi 13 tangu kupatikana kwa chanjo ya ugonjwa huo.

Kutokana na ujio wa dawa hiyo, watafiti mbalimbali wamesema kuwa iwapo dawa hiyo itafaulu, dunia itapata tiba na kutakuwa na uwezekano mkubwa kudhibiti virusi vya Uviko-19 kabla havijaenea zaidi na kuwa mbadala wa chanjo.

Dawa hizo za kumeza zilizotengenezwa na Kampuni ya kutengeneza dawa nchini Marekani ya Pfizer, pia imelenga kuwazuia wasio na dalili zozote za maambukizi dhidi ya kupata virusi hivyo.

Mkuu wa Utafiti wa kisayansi kwenye kampuni hiyo, Dk Mikael Dolsten alisema dawa hiyo itafanyiwa majaribio kwa watu 2,660 wenye umri wa kuanzia miaka 18 wenye afya njema na wanaoishi nyumba moja na mtu aliyepata maambukizi ya ugonjwa huo.
 
Back
Top Bottom